Stori ya El Chapo imenikumbusha kaka yangu alivyopoteza kila kitu kutokana na mwanamke

BIG BROTHER ALEX

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2025
Posts
1,293
Reaction score
2,214
Hii inshu ya El Chapo imenikumbusha kaka yangu.

Mwaka fulani maeneo fulani Kanda ya Ziwa, katika mkoa mpya fulani, kipindi hicho palikuwa bado bush sana. Kaka yangu alikuwa akijihusisha na utafsiri wa movie za kihindi, kizungu na kichina katika ukumbi mkubwa sana kwa kipindi hicho.

Kutokana na mazingira ya wakati huo, DJ alionekana kama super star mwenye ufahamu mkubwa wa mambo. Just imagine unaangalia Kuch Kuch ya Shah Rukh Khan, halafu unatafsiriwa na mtu makini. Akili inakutuma kwamba huenda DJ naye ni fundi kama Shah Rukh Khan tu.

Sasa katika wateja waliokuwa wanaingia pale ukumbini kulikuwa na dada mmoja, si jina lake halisi, aliitwa Mwaida. Huyu alikuwa pisi kwa kipindi hicho, ashikiki. Washikaji wengi walijigonga sana. Alikuwa kama Wema Sepetu wa miaka hiyo mkoani.

Sasa basi yule demu akatokea kumpenda bro kwa sababu bro alikuwa star, na yeye pia akataka kuwa na demu star. Tetesi zinadai demu ndiye aliyemtongoza bro, na bro akajaa kwa sababu demu alikuwa pisi na star hapo mkoani.

Baada ya muda, bro aliacha kazi pale na kuhamia sehemu nyingine yenye masilahi zaidi akiwa na Mwaida. Wakaanza kuishi pamoja kama mpenzi na mpenzi wake.

Siku moja akiwa ndani, alishangaa mlango unagongwa kwa fujo. Akauliza ni nini tena. Ikabidi Mwaida afungue. Mara ghafla polisi wakaingia na kuwaamuru wote waliinua mikono juu chini ya ulinzi. Bro akawa anashangaa kinachoendelea. Polisi wakadai wamekamata majambazi waliodai kuwa walikuwa wakificha silaha zao, yaani bunduki, kwa bro, hivyo walikuja kuzifuata na kumtaja bro pamoja na demu wake kama washiriki.

Bro alishangaa na kukataa, akisema hana silaha yoyote ndani ya geto lake. Lakini wale majambazi wakamwonyesha Mwaida na kusema anajua zilipo. Baada ya kofi moja tu, Mwaida alibinua kitanda, akafungua sehemu fulani na kutoa bunduki. Bro alibaki hana nguvu, hajui hata zilifika humo saa ngapi.

Hapo hapo wakawekwa chini ya ulinzi na kupewa kesi ya ujambazi yeye, demu wake na wale jamaa. Cha kushangaza, haikupita muda demu aliachiwa, huku bro na wale jamaa wakibaki wanateseka. Hawakuhukumiwa mara moja, lakini walikaa miaka jela wakisubiri hukumu.

Hawa mademu kuishi nao kunahitaji maombi sana, na kwa bahati mbaya si rahisi kupambana nao. Mara nyingi mwanaume hujikuta ameshapoteza kila kitu kabla hajagundua kilichotokea.
 
Ila nyie vijana wakiume wa sasa ,
20260226_055058.jpg
mnalalamika sana kuhusu wanawake sijui kwanini🤔
 
Stori ina matobo sana kama pakacha.
 
Mfano ndogo TU mwanamke uzuri wake hauna maana mbele ya wanawake wenzake
LAKINI utapewa thamani pale atakapo jitokeza mbele ya wanaume na wasipo msemesha atapoteza Hali ya kujiamini atajiuliza maswali. mengi huenda hata kujizuru , kwanini ni kwasababu mwanaume ndio kipimo cha uzuri au ubaya wake
 
Ina maana huyo demu ndio alikuwa anaficha silaha za majamaa yake kwenye geto la msela wake bila msela kujua?
Mkuu HAPO sifahamu, bro hakuwa na HIZO mishe, na kama ange kuwa na HIZO mishe kipindi maaskari wanagonga MLANGO ange baha KUTAKA KUKIMBIA, lakini ye MWENYEWE AKAWA anashangaa, Kuna Nini MBONA SINA hatia yeyote?
 
Back
Top Bottom