Startimes na wizi wa waziwazi

Startimes na wizi wa waziwazi

kat.ph

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2013
Posts
2,221
Reaction score
1,679
Habari wanabodi...

Kampuni ya startimes kupitia ving'amuzi vyake sasa inafanya wizi wa waziwazi kwa wateja wake;

1. Channel zinazitakiwa kuonekana bure (local channels) hazionyeshi, na ukiwasiliana nao wanakwambia uende ofisini kwao na 12,000 (wengine wameambiwa 5500) ili wakupe kadi mpya upate local channels bure (bure?!!)

2. Ving'amuzi sasa vinasumbua kwa baadhi ya watu... Havikamati kabisa hivyo hakuna channel inayoonekana. Ukipiga simu wanakwambia urekebishe antenna yako, ikishindikana uende na king'amuzi ofisini kwao.

3. Matatizo yanaibuka ukishalipa pesa kwa ajili ya kupata channel/kifurushi

Ukienda ofisini wanakwambia wana fundi wao hapo umpe king'amuzi aangalie... Anaangalia halafu either anakwambia umlipe akitengeneze au anakwambia kimekufa automatic tu.... Wanakwambia utoe pesa ununue kingine..

Matatizo haya yote yameanza baada tu ya serikali kuwalipisha fain na nyie kusema mnaendesha kampuni kwa hasara.... Hii ni coincidence au ndio mnalazimisha watu kununua na kutoa pesa kwa njia hii ya udanganyi ili kurudishia hasara mliyopata???
 
Mwanzoni waliniambia niende na 54,000 wanipe king'amuzi kipya.

Juzi wamebadili gia angani wakanambia niende na 24,000. Yaani 12,000 ya kadi mpya, na 12,000 ya kufunguliwa local channels.

Naendelea kusubiri labda itazidi kushuka bei.
 
Back
Top Bottom