Stendi ya daladala ya Mwenge kuhamishiwa Makumbusho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stendi ya daladala ya Mwenge kuhamishiwa Makumbusho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtego wa Noti, Aug 20, 2012.

 1. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #1
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ama kweli ukistaajabu ya Firauni utaona ya Mussa,
  Leo katika vyombo vya habari manispaa ya kinondoni wamesema eti wanahamisha kituo cha daladala cha Mwenge kwenda Makumbusho. Cha kushangaza ni kuwa, ni hivi majuzi tu wametumia mamilioni ya walipa kodi kukarabati kituo hicho cha Mwenge, sasa inakuwaje wakihamishe ghafla kiasi hicho? Kama kulikuwa na mpango wa kukihamisha, kulikuwa na umuhimu gani wa kukikarabati? si wangekarabati hicho kituo cha Makumbusho tu kuliko kupoteza hela za walipa kodi kwa kitu ambacho kitaondolewa baada ya muda mfupi?
  Hivi kweli huko maofisini tkuna vichwa au nazi? hakuna wanaofanya planning hata angalau ya miaka mitano tu?
  Kwa hali hii, this country will remain poor if nothing is is done immediately!
   
 2. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  mbona kama habari haijakamilika, wanahamisha kwa nini, naamini ni lazima watakuwa na sababu,hata kama ni ya kipuuzi kiasi gani lakini lazima watasema tunahamisha kituo kwa sababu a,b,c na hapo Mwenge wanataka kupafanya nini kupaacha paoze? Isije kuwa tu unatafuta sababu za kuthibitisha kile ambacho tayari umeshakijenga katika fikra zako kwamba hakuna jambo zuri linafanyika hapa nyumbani leta habari kamili labda kuna sababu ya maana!

   
 3. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  hawajatoa sababu yoyote...wamesema wanakihamisha tu...labda wameona hapatoshi...
   
 4. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Labda tu haujapata maelezo ya kutosha lakini jinsi serikali pamoja inavyofanya kazi pamoja na madhaifu yake yote nafikiri ni lazima wanatoa sababu zinaweza kuwa za kijinga au za maana lakini lazima waseme tunahamisha kituo kwa sababu kadhaa na pale Mwenge patakuwa kitu fulani!
  Maadamu bado hawajasema ngoja tusubiri wakija kusema labda sababu kubwa kiasi kwamba inafanya hiyo gharama ya kujengea ionekana tone la maji baharini!
   
 5. Sema Chilo

  Sema Chilo JF-Expert Member

  #5
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 324
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makumbusho wapi jamani mbona kuna ujenzi unaendelea?
   
 6. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,836
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mimi ninavyojua Huwa Stend za Mijini sio sehemu za Kwenda Kupumzika ila ni kupanda basi Kuelekea Majumbani baada ya shughuli za mchana Kutwa!! Sasa Kuhamisha kituo kutakuwa na faida gani kwa msafiri anayehitaji Kuwahi nyumbani / kazini kwake? Town trips Stendi ya nini Kubwa!! LAbda Change over Hub!! Ila kwa mwenge Wanahitajika Kuboresha Incoming na outgoing na kupunguza msongamano wa biashara that is a hub!!!!!
   
 7. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #7
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  wanajenga nini tena?
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  hujafafanua vizuri bali unarusha mawe, ngumi, mateke na vichwa kwa Manispaa yako!, ungetueleza vizuri kama mwenge hakutakuwa na kituo kabisa au ni mipango tu ya kuhakikisha magari yote yanapitia mwengi lakini final destination ni makumbusho, kama ni hivyo maanayake ni kuwa kituo cha mwenge kitaendelea kuwa kituo cha kati na si cha mwisho, fafanua, otherwise punguza madongo na dharau kwa mamlaka yako.
   
 9. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  na wao hao manispaa wangesema mkakati mzima kuliko kusema tu kuwa kituo cha mwenge kinafungwa na kinahamishiwa makumbusho....
   
 10. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  sinauhakika kama Manispaa wamesema tu kuwa kituo cha mwenge kinafungwa na kuhamishwa, nadhani kunamaelezo zaidi, nikiyapata haya ndipo nitapata uelewa zaidi juu ya ubora au udhaifu wa huu mpango. more comments reserved.
   
 11. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #11
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,223
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  mwenge nacho ni kutuo (stendi) au SOKO?? Mbona sikuhizi limekuwa soko SOKO LA KILA KITU?
  bora wahamishie tu makumbusho wawaache wamachinga wakiendelea na biashara zao maana hakuna hatua yoyote zinazochukuliwa kuwaondoa waliofanya soko pale, kwanza hawalipi ushuru!

  yaan stend ya mwenge kilichobaki ni pale wanapotoza ushuru wa magari tuu, baaasi baada ya hapo hakuna la maana, stendi gani chafu inanuka, mabomba ya maji machafu yamepasuka kila sehemu.
   
 12. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #12
  Aug 20, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hivi ni MWENGE STAND au MWENGE SOKONI?
   
 13. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #13
  Aug 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,229
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  sasa kulikuwa kuna umuhimu gani kukikarabati kwa gharama kubwa wakati ule kama kitu chenyewe ni cha muda mfupi?
   
 14. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #14
  Aug 20, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Wana tapatapa hawajui wanataka nini na wasafiri wanataka nini...acha wapeleke popote hata mabwepande wapeleke tu poa:sisi tupate usafiri na tufike tunakotaka kwenda bila bughudha na bila kero!
   
 15. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #15
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kama hapatoshi sasa makumbusho itakuwaje maana katikati ya stendi wamejenga jumba sijui ni la nini..
   
 16. tutaweza

  tutaweza JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Hiyo miradi ndio sehemu za kupigia hela.
  Si wanajua watanzania tumelala!?
  Kama ni kweli basi nadhani waliopo ofisi ya mipango wanatakiwa watoe maelezo ya kutosha. Huu ni ufujaji!
   
 17. K

  KIDUNDULIMA JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 773
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  hata wakiwa na sababu ya maana kuna barabara gani ya kuingilia makumbusho ili kiwe kituo? pia usisahau kuwa eneo walalotaka kuwa stend lipo kwenye makazi ya watu ambako barabara nyingi zilizopo ni za mitaaa na hazikubuniwa kama barabara za kupita daladala.
   
 18. K

  KVM JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 1,814
  Likes Received: 336
  Trophy Points: 180
  Kama kweli wanataka kufanya hivyo hicho ni kipimo tosha jinsi tulivyo na watu wasioweza kufikiri. Barabara kutoka Mwenge mpaka Morocco ina foleni ndefu sana bila hata haya madaladala yanayoishishia Mwenge.
   
 19. piper

  piper JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mbwa kala mbwa
   
 20. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Hata wewe pia unauliza maswali kama mimi, sio mimi aliyeleta hii mada, hata mimi pia najiuliza maswali mengi inawezekana pia hata mada yenyewe ni uzushi na haina ukweli, kwa hiyo sio haki kuanza kuwahukumu watu (watendaji) bila ya kuwa na ukweli wa taarifa! kwa kifupi mimi sijui labda muulize aliyeleta habari!

   
Loading...