Story behind your date of birth

Story behind your date of birth

Mzizi Mbuzi na mshale wakiwa pamoja inakuaje?
Au mbuzi na mapacha
Au mapacha na ngombe?
Mkuu tracy Mwenye Nyota ya Mbuzi akiwa na nyota ya Mshale

watakuwa kila wakati wanagomban kwa sababu Nyota zao hazielewani hata kidogo. Na

Mwenye Nyota ya Mbuzi akiwa na Mwenye Nyota ya Mapacha watakuwa uelewani wao ni

mdogo sana. Na Mwenye Nyota ya Mapacha Na Mwenye Nyota ya Ng'ombe hawataelewana

kimapenzi itakuwa kuna ugomvi usio kwisha hapo. Ni Hivi Mkuu:

MAELEWANO YA NYOTA KINDOWA NA MAPENZI NA BIASHARA NA KUSHIRIKIANA KIMAISHA .

Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya
(CAPRICON) Mbuzi anaweza kuelewana na Mwenye Mtu Nyota ya Kaa (Cancer)

Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya (
SAGITTARIUS)Mshale Atakuwa na Maelewano na Mtu Mwenye Nyota Ya Mapacha. (Gemini)

Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya (Aries)Punda Atakuwa na Maelewano na Mtu Mwenye Nyota ya (Libra)Mizani

Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya NG'OMBE (TAURUS)Atakuwa na Maelewano na Mtu Mwenye Nyota ya (Scorpio)Nge

Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya (Leo)SimbaAtakuwa na Maelewano na Mtu Mwenye Nyota Ya Ndoo (AQUARIUS)


Mwanamme Au Mwanamke Mwenye Nyota ya (Virgo)Mashuke Atakuwa na Maelewano na Mtu Mwenye Nyota ya Samaki (PISCES).





 
Yangu ni tarehe 26 oktoba,inakuaje hapo?

Je,mimi naendana na mtu mwenye nyota ipi tarehe yangu ni 26 oktoba?
Cc:mzizimkavu

Mkuu Nikukumbushe Angalia Maisha yako yote ya baadae hapo .

NYOTA YA NG'E (SCORPIO)


  • Hii ni nyota ya 8 katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 23 October na 21 Novemba ya mwaka wowote.
  • Sayari yao ni MARS (MARIIKH).
  • Siku yao ya Bahati ni Jumanne.
  • Namba yao ya bahati ni 9.
  • Rangi ya bahati ni Nyekundu isiyoiva au Maroon.
  • Asili yao ni MAJI.


KIPAJI CHA NG'E (MYSTICAL)

Wenye nyota hii wana kipaji na uwezo wa kiroho wa kuwasiliana na watu katika kutekeleza mambo wanayohitaji.

TABIA ZA NG'E

Wenye nyota ya Nge wana uwezo mkubwa wa uvuto au kuvutia watu katika mambo yao. Ni watu wenye uelewa mkubwa na ni majasiri katika kukabiliana na matatizo ambayo wengine yamewashinda.
Ni wenye tabia ya kutilia mkazo mambo yao, tena kwa ukali na ikibidi kutumia ukatili ili jambo litimie wao wako tayari.
Ni watu wenye tabia ya siri na wanapenda kufanya mambo yao kwa siri sana.Wenye nyota hii kama ilivyo alama yao hawaogopi kiza. Wana uwezo na kipaji cha asili cha kutekeleza mambo yao na wakafanikiwa.
Ni watu wenye akili nyingi, waerevu na wepesi sana kuelewa mambo.
Watu wa Nge vile vile wana tabia au wanaweza kujidhuru wao wenyewe.Mambo yanapowawia magumu.

TABIA YA NG'E KATIKA MAPENZI

Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota ya Nge inatawala sehemu za siri.Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na Nge sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
{mospagebreak}

TABIA YA NG'E KATIKA FEDHA

Hakuna kitu kinachoshindikana kwa wenye nyota hii, na chepesi zaidi ni namna ya kupata fedha. Wana uzoefu mkubwa wa kuhimili matatizo ya kifedha wanapoanguka, hata wakiwa matajiri na wakafilisika.
Watu wa Nge wana bahati ya kuvumbua fedha au utajiri katika njia ambazo watu wengine si rahisi kugundua.
Ni watu ambao sio rahisi kudanganyika wakiona mpango wowote wa kifedha. Mara nyingi ni kawaida yao kuchukua kitu au kufanya mradi ambao wengine wanauona wa kipuuzi na wakaugeuza kuwa wa thamani kubwa.
Ni wakarimu sana wanapokuwa na fedha, na hawapendi kujidai kwa utajiri wao. Wako tayari wakati wowote kuwatumia watu wengine kutekeleza malengo yao.
Kwa ujumla wao ni wataalamu wa kutafuta fedha katika njia ambazo watu wengi hawazifahamu.

MAVAZI YA NG'E

Wenye nyota ya Nge wanatakiwa wavae nguo zenye rangi inayong’ara, zenye kuonekana na maridadi,zilizo katika hali ya suti au mbili kwa pamoja.
Nguo ziwe za rangi nyekundu au shati jekundu au skafu nyekundu. Kitambaa kiwe cha sufi au cha fulana au chenye kumeremeta.
Mavazi yaendane na kofia na wanawake wapendelee sana kuvaa suruali.

MATATIZO YA KIAFYA

Nyota hii inatawala kifuko cha mkojo, uume, uke, kifandugu au kitonoko (coccy), mlango wa kizazi(cervix) na sehemu ya haja kubwa. Vile vile inatawala mfumo wa mkojo na tezi kibofu (prostate).
Matatizo yao makubwa ya kiafya yanatokana na sehemu zilizotajwa ambazo zinatawaliwa na nyota yao wenye nyota hii wanapenda kujizoesha sana mambo ya mapenzi na ngono. Wakati mwingine hisia zao zinakuwa kubwa sana kiasi kwamba wao wenyewe wanajishuku vibaya.
Inapotokea hivi wanahitajika kusafisha miili yao kwa fadhaa iliyowajaa kutokana na mfadhaiko wa hisia zao.
Kwa ujumla ni watu wenye afya nzuri na wanapona haraka maradhi yanayowasumbua. Wenye nyota hii wana tabia ya aidha kula, kunywa au kuvuta kupita kiasi au wengine hawafanyi mambo hayo kabisa.
Kwa vile nyota hii inatawala sehemu zinazoondoa uchafu wa mwili ni vizuri watu wa Nge wakawa waangalifu na mambo yanayochafua mwili wao.
Magonjwa makubwa ya wenye nyota ya Nge ni maradhi yanayohusiana na kibofu cha mkojo, maradhi ya kuziba mkojo, kansa ya tezi kibofu (prostate Cancer), matatizo ya damu ya kike na mabusha.
{mospagebreak}

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'E.

Nyota ya Nge ambayo alama yake ya asili ni Maji ni nyota mojawapo ya nyota zenye nguvu katika mambo ya kikazi.
Ni watu wenye milipuko ya hisia wanapokuwa katika miradi yao ya kazi. Wanafanya shughuli zao kwa hisia kali na hamaki na wanategemea wapate majibu ya kuridhisha.
Ni watu makini sana katika kazi na wanafanya kazi kwa kutilia mkazo na ushupavu wakihakikisha wanatekeleza malengo yao. Ni watu waerevu na wenye kung’amua mambo upesi. Ni wafanyakazi wazuri na wanaheshima kwa wafanyakazi wenzao.
Kazi zinazowafaa wenye nyota hii ni kazi za madawa au tiba, kazi za upelelezi, kazi za utafiti, kazi za fundi bomba, kazi za elimu ya kale, na kazi za ushauri wa mambo ya mapenzi na ngono.

FAMILIA ZA NG'E

Wazazi wenye nyota ya Nge ni watu ambao wanaonyesha utulivu wa hali ya juu. Kimaumbile huwa hawaonyeshi hisia walizokuwa nazo juu ya watoto wao, wanaweza wakawa na chuki kubwa lakini hawapendi kuiionyesha.
Kwa ujumla wazazi hao wanapenda watoto na wanatumia muda mwingi na hisia zao kuwangalia na kuwadhibiti watoto wao.
Pamoja na ukarimu wao ni wazazi wenye kupenda nidhamu na wanataka watoto wao wafuate maadili mema. Wazazi hao walivyokuwa wadogo wamepitia ujanja wote hivyo hawakubali watoto wao wawadanganye.
Watoto watagundua kwamba wazazi wao ni watu wa kutisha na kuogopwa lakini uhusiano wao unakuwa ni mzuri. Wazazi wa kike wanakuwa na hisia kali kwa watoto wao kitendo ambacho kinawafanya watoto wawe katika shinikizo.

MADINI YA NG'E

Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa BERYL NA RED CORNELIUS. Mawe haya yenye rangi ya damu ya mzee (Maroon) na rangi Nyekundu yanaakisi au kuashiria asili ya Nge ya uhusiano wake wa asili na kitu chochote cha miujiza na uchawi.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(NG'E, NG’OMBE)
Tabia ya Nge ya wasiwasi, wivu, hisia kali za kimapenzi na dhana mbaya kwa wapenzi wao hutulizwa na kuzimwa na nyota ya Ng’ombe ambao wana tabia ya utulivu, uaminifu, wasioyumba na wanaopenda kusikiliza wanayoambiwa.

VYAKULA VYA NG'E

Wenye nyota hii wanashauriwa wale vyakula au matunda yafuatayo ambayo yanatawaliwa na nyota yao, Mananasi, wapende sana vitunguu vibichi na vilivyopikwa, Nyama ya Kondoo mchanga na vyakula viambatane na viungo vikali.

NCHI ZA NG'E

Ili kupata mafanikio ya kinyota kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota hii.
Miji hiyo ni Liverpool(Uingereza) na New Orleans(Marekani) na nchi za Poland na Switzerland.

RANGI YA NGE

Wenye nyota hii wanashauriwa wapake nyumba zao au vyumba vyao au magari yao au sehemu zao za biashara rangi nzito yenye kutia shauku na kuvutia kama rangi ya damu ya mzee (Maroon).

Ukitaka Ushauri wa Pete yako ya bahati na mambo yako kufunguliwa ili yaweze kwenda vizuri na malengo yako kufanikiwa waweza kunitafuta kwa kubonyeza hapa.
Mawasiliano
 
Last edited by a moderator:
Ndio hivyo au unaweza kuwa mwanzo wa Tarehe 1 ukaitumia kwa mambo yako mazuri mpaka tarehe 2 ukatumia tena bahati yako ukaruka kutofanya mambo yako mazuri mpaka tarehe 6 na Tarehe 8 na taehe 9 kwa hu mwezi ndio tarehe zako kufanya jambo lolote lililo zuri kwako utafanikiwa Mkuu LEONELL Tarehe zilizobakia unaziache ziende kama zilizovyo unangojea mwezi ujao tarehe kama hizo nilizosema unafanya mambo yako tena mazuri.

shukrani saaana mkuu....kwa maana hiyo kama 1,2,9 na 6,8 so kama ikiwa mwezi wa 3 yaani tarehe 1 mwezi 3 hakuna kitu maana haija match...inakuwaje hapo..? na katika ku match inaamaana kitu chochote utakachofanya iwe kuhama eneo moja kwenda jingine..kutafuta mchumba...kuomba kazi..naomba unieleweshe mkuu...usichoke
 
hahaha am no 9 love to me is story everything ok but sikuwa mgomvi utotoni anyway siyo yote lazima yatimie
 
Vijana wa Mjini wanaita "sanaa" au changa la macho, ni kutwist tu Maneno ndio Maana sifa nyiiingi zinaingialia.
 
Ww kweli mwanga
si kwamba yeye ni mwanga elimu ya nyota ni kweli ipo na Mungu kazuia kwani inamfanya mwandamu amtegemee mwanadamu mwingine badala ya Mungu kama ambavyo wengi wanamwuliza bila kujua yeye huchukua vitu kwenye net na si kwamba anaufahamu wa ndani wa vitu hivyo.
Hujasikia watu wanahangaika kusafisha nyota zao na kuvalishwa mipete ya madini fulani ili wawe na bahati bila kujua baada ya hizo bahati na mafanikio watakayopata kuna vitu vingine vitakuwa vimepandwa maishani mwao.
 
Back
Top Bottom