STORI FUPI: BABA MASIKINI HADI KUWA BABA TAJIRI

Man Middo tz

Senior Member
Sep 9, 2020
154
230
Sikuwahi kuwambia watoto wangu kuwa nilikua nafanya kazi gani. Kamwe sikutaka wajihisi aibu kwasababu yangu, pindi binti yangu aliponiuliza nilikua naenda kufanya nini ninapotoka, nilitumia muda huo kumzuga na kumwambia kuwa mimi ni kibarua.

Kila siku kabla sijarudi nyumbani nilitumia muda wangu kuhakikisha naoga katika vyoo vya kulipia ili kwamba wanangu wasipate dalili yoyote ya kazi inayoifanya.

Nilitaka kuwapeleka shule mabinti zangu niliojaaliwa, nilitaka wasome na waelimike. Nilitaka wasimame mbele za watu wakiheshimika. Kamwe sikutaka yoyote awatazame kwa jicho la huruma na kuonekana mtu duni kama ambavyo kila mtu ananifanyia mimi. Watu mara zote hunidharau na kuninyanyasa.

Niliwekeza kila senti ya kipato changu kwajili ya Elimu ya mabinti zangu. Sikuwahi kununua shati jipya, baadala yake nilitumia pesa hiyo kununua vitabu kwajili yao. Heshima, ndio kitu ambacho nilitaka wakipate kutoka kwangu. Mimi nilikua mfanya usafi.

Siku moja kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili wa binti yangu kujiunga chuo, Sikuweza kumpatia ada. Siku ile sikufanya kazi. Nilikaa pembeni ya matakataka, Nikijaribu kuyazuia machozi yasinidondoke. Wafanyakzi wenzangu wote walikua wakinitazama lakini hakuna hata mmoja aliyekuja kuongea na mimi. Niliumia na kuvunjika moyo. Sikua na wazo lolote la namna ya kumtazama na kumjibu binti yangu pindi nitakaporudi nyumbani na kuniuliza kuhusu kumlipia ada.

Nimezaliwa masikini, siku zote niliamini hakuna kitu kizuri kinaweza kutokea kwa mtu masikini. Siku ile baada ya kazi wenzangu wote ninaofanya nao kazi walinifuata na kukaa pembeni yangu, wakaniuliza kama nawachukulia kama kaka zangu au ndugu zangu. Kabla sijawajibu, Wakanipatia posho zao zote za ile siku, pindi nilipojaribu kuwakatalia kila mmoja alinijia juu akisema

“Tutashinda njaa leo kama itahitajika lakini binti yetu lazima aende chuo”

Kwa kweli sikuweza kuwajibu. Siku ile sikuoga kama kawaida yangu nilienda nyumbani kama mfanya usafi wa manispaa.

Binti yangu sasa anenda kumaliza chuo kikuu hivi karibuni. Binti zangu watatu kati yao hawataki niende tena kazini. Yule mmoja baada ya kumaliza chuo akapata kazi ya muda na wale watatu wakafungua kituo cha tuition. Lakini mara kwa mara ananichukua na kupeleka ile sehemu niliyokua nafanyia kazi, tukifika anawanunulia chakula wafanyakazi wenzangu mimi nikiwa pemembi yao.

Wanacheka huku wanamuliza kwanini anawanunuliza chakula kila mara? Binti yangu anawajibu kuwa “Nyie wote mlishinda njaa siku ile kwajili yangu ili niweze kuja kuwa hivi nilivyo leo, Niombeeni ili niweze kuwapatia chakula kila siku”

Sasaivi sijihisi mtu masikini tena. Kama umejaaliwa watoto kama hawa, unawezaje kujiona masikini.

FUNZO: Unapokua mazazi haikuhitaji kuwa na kazi ya ofisini ili kutimiza ndoto za wanao. Amini kwamba kazi ni kazi muhimu uwe na malengo na mapenzi ya dhati kwa wanao. Jifunze kuishi na watu vizuri haswa katika maeneo ya kazi kwasababu shida haichagui ikupate wapi. Unaweza kujiona wewe uko vizuri sana kifedha na huwezi kushindwa na kitu kama ada au chakula lakini kiasi kwamba kila anaekatiza mbele yako unamuona panya tu ni sawa ila kumbuka wewe unapanga lakini Mipango ya Mungu ni bora kuliko mipango yoyote ile.

Watoto wanapaswa kutambua na kuthamini jitihada za wazazi wao kwasababu kuna wakati mazazi anajinyima hata kula au kuvaa ili mtoto wake asijihisi mnyonge mbele za watu. Mzazi anaweza asivae nguo mpya hata mwaka mzima ili mwanae avae apendeze na asionekane mnyonge na dhaifu au duni mbele za watu. JFUNZE KUWAHESHIMU WAZAZI WAKO KWA KILE KIDOGO WANACHOKUFANYIA.

Kama imekugusa hebu sema “ASANTE BABA NA MAMA KWA HAPA MLIPONIFIKISHA”

LIKE NA SHARE NA WENGINE.

NIFOLLOW

Instagram @middotz_

*Facebook page man Middo

Email: rmadodi7@gmail.com

Whatsapp: 0655 969 963

Twitter @middotz_
1684042062775.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom