Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,307
- 40,941
Kama kichwa kinavyoeleza,leo Tanzania inaweza kuweka historia mpya katika nyanja ya soka iwapo itafanikiwa kushinda mchezo wake dhidi ya Lesotho.
Kipigo walichokipata hapo jana Cape Verde cha 1-0,kinaipa nafasi kubwa Stars kufuzu kwasababu tunahitaji points 3 tu na kufikisha points 8 ambazo hakuna timu itakayoweza kuzifikia maana mwisho wao ni 7.
Katika siku ya historia kama hii nilitegemea wale wenye ruhusa ya kurusha game hii wawe wameandaa big skrini kwenye openi sipesi kama uwanja wa karume au Mnazi mmoja au huko mikoani pale Nyamagana mwanza, sokoine, Namfua,kaitaba,samora na maeneo mengine ya wazi ikiwa ni kama mkakati wa biashara pia,maana shamrashamra zingeanza mapema hata saa saba hivi hadi muda wa mechi.(kazi kwenu watu wa masoko nimewaibia tu idea yangu).Watz wengi leo macho na masikio yapo Lesotho so ni fursa kubwa hii.
Pia kama wapenzi wa soka tujiandae kisaikologia matokeo ya mpira huwa hayatabiriki sana pamoja na timu yetu kuwa na homa za vipindi,leo wanacheza vizuri kesho unajiuliza ni hawa kweli? Ila nina imani kocha Emmanuel Amunike atatuvusha maana tuna mechi mbili mkononi hadi sasa.
MUNGU ibariki Taifa Stars, MUNGU ibariki Tanzania