Steven Wassira arudisha fomu za Urais

chipoteka

Member
Jan 9, 2015
66
25
ImageUploadedByJamiiForums1434970745.009602.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1434970766.156699.jpg
Baada ya kuzunguka katika mikoa yote Tanzania kwa usafiri wa njia ya barabara na kufikia wanachama moja kwa moja ktk maeneo yote ya mjini na vijijini..hatimaye mtia nia wa Urais wa CCM Mh.Steven Massatu Wassira leo atarudisha fomu za wadhamini ktk makao makuu ya CCM-Dodoma.


Mh.Wassira ndio mgombea aliyepata nafasi ya kuzunguka ktk mikoa yote Tanzania wakati wa kutafuta wadhamini.Katika mikoa,wilaya na Vijiji alivyopita,Mh.Wassira aliungwa mkono na wanachama wa kada zote za vijana,kina Mama,kiba Baba na Wazee ndani ya chama cha Mapinduzi wametokea kumuunga mkono na kumtia moyo ktk safari yake ya kuomba ridhaa ndani ya chama ya kupererusha bendera ya CCM ktk uchaguzi mkuu wa 2015.Wanacham a waliojitokeza ni wale waliofika kwa moyo na kwa kujitolea bila ujira


Alipopata wasaa wa kuwasalimia viongozi na wanachama ktk maeneo hayo,Mh.Wassira amesisitiza kuwa CCM ni chama kikubwa,hivyo kinahitaji mgombea mwenye rekodi nzuri ndani na nje ya chama ili kushindana na vyama vya upinzani ambavyo vitaleta ushindani ktk uchaguzi wa mwaka huu,ameelezea uzoefu wake wa kukitumikia chama na serikali kwa uadilifu na uaminifu kwa muda mrefu,huku akiwa na uzoefu na ujuzi aliouchota toka kwa Rais Kikwete na watangulizi wake ambao alifanya nao kazi kwa uhakika.Amesisitiza suala la umoja na mshikamano ndani ya chama na Taifa kwa ujumla,akiwa katika Visiwa vya Zanzibar alisisitiza suala la umoja na mshikamano linalochagizwa na uwepo wa Muungano,hivyo aliahidi kuwa mmoja wa watu watakaouenzi na kuutunza Muungano.
ImageUploadedByJamiiForums1434970798.075861.jpg

Aliasa juu ya "purukushani" ndani ya chama zinazoongozwa na rushwa na uungwaji mkono wenye harufu ya rushwa na hongo.Akitoa rai kwa wanachama wa CCM ktk maeneo aliyopita,Mh.Wassira alisema vipaumbele vyake vitaongozwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi,itakayopitishwa na kukubaliwa na vikao rasmi vya chama,akisisitiza yeye binafsi hawezi kuwa na vipaumbele zaidi ya vile vitakavyoamuliwa na chama,anaamini CCM ikiwa ni moja ya chama makini msisitizo wake utakuwa ktk elimu,afya,kilimo na miundombinu,huku akisifu juhudi zilizofikiwa na serikali ya awamu ya nne na kuendeleza pale ilipoishia.

Katika kilimo amesisitiza kuwa mara zote ilani ya CCM huegemea ktk kuimarisha kilimo chenye tija,toka ktk jembe la mkono mpaka uzalishaji wa kutumia zana za kisasa za kilimo,ili kuliongezea Taifa chakula cha kutosha na kuimalisha uchumi wa mkulima wa Tanzania,uboreshaji wa elimu na huduma za afya ktk maeneo yote ya mjini na vijijini na huku akisisitiza kuimarisha miundombinu ili kuunganisha maeneo yote ya nchi.


Ikumbukwe kuwa Mh.Wassira ni mmoja wa makada wenye imani na kuungwa mkono na wana-CCM wengi bara na Visiwani,hivyo nafasi yake ktk kuelekea kinyang'anyiro hiki inatazamwa na wengi kwa namna ya kipekee.
 
Namuonea hurumaa... huyu anafaa uwaziri tu basii... Urais hawezi at all..!!
 
Huyu ndio chaguo la wengi ndani ya chama...muadilifu na huru ktk makandokando ya rushwa
 
Wakimpitisha Huyu Jamaa Itakuwa Bomba Sana Maana Ata Akiwa Rais Upigaji Nje Nje Maana Huyu Si Yule Wakudozi?
 
Nimemsikiliza leo Bungeni,nilikuwa simkubali...ila leo kaongea kwa dhati
 
Jamani nina swali. Kuna uhusiano upi Kati ya kugombea nafasi ya ubunge na makazi? Naamanisha naweza kugombea ubunge katika jimbo ambalo sijazaliwa wala sijawahi kuishi? Na kama hairuhusiwi kugombea nafasi hiyo ni kifungu kipi kimeandika hicho kitu?
 
Back
Top Bottom