Startimes, hebu kuweni serious kidogo!

Ta Nanka

JF-Expert Member
Oct 8, 2013
1,226
1,902
Mmekuwa na tabia ya kukata matangazo kila ifikapo saa saba usiku. Sifahamu matangazo hurejea alfajiri/asubuhi ya saa ngapi. Sina hakika tatizo lilianza lini lakini mwezi Juni niliuliza nikajibiwa “kuna tatizo kwenye minara linafanyiwa kazi”. Miezi mitatu baadae, bado maelezo ni yale yale, “kuna tatizo kwenye minara linafanyiwa kazi”.

Hivi nyie watu mko serious kweli?

Tatizo gani hilo ambalo haliwezi kutatuliwa kwa miezi mitatu?

Kwanini mnaibia wateja? Mtu akilipia kifurushi cha mwezi (siku 30), amelipia saa 24 x 30. Kwa hizo saa ambazo mnakuwa hampo hewani, kiuhalisia mnakuwa mmemuibia siku angalau 5.

Msijiaminishe kwamba kwa muda huo hakuna wa kuangalia TV. Wako wako kwa majukumu/aina ya maisha muda huo wanakuwa macho na wanaweza kuhitaji kuangalia TV.

Hebu kuweni serious angalau kidogo!!
 
Star times waachieni watu wa Vinginguti na huko Buza kwa Mpalange.
Mtu unakaa Survey unafunga star times? Kwanza utakua unadhalilisha majirani zako na mama mwenye nyumba
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom