StarTV ni hovyo, hamvumliki: Wapi tamithiliya ya "NO GREATER LOVE?"

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,541
Kituo cha luninga cha StarTV huwa kina kipindi cha tamithiliya siku za jumanne na ijumaa kuanzia saa 3:30 - 4:30 usiku, jumamosi na jumapili kuanzia saa 3:00 -4:00 usiku.

Mara nyingi hupendelea kurusha tamithiliya za Kifilipino na mara chache za ki - Mexico. Kwa sasa wanarusha tamithiliya ya Kifilipino iitwayo NO GREATER LOVE.

Lakini kinachosikitisha ni kituo hiki cha luninga kutokuwa kwao consistent na vipindi vyao hususani vya tamithiliya.

Kwamba jamaa huwa wanaanza vizuri tu kwa matangazo ya kuitangaza sana tamithiliya hiyo kwamba itaanza kurushwa siku na tarehe fulani.

Siku na terehe hufika na kuanza kurushwa hewani. Lakini ghafla husitisha tena ikiwa imefikia sehemu nzuri kabisa na sisi watazamaji tukiwa na hamu ya kujua nini kitajiri episode inayofuata.

Huku ukiwa umeseti ratiba yako kulingana na muda wa kuanza kwa kipindi unashangaa kukutana na tangazo lisemalo;

"Kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu, leo hatutakuwa na tamithiliya ya........endelea kutazama vipindi vingine vya StarTV"

Binafsi huwa inaniudhi sana kwani haitokei mara moja au mbili bali ni mara nyingi sana tu!

Mfano, kama nilivyosema mwanzo, kwa sasa wana tamithiliya inayorushwa na kituo hicho itwayo NO GREATER LOVE.

Ni nzuri sana na ina madhui mazuri juu ya mahusiano ya mapenzi, ukatili, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka dhidi ya watawala.

Mimi ni mfuatiliaji mzuri wa story hii, lakini ni wiki ya tatu sasa hawa jamaa hawairushi tena na wametuacha watazamaji wao ktk dilemma kubwa na hakuna sababu hasa ya msingi wanayotupa ili tuwaelewe.

Mimi kwangu natumia king'amuzi cha Dstv ambamo ndani yake StarTV imo - channel ya 291.

Inawezekana na naanza kuhisi labda wameihamishia ktk moja ya channel zao za king'amuzi cha Continental na kwa hiyo wanataka kila mtu awe nacho.

Itawezekana vipi iwe hivyo? Na kama ni kesi hiyo basi, ondoeni channel yenu hii ktk ving'amuzi vingine ili tujue moja na tusiwaone kabisa!

Pia nichukue fursa hii binafsi kuwapongeza ITV kwani nao wana kipindi cha Tamithiliya za ki - Mexico (telenovela) kila j3, j4 na j5 kuanzia saa 4:00 usiku na Kwa sasa tamithiliya iliyo hewani inaitwa "La Garta - The Stray Cat"

Hawa jamaa wako very consistent, haitokei hata siku moja ktk seting ya ratiba yao wakashindwa kuirusha.

Hata kama kuna kipindi cha dharura mara kinapoisha, huwa lazima wairushe hata kwa kuchelewa. Huu ndiyo uungwana kwa sababu wanajali watazamaji wao na pia kuthamini muda wao.

Lakini StarTV hebu jirekebisheni au acheni kuanzisha vipindi ambavyo hamna uwezo wa kuvi maintain ili viwe hewani. Na lazima mfahamu kuwa bila watazamaji hakuna maana ya kuwa na kituo cha luninga. Kwa hiyo hebu tunaomba mtuheshimu na kuthamini muda wetu tunaotenga kufuatilia kipindi fulani!!
 
KTN ya Kenya iliisha kabisa lakini star tv walisema kesho tarehe 26-2-2016 itaanza kuonyeshwa. Ofcourse ya Itv iko vizuri sana na hawajawahi kutoionyesha! Stray cat pia inaonyeshwa citizen tv saa mbili na robo usiku! Sema wao wako mbele sana! Pole mkuu naona tamthiliya pia ni ugonjwa wako kama mie!
 
Back
Top Bottom