startimes wananiboa.

sabufa

Member
Joined
Apr 21, 2013
Posts
26
Reaction score
4
Startimes wananiboa sana.Nilinunua kisimbuzi chao januari 2012 na nilitumia antena ya ndani tu nikawa napata matangazo vizuri.Lakini kuanzia februari mwaka huu,picha zinaganda.Nimenunua antena ya nje lakini picha zina zinaganda na nimejaribu kuinua antena juu signal inaishia 41 tu.Hivi TING wameishaingia mkoa wa Mbeya?.Mimi niko Chunya.
 
Hawa mimi nlichopanga ni kwenda kuwaachia kingamuzi chao pale na kuondoka...
 
Poleni. Sisi wenzenu huku digtek DTV na UBC hatuioni kabisa tunaona giza hata fainali ya UEFA hatukuona. Sijui wenzetu huko ZUKU na AGAPE mnaendeleaje?
 
Wakuu kama mtu ulijipinda kununua Tv hata kwa laki na nusu jipinde tena 250,000 upate dish lako ili ufaidie FTA bureeeee! Hawa wote wezi tu!
 
poleni sana....najua wengi wanaweza kusema mimi napromote startimes...lakini si kweli.....nina zaidi ya mwaka natumia startime....nina antena ya nje nzuri sana....kwa kweli sijawahi kupata tatizo lolote la signal kasoro mara chache ambazo kuna chaneli za nje zinapotea kabisa na wenyewe startimes wanaweka tangazo na apology....ushauri wangu kwa watu wote wenye startimes decoder,nunueni antena nzuri sio za kuungaunga then tafuta fundi wa kuinstall antena(wapo wengi tu uswazi) mimi walinifungia kwa tsh 10,000 tu....na hadi leo haikwami wala nini iko very clear....kuna chaneli zingine wenyewe ndio wanaquality mbovu startime ni msambazaji hawezi kuongeza quality ya chaneli fulani fulani haswa za kitanzania....kwa kweli kwa ving'amuzi hamna kinachofikia startimes(DSTV is another league,usiiweke hapa)
startimes wana chaneli nzuri sana kwa mfano
news:bbc,aljazeera,msnbc,cctv
sports:mcs(french tv),setanta,eurosport
entertainment:bet,mtv,E!entertaiment,fashion tv,Etv(south africa),Estar,Fox,FX,stv music,stargold,discovery science,nation geographic gold etc
local:tbci,2...chaneli 10,dtv,star tv,itv,eatv,clouds tv

mnyonge mnyongeni haki yake mpeni....ukiondoa DSTV hakuna king'amuzi kingine chenye package nzuri zaidi ya STARTIME....kama kipo orodhesheni chaneli hapa tuzichambue

kids:nicklelodeon,kidsco
 
Msema kweli mpenzi wa Mungu yaani hakika nilijuta kununua king' amuzi cha startimes na nimekinunua mwezi february mwaka huu kimebaki kama pambo tu sitaki hata kukiwasha kinanichefua mno!
 
Hamia DSTV acha ubakhili...Simu mchina, Tv mchina na kinag'amuzi unanunua cha mchina??
 
Dstv mpango mzima....startimes matapeli.....wezi tu
 
naomba kujua dstv kama locol tv zote zipo kweli mchina noma du
 

Mkuu unaiwazia TING? Ili utazame channel gan? Mimi nina Ting najuta kutoa elfu tisini zangu
 
uko chunya maeneo gani SABUSA? chokaa,kibaoni,sinjilili,uzunguni,madukani,sinza,chunya mjini,kiwanja,mbugani,mlimanjiwa,makona,ifumbo au mkwajuni? nitajie uliko nitakushauri la kufanya. valamushe voonti uho!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…