State sponsored genocide in MAFIA ISLAND (?) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

State sponsored genocide in MAFIA ISLAND (?)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Game Theory, Dec 24, 2008.

 1. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Hivi serikali inapoamaua kwa kusudi kuwazuia wananchi wa kisiwa cha mafia wapatao 40,000 wasivue samaki maana yake ni nini? surely this is a clear road to STATE SPONSORED GENOCIDE KULE KISIWANI MAFIA...if not GROSS human rights violations na mbaya zaidi wanajeshi wamefika kule wanawapiga watu na kuwaumiza vibaya kisa wamepatikana na nyavu za kuvulia samaki

  Serikali inapowaambia wanachi wavue samaki kwa ndoano maanake ni nini hasa?

  Serikali inapowaambia wananchi wasitumie nyavu ndogo kuvua samaki inategemea wananchi wa MAFIA wasile dagaa au vipi?

  Na sharti la kuwaambia wananchi wakitaka kuvua waende deep sea nalo haliingiii akilini maana tunajua hakuna raia mwenye chombo cha kwenda kuvua deep sea kule mafia

  Mbaya zaidi kuna taarifa kuwa kuna watu washaanza kudhoofika kwa njaa baada ya kupigwa marufuku kuvua samaki

  Nakumbuaka ma environmentalists walivyopiga makelele kuhusu mradi wa kamba na naona this time wamerudi tena back door bila kuwafikiria raia wa mafia kwa kulobby raia wapigwe marufuku kuvua samaki


  No wonder jamaa wa human rights watch wameamua kupiga kambi pale kisiwani kukusanya ripoti yao
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  imagine mfugaji kule Arusha kuambiwa asifuge na huku wanajeshi wanatumika kumwambia asifanye hivyo...hii ni goood recipe for disaster
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Ni kwamba serikali inataka kuhakikisha kuwa hao samaki wanaowategemea wanaendelea kuwapo hata kwa wajukuu wao!
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2008
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  cja kuelewa
   
 5. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Samaki katika eneo la Mafia wanakuwa over-fished kiasi cha kwamba hawapati nafasi ya kuzaliana. Nyavu ndogo zinazuiwa kwa sababu hiyo hiyo ili samaki wadogo wapate nafasi ya kukua na kuzaliana. Kwa maneno mengine wakiendelea kuvua walivyozoea hivi karibuni tuu hata hao samaki watapungua kiasi cha kutowatosheleza kizazi kijacho.

  Kama vile uzalishaji wa kamba ungeongeza sumu katika mazalio ya samaki kiasi cha kufanya sehemu iwe mfu. Sehemu zote ambako biashara hii imefanyika, matokeo yake ni kuwa baada ya muda hakuna cha samaki wala kamba wanaopatikana. Wawekezaji hao wanajiondokea na kuwaachia wakazi na bahari yao iliyokufa!

  Amandla.........
   
 6. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #6
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huwezi kuzuia uvuvi wote kwa nyavu ndogo. Manake si samki wote huwa wanakuwa wakubwa, mfano Uduvi, dagaa, soga nk. Hivyo kinachotakiwa kufanywa na Serikali ni kusema kuwa ni wakati gani ambao uvuvi unatakiwa kusimamishwa ili kutoa muda kwa samaki kukua. Hii inatokana na tafiti zilizofanywa kujua ni wakati gani samaki wanazaliana na kutoka hapo unawekwa muda ili wakue. Ama jambo jingine ni kuanzisha "No fishing zones" (maeneo ambayo hayavuliwi kabisa) ili kuwa ndio matagio na sehemu za kukulia samaki. Ila huwezi ukaja na sheria tena unatumia jeshi kuzuia nyavu ndogo, kila mtu anajua kuwa nyavu ndogo zinavua samaki wadogo, lakini si kila samaki mdogo huwa hajakomaa ama kukua kiumri.

  Hivyo kwa hili Serikali inachemsha kuzuia moja kwa moja nyavu ndogo. Kwani Taasii ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (Tanzania Fisheries Research Institute-TAFIRI), Kitivo cha Sayansi maji na Teknolojia (Faculty of Aquatic Science and Technology-UDSM), Taasisi ya Sayansi ya Bahari (Institute of Marine Science-IMS Zanzibar) na hata Kitengo cha Uvuvi (Fisheries Department) Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi wana kazi gani?. Wao ndo wanatakiwa kufanya utafiti na kuishauri Serikali ni jinsi, wakati, mahala na nyenzo gani Wananchi watavua samaki bila kuathiri sana mazao yatokanayo na bahari, maziwa na mito.

  Lakini kama nchi inaendeshwa kisiasa zaidi bila kufuata ushauri wa wataalamu wetu wa mambo hayo ni ujinga mtupu. Sasa tunatumia fedha zote kusomesha wataalamu wa fani mbalimbali kwa ajili gani?, kama hatuwatumii kutoa ushauri ama hatufuati wanayoshauri?.
   
 7. Mtanganyika

  Mtanganyika JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2008
  Joined: Jul 18, 2007
  Messages: 1,613
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 180
  GT
  Mzee nadhani sababu kubwa ni kwamba marine species wako in danger huko mafia. Nadhani serikali imechukua hatua hizi kutokana na wavuvi kuto kuthamani kwamba kuvua samaki wadogo kunaweza kuleta madhara katika ecosystem nzima.

  Katika upande mwingine wa shilingi, nadhani measurement walizochukua serikali zinaonyesha kuwa za kibabe zaidi.
   
 8. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #8
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mtanganyika, kuna masuala mawili hapa, kuna samaki wadogo (small fish) na samaki wasiopevuka/hawajakuwa (immature/juvenile fish). Hivyo huwezi zuia samaki wote wadogo kuvuliwa kwa kuwa kutasababisha uharibifu wa mazingira, lakini unatakiwa kuwa na vigezo watu wasivue samaki wasiopevuka, na hii ndio inafanyika sehemu nyingi duniani. Sio kuzuia samaki wote wadogo kuvuliwa. Manake si samaki wote wadogo hawajapevuka.
   
 9. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mfumwa.

  Una uhakika gani kuwa serikali haijafanya hicho unachosema? Kwamba serikali inatoa muda ili samaki WOTE waweze kupata nafasi ya kukua na kuongezeka? Sisi hatuna Coast Guard sasa kuna ubaya gani kutumia jeshi kuhakikisha kuwa sheria inafuatwa? Unless kama hao wanajeshi wanatumia "violence" kufanya hivyo!

  Hapo hapo Mafia kuna kituo cha Mafia Island Marine Park ambacho kina wataalamu wa masuala ya uvuvi. Hawa bila shaka ndiyo waliotoa ushauri wa kuzuia uvuvi wa nyavu ndogo. Bila shaka baada ya kuona kuwa hatua nyingine ni vigumu kuzitekeleza.

  Kusema kuwa hauwezi kuzuia uvuvi wote wa nyavu ndogo sio sahihi. Mbona nchi nyingi zimefanya hivyo ilikuokoa samaki wao? Ninavyojua mimi ni kuwa hakuna nyavu zilizo selective ambazo zitaweza kuainisha kuwa huyu ni samaki mchanga na huyu amekomaa lakini ana umbo dogo. Basi si bora kuwaachia wote waishi? Wadogo na hao ambao wamekomaa lakini wana umbo dogo?

  Ukweli unabaki pale pale. Samaki wetu wako hatarini na ni lazima serikali ichukue hatua ya kuwalinda. Hatusaidii kwa kudai kuwa ati kuna genocide inaendelea! Si kila kitu kifanywacho na serikali ni kiovu.

  Amandla........
   
 10. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Fundi Mchundo, sio kwamba nataka tubishane ni kueleweshana kwa njia ya mjadala. Serikali kama ingefuata ushauri sidhani kama ingefikia kuzuia nyavu zote ndogo na kusema itumike ndoana wakati kuna samaki sharti wavuliwe na nyavu ndogo na huwa wameshakuwa japo kimaumbile ni wadogo. Kutoa muda ni kama nilivyoeleza post iliyopita, unaweza sema mwezi fulani mpaka fulani inazuiliwa kuvua ili samaki wakue, ama unaweza tenga maeneo maalum ambayo hayavuliwi kabisa kutoa nafasi samaki kuzaana na kukua. Unaposema hatuna Coast Guard unaongopa, tunavyo vitengo vya ulinzi vinavyoratibiwa na Fisheries Department kwa kila maziwa na baharini pia. Mikoani viko chini ya maafisa uvuvi wa mikoa. Na vile vile kama ulivyosema kuwa Mafia kuna kituo cha Mafia Island Marine Park , hawa wana watu wanaitwa "Park Rangers" kazi zao ni ulinzi wa Rasilimali zipatikanazo majini na maeneo yanayozunguka. Hivyo kutumia jeshi labda wamezidiwa iwe wamezidiwa nguvu, ama hawa wavuvi wanatumia silaha nzito za kijeshi, ama wako wachache ikawa hamna budi, hapo ni sawa.

  Nakumbuka jeshi liliwahi tumika sana mwambao wa Dar es Salaam kuzuia waliokuwa wanatumia mabomu kuvua samaki katika Matumbawe (Coral reefs), na lilisaidia sana, lakini hii ilikuwa ni "sensitive issue", mtu anatumia Mabomu. Ndio maana jeshi lilitumika.

  Nchi nyingi hazizuii nyavu ndogo, bali unatakiwa uwepo utaratibu wa kuzitumia. Kuhusu samaki kuwa hatarini sikatai, sio kwetu tu ni dunia nzima. Mfano hata Japan Nyangumi wako hatarini sababu ya kuvuliwa sana. Hivyo dawa ni kuwa na njia mbadala ambayo itaongeza samaki bila kuathiri wananchi. Ni ujuha wananchi wakose shughuli ya kiuchumi ili samaki wakue, wakati wananchi ndio wanaotegemewa kufanya kazi ili kukuza pato la Taif.
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mfumwa.

  Sidhani kuwa unataka kuleta ubishi. Kutokana na maelezo yako naamini ni kweli una ujuzi kuhusu suala hili ambao wengi hatunao.

  Tunapotofautiana ni pale unaposema kuwa kuna njia mbadala za kuhakikisha uhai wa samaki hawa ambazo serikali ilipaswa kutumia kabla ya kuzuia uvuvi wa nyavu ndogo. Imani yangu ni kuwa kwa sababu hao watu wa Mafia Marine Park wapo pale basi bila shaka hizo njia unazoshauri waliona hazitakuwa na mafanikio wanayotarajia katika wakati walio nao. Hawa wapo muda mrefu tuu pale Mafia na ni lazima hizo hatua wamejaribu bila mafanikio.

  Ni juu yetu kama wataalamu kuwafahamisha wananchi kuhusu nia ya hatua kama hizi badala ya kubeba mabango kudai kuwa kuna mpango wa Genocide dhidi yao! Genocide ni neno zito sana na halipaswi kutumika hapa. Kwa kufanya hivyo, hatuwatendei haki ndugu zetu!

  Amandla.....
   
 12. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #12
  Dec 24, 2008
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Fundi Mchundo, nikisema ukweli sina ujuzi wa mambo hayo, ninajaribu tu kufikiri na kuangalia hali halisi. Haya ngoja nikubaliane nawe kuwa hawa jamaa (Mafia Marine Park) ndio waliotoa huo ushauri baada ya njia nyingine kutoleta suluhisho. Lakini ukumbuke yawezekana ushauri huu ukiingia kwa ndani unaweza kuta unawasaidia wale wenye mameli makubwa ya kuvua samaki (kama kamba nk) kule, yaweza fananishwa na wale watoao ushauri kwa sekta za madini. Lakini baadae tutajua ni nani yuko nyuma ya hili suala, ni suala la muda japo Wananchi wanaumia. Kusema ni "Genocide", hata nami nachelea, lakini muanzisha mada huenda ana wazo zuri kutumia hilo neno kuvuta hisia.

  Muito Obrigado...
   
 13. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #13
  Dec 24, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Mfumwa. Uamuzi huu wa kuzuia nyavu ndogo utawasaidia vipi hao wenye trawlers? Wao nao si waliishapigwa marufuku kutumia nyavu ndogo na NDEFU?
   
 14. S

  Sammy Sr. Member

  #14
  Dec 24, 2008
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikoa kama nchi ndogo ndani ya Tanzania

  ZIARA yangu hivi karibuni huko Rwanda kanchi kadogo pembezoni mwa Tanzania imenionesha kwamba Watanzania tunacheza na sio serious kuihusu maendeleo yetu.

  Ningeliomba wana JF mfanye mpango mkawaoneshe viongozi wetu uchawi Rwanda inayoufanya leo ili kesho na kesho kutwa wakiendelea EPA, Richmond na Dowans zao wasijeshangaa Rwanda ina register GDP per capita ya $ 5,000 wakati sisi tunalemaa lemaa katika $600 mwaka nenda, mwaka rudi.

  Kama Rwanda nchi ndogo kuliko mkoa wa Mwanza na yenye rasilimali ndogo kuliko mkoa wa Mwanza inaweza kufanya inachokifanya tatizo letu jama ni nini?

  Kwanza, hatujatambua tunakotaka kwenda. Pili, tunawaweka mbele sana Wazungu na mawazo yao yasiyo ya kina na uzito katika mazingira yetu mbele mbele mno kama vile sisi wenyewe hatuna kimbelembele! Kwenye siasa lakini......

  Wao wana magavana sio wakuu wa mikoa. Hawa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya mimi naona vile wamekuwa breki kwenye maendeleo ya mikoa na nchi kwa ujumla. Nadhani inafaa sasa tuwe na tuongozi tudogo tunakochaguliwa na wakazi wa mkoa ili mambo yasiwe yanakwenda kama kawa hata aingie au atoke mkuu huyu mambo ni yale yale wakazi hawaoni kifuu wala nafuu!

  Nina hakika kuna mikoa hapa ikiwemo vinchi vya Zanzibar na Pemba vikiachiwa kupanga na kupangua vinaweza kujigeuza Dubai au Sharijah fumba na kufumbua. Vinginevyo, ngoja 2010 Rwanda wanakuja na Dubai kati ya Afrika. Nchi hii (Orijinoo Komedii: Enzi za Mwalimu:-Wizi Mtupu!).

  Hakuna lilinifurahisha kama kukuta wakati sisi tunashikwa na kigugumizi kuhusu maBMW, maToyota VX na mashangingi mengine yanayokunywa kama sio kufakamia mabilioni ya fedha katika peteroli na spea pati wao walichukua miezi mitatu tu kupanga na kupangua shughuli hiyo ya magari. Kila mtumishi wa umma aliyejaza fomu alipewa mkopo akanunua gari lake mwenyewe na waliozembea siku ya siku, yaani, ilipofika siku 90 juu ya mshale kama sio mkuki mawaziri na wakuu wengine waliojisahau walijikuta wakirudi nyumbani kwa mguu.

  Nidhamu sisi hatuna. Tutayaweza haya. Utawala wa kisheria ni bongo fleva ambayo wakuu hawana hata habari nayo. Na nchi inakwenda kwa kudra ya Muumba, lakini, itafika muda tabia hii itatuumbua!

  Tupende tusipende, ukiwa huna kiongozi wa juu anayefaa iwe TANESCO, POSTA, TRL, mkoani, wilayani, wizarani na kadhalika ni kazi ngumu kweli kuleta maendeleo.

  Na pengine wakati umefika tuanze kuzungumza vipi Watanzania tuliowasaidia wengi kujitawala au kujikomboa kwa hili au lile tumekuwa ndio watu wa mkiani kimaendeleo miaka yote hii. Tuzungumze: TATIZO AU MATATIZO YETU NI YAPI? NA DAWA YAKE NI IPI?
   
 15. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2008
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mzee Sammy Sr,
  Ingawaje uko nje ya Mafia topic...unayosema over Rwanda ni kweli tupu! Nasema ahsante sana kwa mawazo ya uzalendo...Inshalah iko siku nasi tutaamka tu!

  Tz is a sleeipng giant...taabu je tutaamka lini?
   
Loading...