Stashangaa washabiki wa CCM na JK kufanya yafuatayo!!! SOMA NA TAKAFAKARI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stashangaa washabiki wa CCM na JK kufanya yafuatayo!!! SOMA NA TAKAFAKARI

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kanyagio, Nov 7, 2010.

 1. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #1
  Nov 7, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  uchaguzi ndo huo umeisha na CCM kuingia madarakani kupitia kura za wananchi na pia kufanya ujanja maeneo kadhaa.

  Kama kawaida yetu tutasahau haraka na maisha kuendelea na wananchi kuanza kulalamikia hali mbali ya maisha..

  mimi sitashangaa yafuatayo kutokea:


  1. Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kusikitishwa na uteuzi wa nafasi mbalimbali utakaofanywa na JK... utasikia wanasema du kawaweka maswahiba wake
  2. sitashangaa wananchi washabiki wa CCM kulalamikia rushwa kushamiri Tanzania .. kama kwamba walikosa mbadala wa kumweka uongozini kupambana na rushwa kwa umakini zaidi ..
  3. sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuanza kulalamikia hali ngumu ya maisha.. ngoja nitoe scenario moja: chadema wana sera ya elimu bure hadi kidato cha sita (6) kama si chuo kikuu. lakini sitashangaa walioinyima kura Chadema kuanza kuja kwako kukupigia magoti kuomba msaada wa kifedha ili apate ada ya kumpeleka mtoto sekondari.
  4. Sitashangaa wananchi washabiki wa CCM waliokuwa wanavaa sare na kucheza kama hawana akili nzuri wakati wa mikutano ya kampeni kuendelea kuwa katika hali zao duni............ why? kwa sababu serikali imeshindwa kuwa visionary
  5. Sitashangaa wananchi mashabiki wa CCM kuendelea kuishi katika nyumba za mbavu za mbwa (kama ile tuliyooneshwa wakati wa kampeni ikiwa na bango la JK) wakati wamekataa kumpigia kura Dr. Slaa aliyekuwa ameahidi kushusha bei ya saruji (cement) ili wananchi walio wengi waweze kujenga nyumba imara na bora
  6. sitashangaa wanachi mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia ukosefu wa dawa hospitalini..
  7. Sitashangaa wananchi mashambiki wa CCM kuendelea kulalamikia vitendo vya rushwa mahakamani na polisi
  8. sitashangaa wananchi na mashabiki wa CCM kuendelea kulalamikia utendaji mbovu wa idara mbalimbali za serikali (kumbuka jinsi Clouds walivyokuwa wanachambua utendaji mbovu wa idara mbalimbali e.g. EWURA, DAWASCO, TANESCO lakini wakawa vuvuzela wa CCM wakati wa uchaguzi)
  9. Sitashangaa wapenzi wa CCM kulalamikia mishahara wanayopata na wakati huo huo kulalamikia posho kubwa za viongozi
  10. sitashangaa watu hawa kuvaa ma- Tshirt, kofia na kanga 2015 kushangilia na kushabikia CCM wakati wa uchaguzi mwingine
  kutokana na hili naomba tushirikiane pamoja kuzidi kutoa elimu ya uraia, ipo siku yatabadilika ... "YANA MWISHO" (nukuu toka kitabu cha KULI)
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,316
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa ni kuwa hatujui hata kama kweli tuwalaumu hawa watu kwa sababu hatujui hata kama kweli walikipigia kura CCM au ni NEC imetupandikizia JK na askari wake wa kimamluki kutuongoza isivyo halali na kinyume cha sheria.......kutokana na mazingira haya siyo kosa kuwapigajeki jamaa hawa walalahoi wa CCM kwa sababu hata wao ni waathirika wa mfumo kandamizi wa CCM na JK wake...............
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Kama vile ina mvuto flani hivi....ngoja niende ibadani nikirudi nitacomment
   
 4. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  CHADEMA IMEKAMATA ARUSHA NA MWANZA, na pia manispaa nyengine.

  Kwenye maeneo hayo, inaweza kusimamia sera zake.

  TUONE KAMA ITAFANIKIWA kwenye Local Governments ilizokamata.

  Utendaji unatakiwe uwe demonstrated sio maneno maneno.

   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Inasemekan watanzania ilimradi kuwe na amani tu hata wakila nyasi kwo sio tatizo, hata mafisadi watumie mabilioni kujinufaisha wao watanzania wala hawana wasi ili mradi amani ipo.
   
 6. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #6
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu uliyoandika ni ukweli mtupu kwa sababu umereflect tabia za Watanzania - Wachaguaji wabaya, walalamikaji wazuri. Yote uliyotaja tutayaona hivi punde.
   
 7. 3D.

  3D. JF-Expert Member

  #7
  Nov 7, 2010
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 1,022
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni kweli. Kinachosababisha haya kwa kiasi kikubwa ni Watanzania kuwa "watiifu mno" kwa viongozi wa dini, kila watakachoambiwa na viongozi hawa wanakitekeleza bila kujiuliza.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Nov 7, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Unataka Chadema wademonstrate uwezo wao mara ngapi! Nenda kaangalie wilaya ya Karatu! Umeona mji wa Moshi ulivyo msafi na chadema inaongoza pale sasa linganisha na uchafu wa jiji lenu la DAR!!
   
 9. Makame

  Makame JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unachotaka ni kwamba watu wafanye VURUGU na FUJO zisizo maana?

  MWANZA MJINI, Ilemela na Nyamagana; wakati KURA zinahesabiwa; WANACHADEMA walifanya uharibifu wa mali; hivi huo ni uungwana? Kisa cha Vurugu hizo? Ni barua iliyochakachuliwa na Dk Slaa [Cheki thread ya Dk Slaa amechakachua Barua]. Do you really want people to demonstrate againstthe VOTE of MAJORITY?

  Mahitaji ya maendeleo siku zote yatakuwepo, hata atawale nani hapa; hakuna atakaegeuza TZ pepo. Wananchi wamefanya chaguo lao; walipofanya hivyo walijua kuwa kuna wengine; bali waliamua kumchagua JK kwa kuwa waliona ndio best of the contestants.

  Vyama vyote vimekubaliana na matokeo kasoro CHADEMA. sasa ni nani Un Democratic?

  Please mates!

   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280
  Mkuu washaanza kulalamika tayari. Je, hukuona taarifa ya habari TBC1 juzi saa 2 usiku? juu ya bei ya mfuko mmoja wa simenti kuuzwa Tshs 20,000= huko Songea?

  Halafu mama Ishengoma (Kaimu RC) anawataka wafanyabuashara kushusha bei, nawao wakadinda!!

  Maumivu ni kwetu sote Watanzania uwe CCM, CHADEMA, CUF, TLP, NCCR hapa ndo panaponifurahisha!!!!!!!!!
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2010
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ndio watz walivyo wala sishangai kabisa..duh
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Ulitaka watu waende nyumbani ili mumrudishe Masha mjengoni sio? Simply vurugu zimesababishwa na nec kutokana na shinikizo la chama tawala pale kuknkoonekana upinzani ni mkali. Walikuwa waaangalia possibility ya kuchakachua na ndio maana watu walikosa uvumilivu. Mbona majimbo ambayo ccm ilishinda majibu mara moja?? Ubungo, Kawe, Arusha, Segerea na mengine meeeengi eti ndio wanahesabu kura. Try to be realistic !!!!!
   
 13. v

  vassil Senior Member

  #13
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 121
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  huu mtandao umevamiwa na mataahira ya ccm tafadhali nendeni mkae na genius wenu dr kikweche
   
 14. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #14
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Si mara ya kwanza kwa chadema kushika uongozi wa manispaa na uzoefu unaonyesha ndio halmashauri pekee zilizofanya vizuri kuliko hizo zenu za ccm. Na ndio sababu zote hata ambazo mbunge katoka ccm bado zitabaki chini ya chadema. Subiri upate shule sio longo longo zenu.
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Nov 7, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Basi wakamfungulie mashitaka ya kuchakachua barua mbona wanaogopa?
   
 16. Kisima

  Kisima JF-Expert Member

  #16
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 3,768
  Likes Received: 2,222
  Trophy Points: 280
  Makame ubongo wako ni mfu! Ntakusimulia kisa cha wakulima wawili wa mahindi;
  ''mulima1: yeye alipalilia shamba lake vizuri kuzuia magugu yasizoofishe mazao lakini akaghaili kulinda shamba lake lisivamiwe na ngedere matokeo yake ngedere walishambulia mazao yote.
  Mkulima2. Yeye hakujihusisha sana na palizi ila alilinda shamba lake licvamiwe na ngedere, japo mazao hayakusitawi vizuri ila alifanikiwa kuvuna japo mazao kidogo kuliko mkulima wa kwanza'' makame, unajifananisha na yupi kati ya wakulima hawa?
   
 17. S

  Sitakioa Member

  #17
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo makame kaniboa hadi nahc usingizi.hivi wewe unamiliki viwanda vingapi?au gari kumi na ngapi?unataka kujifanya unaipenda sana ccm ee?kuwa na watu 1000 kama wewe wenye mawazo hayo bora tuwe na nguruwe milion miamoja nchini.think bro kwanini tuendelee kuteseka kiasi hiki wakati kila kitu tunacho?acha kuundergrade ubongo wako makusudi huku hali halisi unaiona.
   
 18. Ulimate4

  Ulimate4 Member

  #18
  Nov 8, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Arusha wamejiponza wenyewe,kwa sifa za kutaka mabadiko bila ya kuzisikiliza sera na kuzipembua ,wakafuata ushabiki na kumchagua mbuge hewa mwenye elimu ya darasa la 7,sasa sijui ni mabadiliko ya aina gani wanategemea kuletewa na mbunge huyo.
  Tutegemee vituko toka mule mjengoni.
   
 19. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #19
  Nov 8, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Hata mimi sitashangaa. Na sitashangaa kama huyu Makame ndani ya JF anayetetea CCM na NEC akiwa ndo Lewis Makame mkurugenzi wa NEC au ndugu yake flani!!
   
 20. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #20
  Nov 8, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Unapoteza muda wako bure!!! Jaji Mstaafu Makame ni mzee sana!! Sidhani hata huwa naingia humu kusoma!!!

  Keshajiishia...:doh:
   
Loading...