Kama ni mkazi wa Dar hizi stand mbili bila shaka utakuwa unazifahamu.
Ukizitazama hizi stendi utaona utofauti mkubwa wa uwezo wa kiutawala kati ya sehemu hizi mbili. Stendi ya Mawasiliano wamachinga wamekaa kimpangilio mzuri sana. Kuna vibanda vimejengwa pembezi ya hifadhi za barabara lakini vina hali nzuri. Wameacha njia za watembea kwa miguu na mazingira yao ni masafi, mitaro haijaziba na kiukweli panapendeza.Abiria wana mahali pa kukaa chini ya vivuli wakisubiri magari.
Eneo la soko limetengwa pembeni ya stand napo bidhaa zipo kwa mpangilio hazitandazwi chini soko ni safi muda wote.
Stendi ya Mbezi Luis ni mpya kuliko ya Mawasiliano lakini inauongozi mmbovu sijawahi kuona.
Haina mpangilio wa kueleweka wapi wakae wamachinga wapi wakae bodaboda na daladala zipark kwa utaratibu gani. Mabanda ya wamachinga yamejengwa juu ya mitaro, mitaro ni michafu, barabara ni chafu, hakuna maeneo ya abiria kukaa zaidi ya wa mwendokasi tu. Abiria wanapigwa na jua na mvua muda wote.
Hapaeleweki soko ni lipi, barabara ni ipi na stend ni ipi. Ni vurumai muda wote kuna wapiga debe na vibaka wengi wanaohatarisha usalama wa raia.
Naomba serikali iuangalie kwa karibu sana uongozi wa stendi ya Mbezi Luis kwa ukaribu sana stendi ni mpya lakini imekuwa kama dampo.