uchaguzi ndo huo umeisha na CCM kuingia madarakani kupitia kura za wananchi na pia kufanya ujanja maeneo kadhaa.
Kama kawaida yetu tutasahau haraka na maisha kuendelea na wananchi kuanza kulalamikia hali mbali ya maisha..
mimi sitashangaa yafuatayo kutokea:
- Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kusikitishwa na uteuzi wa nafasi mbalimbali utakaofanywa na JK... utasikia wanasema du kawaweka maswahiba wake
- sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kulalamikia rushwa kushamiri Tanzania .. kama kwamba walikosa mbadala wa kumweka uongozini kupambana na rushwa kwa umakini zaidi ..
- sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuanza kulalamikia hali ngumu ya maisha.. ngoja nitoe scenario moja: chadema wana sera ya elimu bure hadi kidato cha sita (6) kama si chuo kikuu. lakini sitashangaa walioinyima kura Chadema kuanza kuja kwako kukupigia magoti kuomba msaada wa kifedha ili apate ada ya kumpeleka mtoto sekondari.
- Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM waliokuwa wanavaa sare na kucheza kama hawana akili nzuri wakati wa mikutano ya kampeni kuendelea kuwa katika hali zao duni............ why? kwa sababu serikali imeshindwa kuwa visionary
- Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuendelea kuishi katika nyumba za mbavu za mbwa (kama ile tuliyooneshwa wakati wa kampeni ikiwa na bango la JK) wakati wamekataa kumpigia kura Dr. Slaa aliyekuwa ameahidi kushusha bei ya saruji (cement) ili wananchi walio wengi waweze kujenga nyumba imara na bora
- sitashangaa wanachi mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia ukosefu wa dawa hospitalini..
- Sitashangaa wananchi mashambiki wa CCM kuendelea kulalamikia vitendo vya rushwa mahakamani na polisi
- sitashangaa wananchi na mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia utendaji mbovu wa idara mbalimbali za serikali (kumbuka jinsi Clouds walivyokuwa wanachambua utendaji mbovu wa idara mbalimbali e.g. EWURA, DAWASCO, TANESCO lakini wakawa vuvuzela wa CCM wakati wa uchaguzi)
- Sitashangaa wapenzi wa CCM kulalamikia mishahara wanayopata na wakati huo huo kulalamikia posho kubwa za viongozi
- sitashangaa watu hawa kuvaa ma- Tshirt, kofia na kanga 2015 kushangilia na kushabikia CCM wakati wa uchaguzi mwingine
kutokana na hili naomba tushirikiane pamoja kuzidi kutoa elimu ya uraia, ipo siku yatabadilika ... "YANA MWISHO" (nukuu toka kitabu cha KULI)