Barabarani
Member
- Sep 27, 2017
- 19
- 8
Sehemu nyingi nchini wameweka hii mistari ya “Simama” (Stop lines) kwenye kila vivuko vya watembea kwa miguu. Japokuwa lengo ni zuri, pengine wahusika hawajafikiria vizuri hasara, usumbufu na mkanganyiko unaoletwa na hii mistari. Nitatoa mifano michache tu.
1. Stop Lines peke yake bila kuwepo Stop signs, Stop Warning Sign au Stop markings.
Mstari wa Simama (Stop Line) huambatana na alama ya Simama (Stop Sign) na kazi yake ni kuashiria wapi usimamishe gari lako kabla ya kufika kwenye kivuko. Mstari mzima kabla ya kivuko cha watembea kwa miguu KIMSINGI unakutaka usimame, bila kujali kama kuna mtembea kwa miguu au la.
Tatizo ni pale unakutana na huo mstari bila hata ya kuwepo Alama ya Simama, Tahadhari au hata Mchoro wa barabarani kukuonya mapema kuwa mbele kuna kivuko cha watembea kwa miguu ambapo utalazimika kusimama. Hili ni muhimu kwani kimsingi Alama ya kivuko cha watembea kwa miguu yenyewe haimrishi mtu kusimama hivyo basi ili kuondoa kushtukiza watu ni budi pawepo alama ya tahadhari au amri kwa madereva kuwa watawajibika kusimama wakifika eneo husika. Surprises barabarani ni hatari. Ni vizuri mistari hii iambatane na alama ya Simama au neno “Stop/Simama” kwenye lami au iondolewe kabisa.
2. Hakuna mantiki ya stop lines kwenye kila kivuko cha watembea kwa miguu kwenye barabara za barabarani 30/50 speed limits.
Ukishadhibiti mwendokasi mpaka30/50 kmh unakuwa umemuongezea dereva uwezo na muda wa ku-scan njia vizuri na kuona kama kuna watumiaji wengine wa barabara. Kitaalam ukiwa unaendesha 50kmh, unakuwa na breaking distance ya mita 14-15. Maana yake ni kwamba ukiwa unaendesha 50kmh, ukianza kushika breki gari lako litatembea mita 14-15 hadi liweze kusimama kabisa. Kwa spidi ya 50, utaona kabisa kwamba dereva atakuwa na uwezo wa kuona kivuko au watembea kwa miguu mapema na kusimama kuwapisha na hasa ukizingatia kuwa kuna alama za tahadhari ya kuwepo kivuko cha watembea kwa miguu. Ni kweli pia kwamba madereva wengi hawasimami kuwapisha watu wanaojaribu kuvuka lakini ufumbuzi sio kuweka Stop lines kwenye kila kivuko au kulazimisha magari kusimama kwenye kila kivuko cha watembea kwa miguu hata kama hakuna mtu anayevuka. Pengine aidha tutumie bumps au iwe ni lazima kusimama kama tu kuna watu wanaovuka.
3. Kwenye maeneo ya makazi au miji Stop lines kwenye vivuko vya watembea kwa miguu zinaleta usumbufu usio wa lazima hasa pale unapokuta kuna vivuko kadhaa vya watembea kwa miguu vimeachana mita chache. Mfano mjini kila baada ya mita mia tano unakuta zebra crossings yenye Stop lines, ambazo kimsingi zinakutaka usimame hata bila pedestrians kuwepo. Utasimama mara ngapi bila kusababisha jam au ajali ya kugongwa na magari yanayotokea nyuma? Ni aidha hatujali muda au hatufahamu vizuri muktadha wa kutumia hizi Alama za Barabarani.
Tufikirie tena vizuri.
Barabarani.
>>>Kama unahitaji kujifunza zaidi kuhusu alama za barabarani, unaweza ku-download Application ya simu ya AlamaBarabarani Quiz - Google Play au App Store -