Story: Bora Mchaga Mwizi Kuliko Mpare Bahili....

Money Penny

JF-Expert Member
Jun 20, 2016
15,743
14,667
WACHAGAAAA MPOOOOOOO


SHIMBONI SHAFOOO WACHAGAAAAA... HAYA MMESHAHESABIWAAA MKUJEEE HUKU TUWEKANE SAWAAA.... MAISHA YAMEBADILIKAAAA SASAAAA MFANYE KAZIIII KWERI KWERIII


KIRU

Haya sasa wale wachaga mkujeee Kyalow kapeace binti kiziwi Mwifwa Principal Focus mahalipema mahondaw BAK bakalemwa milembe Bak byzo I.T bakar shomar bakalemwa milembe Bakari Abbasi Behaviourist Karucee karagwe2005 Karakwende karunda GuDume Jitu jeusi emmyta
Binti Magufuli Binti Kirembwe Binti Kagundo binti miss Naantombe Mushi Shunie Dinazarde Mwifyusi espy Mzigua wa kuchovya Mzigua90 Don Clericuzio Don Chunu Don arl Don Alaba JITU LA MIRABA MINNE



Mashemeji zangu mkujeee Tarime Tarime one Ngosha Mashine Daby for life Evelyn Salt evelyne dnd Mtoto halali na hela mtoto matataa Mtoto mkubwa mtoto mrito Mtoto mkubwa Mtoto mtukutu Mtoto Wa Africa mtoto mtafutaji
mshana jr mshana mouddy
gemmanuel265 mysterio My son My Son drink water Kete Ngumu keteka ketete Mungu Mweusi Munguwatosha Mungura maila salaniatz Vladmir Putin Jiwedogo Avatar mok Demiss NJOGHOMILE Granta zombi lindunduru Tantaw Nokia83 Beira Boy Consultant sumbwi Quinn mayenga Mpagani KakaKiiza Good Guy Good Guy NEIGHBOUR jje's popoma Madame S MadameX Madame B john agrey John Elia Smart Mwaki smart mind69 Smart Technician Smart911


SEHEMU YA 1

A. MAMA SITAKI KUOLEWA NA WACHAGAA







MANKA:

Yani mama mimi sipendi kabisa kuolewa na hawa ma shemeji zako wa kichaga, unajua sielewi kwanini uliolewa nao mama; kwanza ilikuwaje ukaolewa na wachaga!?


Mama Manka: ah acha tu mwanangu, ila baba yako nampenda sana


Manka: du kweli una moyo! sio kwa maisha haya tunayoishi asee. Mzee ana hela ana mali lakini tunaishi kama mafukara machokoraa wa kutupwaa!


Angalia familia ya akina Eliza na akina Ngosha pale angalia akina Lulu wanavyoishi.

Huyu Mumeo sijui yupoje!? kwanza amerudi? maana akiniskia nitakomaa


NKAKENI: kwanza Mama hii Tabia ya Baba kila akirudi nyumbani watoto tunamwogopa kama Mungu ni nini lakini?!


Kwanini tusiwe kama akina Ngosha Baba yao akija tu wanamkimbilia wanamkumbatia wanaenda nae ndani.

Sisi Baba akija kila mtu anakimbilia kulala na hapo uwe umefanya homework zote umemaliza, Baba yako mzazi anakuwa kama shetani wa kuzimu bwana! Mimi haya maisha siyapendi hata kidogo yani wachaga nimewachukia hakuna mfano wake! siwapendi na sidhani kama nataka hata kuolewa nao, wanaanzaje labda? na ikitokea siku mmeamua kula mahari ya mchaga kisa mnanioza mimi, mtajiju, nitafanya mpango huo mtanikuta nimeshaolewa sehemu nyingineee... yani kuolewa na mchaga! Bora nikaolewe na Mpemba au Mwarabu anigeuze jinsia lakini sio Mchaga, Never!


Manka: alafu Tabia ya kutulazimisha kwenda Moshi, kila mwezi wa 12 kama wafungwa nimeshachoka sitaki.. sasa hivi nimemaliza sekondari naenda chuo nataka uhuru wangu. Nimefaulu form 6 sawa naenda hapo Ifm kusoma kwanza nataka nikae hostel, niishi maisha ambayo Mungu amenipangia kuishi sio haya ya Mungu-shetani-Binadamu

Mungu akitokea shetani anakimbia

Shetani akitokea Binadamu anakimbia nimeshachoka Mama


Nataka nikienda chuo niende kujirusha nakula bata na kuku mzima, sio hapa nyumbani ni vipapatio tangu tupo wadogo mpaka wakubwa ni nini hiki?


Mimi mpaka sahivi sina bwana, sijui hata kupenda, sijui chochote kuhusu wanaume, wanaume nawaona kama mashetani maisha gani sasa haya!? yani wanaume siwapendi kwasababu ya huyu anayeitwa Baba yetu, mshenzi sana ni katili wa kufa mtu!


Nkakeni: kuhusu kula kuku, kwanza mpaka twende sabasaba au twende Moshi Krismas ndio tunakula paja na mgongo ila hapa nyumbani vipapatio kwenda mbele yani mama ni aibu sana!


Alafu Mama nimesahau kukwambia, nimepata mchumba Mama yangu, natamani nije kumtambulisha ila nawaza naanzaje, wakati baba namwona kama Chui


Mama; oh mwanangu umepata mchumba, jamaani hongera sana, anaitwa nani, kabila gani, anaishi wapi, anafanya wapi kazi? analeta lini mahari? !


Nkakeni: mahari?! Mahari nani analeta nimempiga stop staki mahari maana ni aibu na huyu baba yetu ushenzi mtupu! Mama sio kwa mateso ya hapa nyumbani

Huyu mzee ni dictator wa kufa mtu, alafu mama mumeo nitakuja mfanya kitu kibaya mpaka arudishe namba kwa Mungu!


Mama: kwaiyo unataka kumwuua baba yako?!


Nkakeni: simuui ila nitamfanya kitu mbaya mpaka ajute kuzaliwa ataondoka mwenyewe atuachie sisi tuishi vizuri.

watu tunaishi kama tupo mafia au Sudan kusini kwenye vita kumbe tunaishi kwa wazazi


Pendo: Hivi Mama, huyu mumeo anajua kupenda kweli?

Kwanza ulimpatia wapi maana wewe sio wa kabila hili wewe ni mtu wa Dodoma


Mama: mh jaman mbona mmeniandama hivi?!

Wewe Nkakeni unataka kuolewa wakati shule ndio kwanza form 4 umemaliza acha ujinga, soma mpaka chuo upate kazi. Baba yako hatopokea mahari bora umrudishe huyo mchumba wako


Manka: dada Pendo, unakumbuka tuliendaga Moshi juzi kati kwa ajili ya christmass, si shangazi akawa anaongea na marafkizake anawaambia wifi yake ni Chyasaka?!


Pendo & Nkakeni: eh niliskia nilitamani kumpiga shangazi na jiwe kama sio kaka kunistopisha! alinikera sana shangazi


Pendo: Hawa wachaga mimi siwapendi hata tone

Embu angalia Baba ana hotel 3 Dar es salaam. .. Ana hotel 1 Moshi. .. Ana nyumba 3 dar za kupanga, anafanya kazi serikalini ni boss lakini watoto wooote tumesoma shule za kayumba kuanzia vidudu mpaka chuo labda kama Nkakeni atapata bahati ya kusomeshwa shule za uzunguni za ulaya


Mimi kama dada yenu Pendo sitaki kabisa kusikia habari za kuolewa.


Kama wanaume wote wapo kama baba yangu, basi wakae na madyu dyu yao sitaki kabisa kuwaona! bora nife na bikira yangu nirudi Mbinguni niitwe Mtakatifu kuliko kumpa mwanaume usichana wangu alafu aje anitese kama Baba alivyomtesa Mama, sitaki huo ujinga hata kusikia!


Mama: akainama chini, mchozi ukaanza kumtoka mama wa watu, wakawa wanambembeleza ikabidi Mama yao afunguke kabla mumewe hajarudi


Unajua nimeumia sana pale Pendo aliposema hataki kuolewa tena imeniuma sana. Pendo naomba ufute hio kauli haraka sana maana itakutesa maisha yako yote hata kama utaolewa au laa


Miaka ya 70 nilipomaliza shule form 6, wazazi wangu wote walifariki katika ajali ya bus, wakitokea dodoma kwenda Dar.


Wazazi wangu walikuwa wanapendana sana sana sana hamna mfano wake!


Tangu hapo nikaja kulelewa na jamaa ya baba alikuwa Mchaga, alinitesa sana hakunijali alinifanya kama kijana wa kazi... kuamka asbh saa 12 kukatia ng'ombe majani na kurudi kukamua maziwa mpaka uje kunywa chai ni saa 4 asbh, chakula cha mchana saa 9 jioni cha usiku saa 5 usiku Kuamka asbh saa 10 asbh

Maisha yakawa magumu Elimu yangu ya form 6 ikaishia hapo hapo sikuweza kwenda national service wala wapi nikawa mkatia ng'ombe majani wa jamaa alienichukua.


Kwetu nimezaliwa mtoto peke yangu, sikuwa na ndugu na wazazi walipokufa nikabaki mwenyewe


Nikaishi na wale watu kwa muda wa miaka 5, siku moja akaja Baba yetu toka kijiji kingine cha huku Moshi, akaniona akanipenda akawa ananitaka mimi namkataa kwasababu sikuwahi kuwapenda wachaga kabisaa kwa yale mateso ya yule Baba na mkewe


Hapo natamani kutoroka sipati nafasi, kila nikijaribu nakamatwa basi nikakata tamaa nikaamua kukaa tu sasa sina msaada hakuna kitu, kanisani siendi maana nimeshakuwa dada wa kazi wa ile nyumba.


Nikaona bora nijifunzage na kichaga nikaanza kujifunza nikaweza!


Yule baba alienichukua aliniwekea ulinzi mkali na akahakikisha watu wote pamoja na majirani kuwa mimi ni mtoto wake.


Maisha ykawa yanazidi kuwa magumu kwangu kweli kweli, tena sana nikawa navumilia navumilia nahisi 40 yangu ikafikia tamati.


Siku 1, ilikuwa usiku wa mwaka mpya pale kijijini kwetu Kilimanjaro, wakawa wanachoma matairi shangwe za hapa na pale, wanapika pombe za makunduuu (makunduu ni ndizi za kupikia pombe )




Nikakaa kwenye kijiwe naangalia watu wanasherehekea mwaka mpya wa 1978

Sipo mbali na mlango wa nyumbani nikaamua kuonja na pombe ya makunduuu

Mara naskia mtu ananikaba shingo alafu akaniziba mdomo sikukumbuka kitu kingine tena baada ya hapo!


kuzinduka niko kwenye chumba nisicho kijua, kuna kitanda kimoja basi.

Nikajua naota nikarudia kulala, kuzinduka tena baadae kweli sipo nyumbani kwetu, nikaanza kupiga kelele;

Mara akaja kijana mmoja nisiemjua akanifokea unanini wewe mwanamke shida nini?!

Hujui kuwa umeshaolewa?!


Nikamwuliza nimeolewa?! kivipi?!


Kijana: nimekuoa jana usiku nimekuiba kwenye mkesha wa mwaka mpya na leo yameshapita masaa 18 yakifika 48 hawakuoni nyumbani basi wanajua ushaolewa


Eh kuskia hivyo nikapiga makelele zaidi, ili majirani waje lakini hamna cha majirani wala nini!

Kumbe kanificha porini hamna watu mpaka utembee km 5, alifanya makusudi akijua kule watanitafuta akaamua kunificha mbali.


Kweli masaa 48 yakapita kweli, nikawa rasmi mke wa mtu nisiemjua kwa kuibwa baada ya siku 3 nikarudishwa kijijini kwao Machame.

Nikakaa mke wa mtu, nina uchungu sina raha naona dunia yote imeniangukia mimi, kadri siku zilivyozidi kwenda nikaikubali ile hali kuwa basi nimeshaolewa! ila kwa yule bwana nilikuwa nimeruka majivu kwa kukanyaga motooo


Miezi 9 ikapita nikamzaa kaka yenu huko kijijini, baadae maisha yakawa magumu mume wangu ambae ni Baba yenu akaumwa sana karibu ya kufa, wazee wa baba yenu wakakaa kuumizana kichwa na kufanya maombi ya kimila wakajua aliniiba mkesha wa mwaka mpya, wakamwambia mrudishe mtoto wa watu ukamuoe vizuri kwa upya, uombe na msamaha umekosea sana, mizimu ya kwao inaita haraka arudishwe mtoto wa watu kwao.


Ndio hapo nikapona kwa kurudishwa kwa yule baba jamaa na kakaenu,


Yule baba alipotuona alifurahi sana na mke wake, wazee wakaongeaaa wakaomba msamaha yule baba alienilea akakubali akasamehe wakalipa faini ya ng'ombe 30, mbuzi 20 na kondoo 5, zikaletwa ndani ya siku 3, wakaomba dua, basi mume wangu akaanza kupona, baada ya wiki akawa mzima kabisa.


Wakatufungisha ndoa baada ya wiki 2 ndio nikaolewa sasa na baba yenu rasmi huku nimeshazaa mtoto wa kwanza kaka yenu


Baada ya siku 5 za mila na ndoa tukarudi kijijini kwetu Machame kwa mume pamoja na wazee na kakayenu..


Tulipofika baada ya mwezi mmoja Baba yenu akapigiwa simu amehamishiwa kikazi Dar es salaam ndio tukaingia Dar es salaam mwaka wa 79, kaka yenu akiwa na mwaka mmoja tukaingia kwa baraka za wazazi wote


Nyumba ya kwanza tulioishi ilikuwa Kijitonyama, tukaanza maisha hapo akazaliwa Pendo, ukaja Manka ukaja Nkakeni ndio tukahamia Upanga.


Tukaishi Upanga sana mpaka mwaka wa 2000 tukahamia Mbezi Beach enzi hizo Mbezi Beach ilikuwa hot cake sana, lakini ilikuwa inasikika kama Mbezi Beach ya majambazi


Ndio mpaka leo tupo hapa; mmezaliwa mmekulia, mmesoma Dar, wengine kuanzia nursery mpaka Chuo mpo hapa.

Ila ndio hivyo kuwachukia kwangu wachaga hakujasaidia maana ukatili niliofanyiwa na baba yenu ndio niliofanyiwa na baba mlezi wangu


Sikutamani kuolewa kabisa lakini nikaishiwa kuolewa na wachaga hao hao niliowachukia

Sasa nyie watoto mnataka kuleta mapinduzi yapi tena wakati maisha yenyewe ndio haya haya,


Zikubalini hali zenu jamani, acheni ujinga na tamaa watoto

Mnanicheka mimi angalau mimi nafaidi vinono kama kawaida

Baba yenu akiacha paja la kuku nakula.


Na nyie subiri mkiolewa mtakula vinono vyenu msinisumbue mimi


Pendo tema mate chini tafadhali, maneno yasijekukurudia! kiru... wai!


Maisha haya tulionayo ni mazuri sana kuliko yale niliokuwa naishi mimi.


Manka: haya sio maisha Mama, wewe ulivyokuwa na huyo mlezi wako ulikuwa unamwangalia kama Mungu flani na kumwogopa!?

Chakula hamli pamoja, mnawekwa jikoni, kumwona baba mpaka sikukuu haya ni maisha gani jamani Mama?


Mama: ndio, tena bora nyinyi mimi nilikuwa nakula jikoni na mbwa na ng'ombe si bora nyie mnakula chumbani kwenu au jikoni hapa pazuri kabisa!

Mshukuru Mungu basi na hivi mimi ni mama wa nyumbani hata sijui mtafanyaje.

Lkn angalau mmesoma mpaka chuo na kaka yenu anayo ajira angalau mtanisaidiaga huko baadae


Manka: Thats Bullshit Mama! naona Baba keshakuharibu na wewe umeshaanza kufanana nae, hapa lazima baba tumweke sawa haya sio maisha

Si ndio dada zangu au Mnasemaje? !


Mimi bado naendelea kusema sitakaa kuolewa na mchaga kama dada Pendo sijui Nkakeni. Mimi wachaga sitaki hata kuwaona na hapa wamenifuata wachaga kibao nimewakaaaajee sasa sipendi ujinga na ushenzi na wachaga kabisa mama.


Pendo & Nkakeni : ndio je, ngoja kaka aje tuongee nae tuongee na baba kuwa haya maisha hatuyataki tunataka kumfahamu Baba yetu

Sio kumwona Baba kama kituo cha polisi


Wote wakakubaliana kumpindua Baba yao huku wanacheka, Mama yao anawaangalia tu anajua hapa hamna kitu!

Mara wakasikia honi ya gari ikapigwa peeeeee peeeeeeee


Watoto wakapiga yowe Baba huyoooo basi kila mmoja akakimbia na njia yake kulala, nduki kitandani walishasahu wanataka kuongea na Baba yao.


Mama yao akacheeeeka, akajisemea kweli hapa bado sana akaenda kumkaribisha Mume wake, Mzee wa Kichaga!


KUENDELEA NA MOVI HILI BONYEZA BORA MCHAGA MWIZI KULIKO MPARE BAHILI.... - .


 
Huu uandishi wako una shout sana mama.... rekebisha mwandiko na font size.. wengine tupo traditional sana ukishaweka font size kubwa halafu ume bold unanitoa knock out kabisa siwez kusoma... ushauri tu
 
Karibu dear Shunie na Don Clericuzio niliwasahau hawa wanapenda sana story zako uwe unawapa link hata pm
Money Penny ni nani lakini woyoooooooo
Ujifunze kua mkweli Wa moyo wako .

Kinyume na hapo usipende kua Mnafiki au kujaribu kumpaka MTU matope.

Mwenzako ,alivyokua na anaendelea kua bize akishoot tamthiliya ,,Humu JF ulikua kinara Wa kumsema na wenzako kwa kila Lugha iliyombaya.

Karudi ,Unajifanya ,nyooooo nyooooo nyooooooo...

Nabahati nzuri ,Umemkuta Mdada wawatu Hajali your shits .

ACHA UNAFIKI .
 
Ujifunze kua mkweli Wa moyo wako .

Kinyume na hapo usipende kua Mnafiki au kujaribu kumpaka MTU matope.

Mwenzako ,alivyokua na anaendelea kua bize akishoot tamthiliya ,,Humu JF ulikua kinara Wa kumsema na wenzako kwa kila Lugha iliyombaya.

Karudi ,Unajifanya ,nyooooo nyooooo nyooooooo...

Nabahati nzuri ,Umemkuta Mdada wawatu Hakali your shits .

ACHA UNAFIKI .

kumbe alikuwa ananisema vibaya ee?

ahahahahaha KARMA IS THE MOST EXPENSIVE BEYAAAACH!

KWELI MIE NINA MUNGUUUUUU... TO GOD BE THE GLORY

 
Some people shud better take care of their mouthology .... Hizi rangi mbili rangi mbili hazifai sana aiseeeee.

Ndo unasikia ,,MTU anakuchekeaa uson kwako ,,once ukimpa kisogo nifulu kukutetaaaa dooooo!!

Wahivi ,siwapendi .

Sema nn ,, we Fanya kazi yako aiseeee as long as Only Few trustee friends are there !!.
 
Ujifunze kua mkweli Wa moyo wako .

Kinyume na hapo usipende kua Mnafiki au kujaribu kumpaka MTU matope.

Mwenzako ,alivyokua na anaendelea kua bize akishoot tamthiliya ,,Humu JF ulikua kinara Wa kumsema na wenzako kwa kila Lugha iliyombaya.

Karudi ,Unajifanya ,nyooooo nyooooo nyooooooo...

Nabahati nzuri ,Umemkuta Mdada wawatu Hajali your shits .

ACHA UNAFIKI .
Kwa akili zako nilijua tu hutaelewa alichoandika Evelyn Salt
 
Ujifunze kua mkweli Wa moyo wako .

Kinyume na hapo usipende kua Mnafiki au kujaribu kumpaka MTU matope.

Mwenzako ,alivyokua na anaendelea kua bize akishoot tamthiliya ,,Humu JF ulikua kinara Wa kumsema na wenzako kwa kila Lugha iliyombaya.

Karudi ,Unajifanya ,nyooooo nyooooo nyooooooo...

Nabahati nzuri ,Umemkuta Mdada wawatu Hajali your shits .

ACHA UNAFIKI .
Usipende kudandia usioyaelewa utakuja kubakwa
 
Back
Top Bottom