Stephen Chelu: Hatimaye miaka mitano ndani ya JF

Stephen Ngalya Chelu

JF-Expert Member
Oct 31, 2017
7,621
16,373
Tukiwa tumekaa na masela tukipiga story, mara anakuja dada mmoja na kutuambia kuwa kuna ajali mbaya ya basi imetokea Singida. Akaulizwa hizo habari yeye amezotoa wapi, akajibu kuwa ameambiwa na mtu ambaye naye anadai kuwa habari hiyo aliiona ‘Jamaaforums’. Hapo ndipo nilifungua kinywa changu na kumsahihisha kuwa haikuwa ikiitwa Jamaaforums bali Jamiiforums. Hiyo ndiyo kumbukumbu yangu ya awali kabisa kuhusu Jamiiforums. Hiyo ilikuwa 2011 nikiwa kidato cha pili (14 years old).

Hadi leo huwa sikumbuki ni lini na wapi hasa niliifahamu Jamiiforums kwa mara ya kwanza kwa maana kwa kipindi hicho sikuwa na simu hata nokia jeneza. Nimekuwa nikijaribu kukaa na kujaribu kung’amua ni wapi niliifahamu JF kwa mara ya kwanza lakini huwa naishia kuumwa kichwa tu.

Anyway, ilipofika 2013 nilipata simu (itel) yenye uwezo wa kuingia mtandaoni hivyo nikawa naingia JF kama ‘Guest’ japokuwa sikuwa na enjoy kwa sababu simu ilikuwa slow mno kwenye upande wa internet halafu kioo kilikuwa kidogo mno. Mwaka 2015 nilipata simu kubwa kubwa kidogo (zile Tecno za button zilizokuwa na opera mini). Simu hii kiukweli ilinifanya angalau nianze kuifurahia JF kwa sababu ilikuwa fasta kuliko ile ya mwanzo. Nilivutika sana na jukwaa la intelligence kwa sababu kiasili mimi ni mtu ninayependa mijadala migumu migumu hasa ihusuyo imani.

Hatimaye mwaka 2016 niliamua kujiunga jf rasmi nikitumia ID Fulani hivi (Sitoitaja). Basi bwana, nikaanza vurugu humu jukwaani. Nilianzisha mada kama mashine ya kutoa copy lengo na mimi niwe maarufu kama member wengine waliokuwa kwenye kilele kipindi hicho. Kweli bwana, baada ya miezi kama mitatu hivi nikawa nikikatiza kwenye nyuzi mbalimbali watu wananisabahi na kutaniana. Nikaona ‘enhee nakaribia kuwa staa humu JF’ (nikiri kuwa nilikuwa boya sana kuwaza hivyo).

Mwaka mmoja baadaye (2017), kwa sababu kadhaa ambazo niliona ni za msingi, niliamua kuachana na ID ile na kufungua ID mpya (Hii ninayoitumia kwa sasa) ambayo nikaomba iwe verified chap kwa haraka. Maisha ndani ya verified ID yalikuwa tofauti, sikuwa na uhuru kama zamani lakini imenifunza kuwaza mara mbili kabla ya kuandika chochote kwa maana naamini kila neno ninaloandika humu nitawajibika kwalo kama ikihitajika. Lakini pia imenifunza kuwa mimi, kusimama katika mawazo yangu bila kujifuchaficha wala kutetereka.

Leo natimiza miaka mitano jf bila ban wala kuwa na record yoyote mbaya, isipokuwa tu kupishana kauli na baadhi ya member ambalo pia ni jambo la kawaida katika mijadala. Lakini kama kuna yeyote nilimkwaza kwa namna moja ama nyingine, aniwie radhi. Kwa upande wangu sina mtu ambaye nina bifu ama kinyongo naye.
Nimetoboa miaka mitano. Je nitatoboa miaka mitano mingine? Hakuna ajuaye kesho.

Tuendelee kujadili bila kuvunjiana heshima kwa manufaa ya jamii yetu na taifa letu kwa ujumla kwa maana sisi ndo wajenzi wa jamii na taifa letu la Tanzania. Nasema uongo ndugu zangu?
 
Nokia jeneza ni simu gani,

Halafu nafikiri asilimia 80 ya wanachama wa humu ni under 30 ndio maana cc za mijadala zimeshuka
 
Hongera sana mkuu na JF hii ipo very diluted,wengi wanasoma sio to understand but to ask stupid questions yaani tuna ile stupidity ya kuichukua sehemu na kuifanya sehemu ya Maisha yetu,keep it up mkuu na hongera kwa kuwa verified member
 
Nokia jeneza ni simu gani,

Halafu nafikiri asilimia 80 ya wanachama wa humu ni under 30 ndio maana cc za mijadala zimeshuka
Jina la kiwandani, Nokia 3310

2021-04-11 20.29.05.png


Hapa simu wenzake wakiwa wanamzika
2021-04-11 20.28.25.png



Kuhusu hilo lingine, nadhani ni hulka ya mtu tu japo dhana yako inaweza kufanya kazi kwa kiasi fulani. Tiba kuu ni kuwa mstaarabu. Mimi mtu akionyesha kunishambulia kibinafsi na sio kulingana na mjadala, huwa nasepa kimya kimya...akivuka mipaka nachagua kuwa snitch, nam'report kisha nalala mbele.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom