StarTV Live: Uwajibishwaji Viongozi wa Halmashauri nchini

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,263
9,883
Studio Yahya Mohamed.

Halmashauri kadhaa hapa nchini zimekuwa imegubikwa na ubadhirifu mkubwa. Nini maoni yako?

Karibuni kwa mjadala.

Maoni toka Facebook & Twitter pages:

@mrishosalma Viongozi walio kwenye Halmashauri hawana uzalendo wala uadilifu ni ubinafsi tuu umewajaa 'wajirekebishe'na wawe wawajibikaji
Mlawa Zahir bado hakuna uwajibishwaji watu wanaiba wanahamishiwa wilaya nyingine na huko wanaendeleza mchezo uleule hawa wanamtandao mkubwa ndio maana wanalindana,wabadhirifu waondoshwe kazini na wapelekwe mahakamani serikali itunge sheria ya kuwabana hao watu bika hivyo hakuna kitu
Simon Mwangoka Mwasile Madiwani wa mwanza wamethubutu, wabunge kwao ni ngumu kwa vile wao kwao zaidi itikadi za vyama mbele na si taifa! Ndiyo maana utasikia katibu wa wabunge wa ccm Jenista anaitisha caucus ya ccm kwenda kuwatishia wabunge wa ukweli kama Filikunjombe, Lugola.
Peter J Mwita Kafulisha alishasema,'nchi hii imebakwa',hapa cha msingi serikali iweze kuwa na maamuzi magumu kama ya kuwachukulia hatua kali viongozi wasio wajibika,mfano kifungo jela au kufilisiwa mali zao iwe mfano kwa wengine ila hii mambo ya kubebana haifai wenzetu china ukikamatwa unapokea au kuchukua rushwa unanyongwa kwa nini tusiige huu mfano!
Isaya R Mahujilo Tatizo ni hizi 10% while raia ndo wanataseka after madudu kufanyika harimasharini,kuwajibishwa kwake eti anajihuzuru tu bhaasi na chinichi wanaendelea kupeana michongo
 
Studio Mwanza yupo Yahya.

Wageni Mwanza
Mr Boniface, kada wa CCM na mtendaji wa Halmashauri ya Bunda
Chafuka Adam - diwani Igoma CDM

Wageni Dodoma
Mh.Mbatia
Mh.Luhaga Mpina
Mh.Magale john Shibuda

Karibuni
 
Hiyo ni nguvu ya UMMA kwani CDM hakuna kubebana na huyo KOTECHA acha atoke mbona bungeni CDM wanatoka na haiwi kitu, kakimbia kugombea kwake kirumba kaenda Nyamagana kumwaga hivyo vipesa vyake, nenda Kirumba uanguke.
 
Kwanza napenda kupongeza msimamo wa madiwani wa kata za Mwanza kwa kuonyesha msimamo thabiti katika kutetea maslahi ya jamii. Hili lisiishie Mwanza tu, Halmashauri nyingi nchini madiwani ni kama wapo katika usingizi mzito na wengi hawajui wajibu wao. Waamke sasa nao waingie katika mapambano ya kuhakikisha viongozi wazembe wote wanawajibishwa.

Wananchi wa kawaida pia tuamke sasa na kuwashitua viongozi wetu hawa tuliowaweka madarakani kwa gharama kubwa ili kuhakikisha wanasimamia fedha za umma, na miradi ya jamii ipasavyo..

AMANI IDUMU.
 
Hii inatokana na kulindana kwa viongozi kuanzia juu hadi chini.

Mara nyingi office ya CAG inatoa report juu ya ubadhirifu but siyo zote zinafanyiwa kazi.

Halmashauri zetu pia zinafanya kazi katika mazingira magumu kwani nyingi zinafanya kazi manually, hata kama kuna accounting system mfano epicor muda mwingne inakuwa underutilized, wafanyakazi wengi wanakuwa hawajui kuitumia.

Pia Halmaushauri zinatakiwa ziwe na pre-audit section ili ziweze ku-control matumizi.
 
Ukomavu finyu wa demokrasia hapa Tanzania, ni tatizo.

Kimsingi inapotokea halmashauri inaongozwa na upinzani tofauti na chama tawala kwa hapa Tanzania, basi halmashauri hiyo itafisidiwa kwa vyovyote vile, na upande wa utawala.

Hivi hushangai jiji kubwa la Mwanza pale Pamba Rd opposite Pamba police post, katikati ya Jamhuri petrol Station, na Moil kuna ukarabati wa barabara sasa una miezi takriban 7 njia haipitiki! Hadi hivi sasa haijulikani patapona lini!
 
H/M kwa kweli zinatafuna fedha nyingi, hii ni kwa sababu uwajibikaji wa watumishi wa umma uko chini na pia wale ambao wamefanya ufisadi hawachukuliwi hatua kali za kisheria badala yake wanahamishwa vituo. Kingine ni wataalamu wanadanganywa na wanasiasa hvo haswa madiwani ambao wengi wao elimu zao ni za mashaka. Kwa hali hii miradi mingi haifikii viwango kwa kulingana na fedha inayotolewa.
 
Kinachotokea kwenye halmashauri ni sawa na kinachotokea bungeni, hakuna tena mijadala ya maendeleo, mijadala yote sasa inahusu nani mwizi na nani sio mwizi.

Anne makinda kavunja kamati ya nishati na madini, kuna wabunge wanashutumiwa kupokea rushwa, ili wawalinde baadhi ya mafisadi! tunaelekea wapi?

Viongozi wengi siku hizi sio waaminifu, kupata kiongozi muadilifu imekua ngumu kama kupata dhahabu baharini au kupata samaki jangwani.
 
Madiwani wanatakiwa kuzinduka na kusimamia miradi katika Halmashauri zao maana huko ndiko kwenye ubadhirifu mkubwa
 
Mimi naona ni vyema utamaduni wa kulindana umalizwe na kama mtu hataki kuwajibika mwenyewe awajibishwe bila kujali itikadi utakuwa mwanzo wa kujenga taifa letu kwa kuwa kwa sasa watu wakipewa tu madaraka wanayageuza kuwa mali yao.
 
Kimsingi haya yote ya uwajibishaji wa viongozi wa Halmashauri nchini unatokana na mambo makubwa mawili yanayopelekea ubadhilifu wa mali ya umma.

Moja ni kwamba viongozi ambao ni wawakilishi wa wananchi kwenye ngazi mbalimbali kama diwani,mbunge na Rais mfumo wao wa kuwapata ni wa kimashaka unaogubikwa na Rushwa.

Viongozi wengi ambao ni wazuri nimaskini wa kipato, hawana pesa, hawana uwezo wa kugharimia kampeni zao, kampeni ni gharama.

Wajanja ambao ni wafanyabiashara wanapogundua uzuri wa mgombea, huwa wanamfadhili mgombea kisiri siri kwa maslahi yao. Matokeo yake kiongozi anapochaguliwa hawezi kujitenga na waliomgharamia gharama zote za uchaguzi, matokeo yake ni ufisadi kwenye utangazaji wa tenda.

Rushwa na ubadhilifu havitaisha endapo tutaendelea kuacha viongozi wetu wafadhiliwe na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya.

Ni lazima tuamue fedha za mgombea zitatoka wapi na ni nani azitoe.
 
Mtangazaji,

Hali inaendelea kwenye halmashauri kwa sasa ni ukomavu wa demokrasia na tunatakiwa tuwaunge mkono na siyo kulalamika. Haijalishi mtuhumiwa ni wa chama gani maana kwenye vyama siyo mbinguni.

Wengi wenye madaraka katika vyama wanaharibu sifa za vya kwa kuweka maslahi yao binafsi mbele. Hii haivumiliki na haitavulika. Na itikadi za chama haziwezi kuwa machela ya kuwahifadhi wahalifu.
 
Huu ni ukweli usiyofichika kuwa h/mashauri nyingi nchini zina uozo uliokithiri.

Madiwani mmepewa rungu husimamia mapato na matumizi katika h/mashauri zetu. Tumieni nafasi hiyo kuwawajibisha wale wote wanaofanya ubadhirifu unaorudisha nyuma maendeleo ya mtanzania.
 
Halmashauri nyingi sana kuna kutokuwajibika kwa viongozi wetu tuliowapa ridhaa ya kuongoza ila kilichopo ni kubebana na kulindana na hili ni kwanzia ngazi ya chini mpaka ngazi ya juu. Hili kwa watawala naona kama vile sijui ni sera...?
 
Bila upinzani Tanzania tungekwisha... Uwepo wao ndio umetuamsha, watanzania amkeni Jamani!
 
Back
Top Bottom