Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Ni kwamba serikali inataka kuhakikisha kuwa hao samaki wanaowategemea wanaendelea kuwapo hata kwa wajukuu wao!
GT
Mzee nadhani sababu kubwa ni kwamba marine species wako in danger huko mafia. Nadhani serikali imechukua hatua hizi kutokana na wavuvi kuto kuthamani kwamba kuvua samaki wadogo kunaweza kuleta madhara katika ecosystem nzima.
Katika upande mwingine wa shilingi, nadhani measurement walizochukua serikali zinaonyesha kuwa za kibabe zaidi.
Mfumwa.
Una uhakika gani kuwa serikali haijafanya hicho unachosema? Kwamba serikali inatoa muda ili samaki WOTE waweze kupata nafasi ya kukua na kuongezeka? Sisi hatuna Coast Guard sasa kuna ubaya gani kutumia jeshi kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa? Hapo hapo Mafia kuna kituo cha Mafia Island Marine Park ambacho kina wataalamu wa masuala ya uvuvi. Hawa bila shaka ndiyo waliotoa ushauri wa kuzuia uvuvi wa nyavu ndogo. Bila shaka baada ya kuona kuwa hatua nyingine ni vigumu kuzitekeleza.
Kusema kuwa hauwezi kuzuia uvuvi wote wa nyavu ndogo sio sahihi. Mbona nchi nyingi zimefanya hivyo ilikuokoa samaki wao?
Ukweli unabaki pale pale. Samaki wetu wako hatarini na ni lazima serikali ichukue hatua ya kuwalinda. Hatusaidii kwa kudai kuwa ati kuna genocide inaendelea! Si kila kitu kifanywacho na serikali ni kiovu.
Amandla........
Mfumwa.
Sidhani kuwa unataka kuleta ubishi. Kutokana na maelezo yako naamini ni kweli una ujuzi kuhusu suala hili ambao wengi hatunao.
Tunapotofautiana ni pale unaposema kuwa kuna njia mbadala za kuhakikisha uhai wa samaki hawa ambazo serikali ilipaswa kutumia kabla ya kuzuia uvuvi wa nyavu ndogo. Imani yangu ni kuwa kwa sababu hao watu wa Mafia Marine Park wapo pale basi bila shaka hizo njia unazoshauri waliona hazitakuwa na mafanikio wanayotarajia katika wakati walio nao. Hawa wapo muda mrefu tuu pale Mafia na ni lazima hizo hatua wamejaribu bila mafanikio.
Ni juu yetu kama wataalamu kuwafahamisha wananchi kuhusu nia ya hatua kama hizi badala ya kubeba mabango kudai kuwa kuna mpango wa Genocide dhidi yao! Genocide ni neno zito sana na halipaswi kutumika hapa. Kwa kufanya hivyo, hatuwatendei haki ndugu zetu!
Amandla.....
Fundi Mchundo, nikisema ukweli sina ujuzi wa mambo hayo, ninajaribu tu kufikiri na kuangalia hali halisi. Haya ngoja nikubaliane nawe kuwa hawa jamaa (Mafia Marine Park) ndio waliotoa huo ushauri baada ya njia nyingine kutoleta suluhisho. Lakini ukumbuke yawezekana ushauri huu ukiingia kwa ndani unaweza kuta unawasaidia wale wenye mameli makubwa ya kuvua samaki (kama kamba nk) kule, yaweza fananishwa na wale watoao ushauri kwa sekta za madini. Lakini baadae tutajua ni nani yuko nyuma ya hili suala, ni suala la muda japo Wananchi wanaumia. Kusema ni "Genocide", hata nami nachelea, lakini muanzisha mada huenda ana wazo zuri kutumia hilo neno kuvuta hisia.
Muito Obrigado...
Mikoa kama nchi ndogo ndani ya Tanzania
ZIARA yangu hivi karibuni huko Rwanda kanchi kadogo pembezoni mwa Tanzania imenionesha kwamba Watanzania tunacheza na sio serious kuihusu maendeleo yetu.
Ningeliomba wana JF mfanye mpango mkawaoneshe viongozi wetu uchawi Rwanda inayoufanya leo ili kesho na kesho kutwa wakiendelea EPA, Richmond na Dowans zao wasijeshangaa Rwanda ina register GDP per capita ya $ 5,000 wakati sisi tunalemaa lemaa katika $600 mwaka nenda, mwaka rudi.
Kama Rwanda nchi ndogo kuliko mkoa wa Mwanza na yenye rasilimali ndogo kuliko mkoa wa Mwanza inaweza kufanya inachokifanya tatizo letu jama ni nini?
Kwanza, hatujatambua tunakotaka kwenda. Pili, tunawaweka mbele sana Wazungu na mawazo yao yasiyo ya kina na uzito katika mazingira yetu mbele mbele mno kama vile sisi wenyewe hatuna kimbelembele! Kwenye siasa lakini......
Wao wana magavana sio wakuu wa mikoa. Hawa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mimi naona vile wamekuwa breki kwenye maendeleo ya mikoa na nchi kwa ujumla. Nadhani inafaa sasa tuwe na tuongozi tudogo tunakochaguliwa na wakazi wa mkoa ili mambo yasiwe yanakwenda kama kawa hata aingie au atoke mkuu huyu mambo ni yale yale wakazi hawaoni kifuu wala nafuu!
Nina hakika kuna mikoa hapa ikiwemo vinchi vya Zanzibar na Pemba vikiachiwa kupanga na kupangua vinaweza kujigeuza Dubai au Sharijah fumba na kufumbua. Vinginevyo, ngoja 2010 Rwanda wanakuja na Dubai kati ya Afrika. Nchi hii (Orijinoo Komedii: Enzi za Mwalimu:-Wizi Mtupu!).
Hakuna lilinifurahisha kama kukuta wakati sisi tunashikwa na kigugumizi kuhusu maBMW, maToyota VX na mashangingi mengine yanayokunywa kama sio kufakamia mabilioni ya fedha katika peteroli na spea pati wao walichukua miezi mitatu tu kupanga na kupangua shughuli hiyo ya magari. Kila mtumishi wa umma aliyejaza fomu alipewa mkopo akanunua gari lake mwenyewe na waliozembea siku ya siku, yaani, ilipofika siku 90 juu ya mshale kama sio mkuki mawaziri na wakuu wengine waliojisahau walijikuta wakirudi nyumbani kwa mguu.
Nidhamu sisi hatuna. Tutayaweza haya. Utawala wa kisheria ni bongo fleva ambayo wakuu hawana hata habari nayo. Na nchi inakwenda kwa kudra ya Muumba, lakini, itafika muda tabia hii itatuumbua!
Tupende tusipende, ukiwa huna kiongozi wa juu anayefaa iwe TANESCO, POSTA, TRL, mkoani, wilayani, wizarani na kadhalika ni kazi ngumu kweli kuleta maendeleo.
Na pengine wakati umefika tuanze kuzungumza vipi Watanzania tuliowasaidia wengi kujitawala au kujikomboa kwa hili au lile tumekuwa ndio watu wa mkiani kimaendeleo miaka yote hii. Tuzungumze: TATIZO AU MATATIZO YETU NI YAPI? NA DAWA YAKE NI IPI?