StarTV Live: Uwajibishwaji Viongozi wa Halmashauri nchini

Halafu Star tv pls ongezeni Muda hadi hata sa tatu na nusu ili muweze kuwapa muda wa kutosha wageni hapo na pia mpate muda wa kusoma michango yetu wote hapa. Isiwe ni useless kutoa maoni yasiyosomwa..

Salamu kwa Chagulani, nimesoma naye UDSM... he's a strong Man
 
Wapinzani hata wakipata nchi hawatalindana mfano ndio huu,kwani unazani hizo halmashauri zinazoongozwa na ccm hazina ubadhilifu? upo lakini ndo wanabebana nakufichana
 
Kaka nimekuambatanishia an EXTRACT FROM SOCIAL ACCOUNTABILITY REPORT OF MWANANZA CITY COUNCIL IN 2008 By Marcossy Albanie inayoonesha kuwa mambo haya Mwanza yalianza zamani isipokuwa waliokuwepo madarakani wakati huo walifumba macho.

(Although over 50% of the section's allocation goes for Salaries and the payment of salary arrears, the plan for utilization of the remaining 65 mil TZS was expected to focus on services and activities supporting eradication of adult illiteracy).
 

Attachments

  • EXTRACT FROM SOCIAL ACCOUNTABILITY REPORT OF MWANANZA CITY COUNCIL IN 2008.docx
    74.9 KB · Views: 52
Mtangazaji,

Hali inaendelea kwenye halmashauri kwa sasa ni ukomavu wa demokrasia na tunatakiwa tuwaunge mkono na siyo kulalamika. Haijalishi mtuhumiwa ni wa chama gani maana kwenye vyama siyo mbinguni.

Wengi wenye madaraka katika vyama wanaharibu sifa za vya kwa kuweka maslahi yao binafsi mbele. Hii haivumiliki na haitavulika. Na itikadi za chama haziwezi kuwa machela ya kuwahifadhi wahalifu.

Kirokolo, Hakuna anayelalamika, ukomavu wa demokrasia hapa ni upi? kwamba sasa tunapata taarifa nyingi za wizi kwenye halmashauri kuliko tulivokua tunapata zamani? haiwezekani kwamba sasa wizi ndio umeongezeka na ndio sababu tunasikia sana kuhusu ubadhirifu?

Tunapoteza muda kujadili wanaokwapua rasilimali zetu badala ya kutumia muda huo kuweka mipango ya maendeleo, hii si kitu kizuri, inabidi kudhibiti watu wasio na uadilifu kuingia kwenye uongozi, uwe wa kata, halamashauri au nchi
 
Jambo jingine ambalo serikali inatakiwa kuliangalia upya, ni mamlaka na madaraka ya madiwani kwenye utendaji wa halmashauri. Madiwani wengi wana uwezo mdogo wa kiutendaji na uelewa wa mambo. Wamefanya halmashauri kuwa chaka lao la uhalifu na uhujumu wa fedha za umma.

Wakurugenzi wengi wa halmashauri wamekwamishwa na madiwani kutekeleza majukumu yao kwa kuwa hayana maslahi binafsi wa baadhi ya madiwani ambao ni mafisadi. Madaraka ya madiwani yapunguzwe!
 
Serikali yetu inatakiwa kutambua kuwa kushuka kwa kasi kwa imani ya wananchi kwa serikali yao na viongozi wao inatokana na uchafu na ubadhirifu mkubwa unaofanyika ktk halmashauri zetu na kwa kiasi kikubwa kwa kusababishwa na madiwani wetu na watendaji wa chini ambao wengi hulindwa na baadhi ya madiwani kwa maslahi yao binafsi.

Tubalike sasa na tubadili muundo wa kiutendaji wa mabaraza ya madiwani.
 
Hizi halmashauri zimezidi kula pesa, tena wanazitafuna wazi. Kuna H/M huku singida inalalamikiwa na kila mtu si watumishi hadi wananchi wa kawaida, hizi halmashauri zinapaswa kuchunguzwa
 
Halafu Star tv pls ongezeni Muda hadi hata sa tatu na nusu ili muweze kuwapa muda wa kutosha wageni hapo na pia mpate muda wa kusoma michango yetu wote hapa. Isiwe ni useless kutoa maoni yasiyosomwa..

Salamu kwa Chagulani, nimesoma naye UDSM... he's a strong Man

JUMAPILI ratiba yetu imebanana sana tutajitahidi kufukuzana na muda kwa kadiri tuwezavyo
 
Kwakuwa kumekuwepo na tuhuma za rushwa dhidi ya kamati kadhaa za bunge na baadhi ya wabunge, mathalani tuhuma za rushwa dhidi ya kamati za bunge za madini na nishati, maendeleo ya jamii na mashirika ya umma, na mbunge Kafulila aliwahi kuwataja baadhi yao bungeni, na mmojawao amefikishwa mahakamani hivi karibuni kwa tuhuma za rushwa.

Kwanini spika wa bunge akubali kuvunja kamati ya nishati na madini pekee huku akiziacha kamati za maendeleo ya jamii pamoja na kamati ya mashirika ya umma? Hapo spika analindaje maslahi ya nchi kwa kutovunja kamati ambazo haziaminiwi na wananchi?
 
Mwanza:

Mtaa wa Lumumba, Msikiti wa Ijumaa, Mlango Mmoja na mbele ya Oryx Pamba walimwaga zege kuziba mashimo badala ya lami na sasa mashimo yamerudi kwa kasi; angalia hata zinapotokea daladala za Airpot pale mjini kati ni mashimo tu, diwani wa hii kata awajibike
 
Mimi pia nashauri hawa wakuu wa wilaya na mikoa kama wataendelea kuwepo basi watolewe kofia ya chama waingizwe katika utendaji si kuwa sehemu ya watazamaji na mapumziko ya wastaafu.

Hatuwezi kuwakumbatia hawa MaRC na MaDC wao ndio marais wa maeneo yao. Wafanye kazi sio kuzurura tu
 
Ikiwa wabunge ambao ni watunga sheria wetu wanaweza kuhongwa wanaweka picha gani kwa madiwani wetu wa hizi halmashauri. tunahitaji kanini na sheria zipiotiwe kuona jinsi ya kuwąjibisha ili iwemfano.
 
James Mbatia ame-echo mawazo yangu, tunapoteza muda kujadili ufisadi badala ya kutumia muda huo kuweka mipango ya maendeleo, hii ni kwa sababu ufisadi umeongezeka nchini!
 
Yahya, Star Tv

Tukubaliane kwamba kasi ya kuwajibishana tunayoishuhudia ni uthibitisho kwamba kama taifa tunakabiliana na wakati mgumu kupambana na makundi ya watu wachafu amabao tumewakabidhi dhamana na mamlaka ya kutuongoza. Mimi niwapongeze wale wote walioamua kwa dhati kabisa kuwawajibisha viongozi wa namna hii.

Wananchi tunapata shida ya maji hatuna dawa hospitalini walimu wadai madai makubwa sana na muda mrefu barabara mbovu nk...huku watu wachache wakitafuna mali za wananchi bila huruma...

Nikubalinae na Mh. Diwani Adam Chagulani kwamba Sisi na vyama vyetu tutapita lakini nchi itabaki... Tuungane pamoja kuchukua hatua dhidi ya viongozi wasiowaadilifu na wahujumu nchi...tusipofanya hivi tutahukumiwa na vizazi vijavyo
 
Ikiwa wabunge ambao ni watunga sheria wetu wanaweza kuhongwa wanaweka picha gani kwa madiwani wetu wa hizi halmashauri. tunahitaji kanini na sheria zipiotiwe kuona jinsi ya kuwąjibisha ili iwemfano.

Kurunzi, tuna tatizo la msingi. UADILIFU! na hii ni kuanzia juu kabisa hadi chini kabisa, hakuna sehemu palipo salama, si ulisikia pesa za safari za rais zilipigwa?

 
Tatizo kubwa ni ukumbatiaji, mtu anakamatwa kwa ubadhilifu wa fedha anahamishiwa wilaya nyingine anaendeleza mchezo huo huo. Tatizo ni urafiki katika kazi, wangekua wanawajibishwa haya mambo yasingekuwepo.

Baadhi ya wilaya madiwani hawaonekani, wapo kama hawapo pesa zinaishia kuchakachuliwa na wakurugenzi, tena hata hawa maafisa elimu wanapaswa kuchunguzwa. Ni watu wachache wenye uzalendo na hii nchi.
 
Nampongeza diwani wa Igoma Adam kwa msimamo wake wa kupambana na ufisadi katika halmashari ya Jiji la Mwanza, sijui kwa nini mbunge wa Nyamagana Wenje alikuwa anamtetea Meya wa Jiji la Mwanza.
 
Ahsanteni Wakuu kwa michango na mawazo yenu; Yale ambayo hatukuyasoma bado yanabaki hapa kwa reference ya mawazo mema ya kimaendeleo.

Ahsanteni na JUMAPILI njema.
 
NAFIKIRI PIA ITAKUWA VEMA TUKIRI KUWA KUONGEZEKA KWA KAZI ZA ASASI ZA KIRAIA NA Wanaharakati kumesaidia sana kuibua na kuchagiza mabadiriko. Taarifa nyingi za utafiti, uchambuzi na uwazi zimeweka mambo mengi bayana.

Wa pili kujali ni vyama vya upinzani vimetoa nafasi kwa viongozi wenye uwezo wa kuhoji na kutoogopa.
 
Back
Top Bottom