Ombi: Stendi mpya ya Daladala Mwenge ipewe Jina la Nyirenda Shujaa aliyepandisha Mwenge wa Uhuru Mlima Kilimanjaro!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Wahenga mtakumbuka kabla ya Ukarabati wa barabara ya Mwenge palikuwepo na Kituo cha Nyirenda ila ilipoanzishwa ITV kile Kituo cha Nyirenda Watu wakaanza kukiita ITV

Niombe tu kwa mamlaka husika kutokana na historia iliyotukuka ya huyu Nyirenda basi Kituo kipya cha Daladala pale Mwenge kiitwe Nyirenda

Ni Katika kuweka kumbukumbu tu kama ambavyo tuna Vituo vya Mzee Bamaga, Mama Zakaria, Mzee Komakoma, Mzee Manyunju, Mzee Manyanya, Mzee Mwinjuma, Mzee Kopa nk..nk

Ni hilo tu

Mlale Unono 😃😃
 
Nakumbuka kituo cha daladala pale ITV zama zamani kiliitwa Nyirenda. Naunga mkono hoja.
 
Back
Top Bottom