Kinachokusumbua Bwana mdogo ni siasa za majitaka za kujadili watu na sio hoja.........embu chambua hii hoja;DR. Slaa: ''Tukishika Dola tutaruhusu utengenezaji wa pombe ya gongo kisheria''.Huwezi kuwa mwanasiasa kwa haya mambo yako ni mtu wa jazba na siasa majitaka. Jitahidini muunde chama kitaasisi zaidi na sio kifamilia (rejea mtikila chadema chumbani na chadema sebuleni),Sasa kwenye hiyo post yako umeejadili nini?makosa ya spelling kila mtu hufanya hata wewe mara kwa mara hufanya ila watu wanaacha sababu ni kawaida. Kuhusu Wasira kwa maoni yangu na ya wengi ni kwamba amejadili mambo ya msingi sana au ndio unataka JF ijae mambo ya DVD za Lema, ambazo hasemi kilichomo. Acha mambo yako dogo!!
Kuhusu Gongo?
Rejea ukweli huu wa Entrepreneur
"Suala si kumtetea mtu, bali kujadili hoja zilizopo mezani. Hata kama hoja hizo zmetolewa na mpinzani wako kisiasa ni vyema kukubaliana nazo kama zina mashiko.
Sasa ukweli ni HUU,
Alichokisema Dr. Slaa si kipya ktk Taifa hili kwani tayari kina msingi wa
kisheria, tena zilizoandaliwa chini ya Serikali ya CCM.
Rejea; The Moshi (Manufacture and Distillation) Act, 1966 na The Traditional Liquor (Control and Distillation) Act Cap 385.
Sheria hizo zimeweka msingi wa namna ya kutengeneza, kusambaza na kuuza
pombe hiyo (Gongo/Piwa/Moshi)
Sheria hiyo pia inaunda Mamlaka ya Usimamizi na Utoaji leseni. Kama
serikali yetu sikivu ya CCM ingeamua kutekeleza sheria hizi kwa wakati huenda Taifa letu lisingeshuhudia vifo vinavyotokana na unywaji wa Pombe ambazo ubora wake unatiliwa mashaka kwani zingekuwa zinapimwa kwanza.
Kwa Taarifa tu ni kuwa Chief Quality Assurance kutoka TBS amewahi kuthibitisha ubora wa Pombe ya Gongo kutokea Kagera kupitia kipimo cha
Portable Spirit Specification TZS 468:1992 na kusema haina matatizo
yoyote kiafya"