Nilitumia fursa hiyo kukuuliza majina yako (km cjakosea ni Elizabeth), umri, ndugu zako, mtaa na nyumba unayoishi! Nashukuru mungu ulijaribu kuyajibu!
Wakaniomba PF3, nikawajibu sina, hatukupata muda wa kuipitia. Nikaambiwa nikatoe maelezo kituo cha polisi Superstar, nikaenda!
Kurudi - nikakuta ushapelekwa chumba cha x-ray, nikaambiwa mtu wa x-ray amelala, kwa hiyo mgonjwa wangu hawezi kuhudumiwa mpk asubuhi! Nazifahamu sana lugha hz! Nikatoa elfu 5 (ipe jina utakalo). Muda tena, nikaambiwa nikakununulie dawa ya maumivu, nikaenda! Sifahamu nini kilitokea, lkn ulipigwa x-ray ndani ya dak 5.
Polisi: una uhusiano gn na hy majeruhi?
Mimi: simfahamu!
Polisi: Sisi tunaamini wewe ndiye uliemgonga kisha ukajifanya Msamariamwema. Unabisha?
Mimi: Afande mimi sina leseni na wala sijui kuendesha gari.