Star TV should declare their interest

Nashangaa pia,kwanin matangazo ya kumkampenia magufuli wamuweke lowassa na maneno ya Nyerere yanayokosoa mambo mbalimbali?Mwalimu akizungumzia wapumbavu basi wao wanamweka lowassa!Hii si sawa!TCRA kwanini hamuwachukulii hatua hawa?Kama ni tangazo la ccm kwanini wamuweke lowassa?
Mnazidi kutuonesha watanzania kuwa mnatumika!
Star tv inatumika kisiasa,haifai tenaaaa!
 

Mkuu mimi ninacholalamika siyo kuipendelea CCM au la. Nataka waingie ktk dunia ya ustaarabu, wasiwe vuguvugu wawe moto au wawe baridi
 

Nakuunga mkono, kama nilivyosema hapo juu CCM imewahakikishia faini yoyote wako tayari kulipa, kwa maneno mengine pesa inaongea
 
Tatizo ni kwa vyama kama CDM kukosa tv station yake au hata gazeti. Ni aibu kuona Slaa hajaacha chombo cha habari wala jengo la chadema muda wote wa uongozi wake! Unajiuliza mamilioni ya ruzuku yanaenda wapi? Hata miradi ya uwekezaji sidhani kama alibuni dr. Slaa. Apishe akina lowasa waimarishe cdm.
 

Ni wazo lkn sidhani kama chama cha siasa ni vizuri kumiliki chombo kama TV, unaweza ukawa na Tv inayokuunga mkono lkn si kuimiliki moja kwa moja. Mfano nchini Marekani inaeleweka wazi kwamba tv kama fox news wanaunga mkono republicans na MSNBC inaunga mkono Democrat
 
kwani lazima uangalie star TV? unaweza kuangalia miziki EATV au hata bbc, cnn na aljazira.

 

Mkuu ukitakiwa kulitolea ushahidi hili uliloliandika hapa unaweza kufanya hivyo?
 
Kuna clip (TV Ads)imekuwa ikirushwa kwenye TV kadhaa hapa nchi ikimuonyesha Mh Lowasa akikabidhi pesa kwa viongozi wa dini.Tendo hilo la makabidhiano linaambatana na sauti ya mwalimu Nyerere akitahadharisha kuhusu mtu anayetumia pesa kutafuta namna ya kwenda ikulu.

Kwa tafsiri ya kawaida kabisa,clip inataka kuonyesha umma wa watanzania kuwa hizo pesa wanazokabidhiwa hao viongozi wa dini,ndizo zonatumika kununua ikulu,kwamba viongozi wetu wa dini wamenunuliwa na huyu Lowasa.

Me nadhani ni udhalilishaji wa viongozi wa dini na waumini wao.Sitaki kuamini kwa namna maelezo na picha hizo zilivyopotoshwa.Hayo matukio yamefanyika hadharani,huyu bwana amealikwa na hao viongozi wa dini kwa nafasi yake ya uongozi,akachangisha hadharani na kukabidhi hadharani kwa wahusika.Ni wangapi serikalini akiwepo na rais wameshawahi kuendesha harambee hivy?

Viongozi wa dini hilo Tangazo linawadhalilisha sana,waumini na sisi tangazo linatuambia kuwa viongozi wetu wa dini wamenunuliwa,huu ni udhalilishaji.

CCM wamepotoka ktika hili
 
mkuu lile ni tangazo limelipiwa kama yanavyolipwa ya tigo na voda
 
No. Kuna tofauti kubwa. Ni dhana iliyoko ndani yake. Hao wanaunganisha speech ya Nyerere kuhusu rushwa kisha wanamwonesha Lowassa akigawa fedha kana kwamba anatoa rushwa. This is wrong. TCRA wanatakiwa waingilie kati. Haya ndiyo yanakatzwa kwenye cybercrime
 
shida wanaonyesha usivyovipenda tu hakuna kingine. sawa na itv channel 10 ..jf tu ndio non alignment movt NAM
 
TULIEN mafisadi dawa iwaingie mpaka ktk mifupaa hahahaa! ITV vp haiwatosh kurusha hbar zenu...
 
Hapa NEC inahusika kuchukua hatua lakini mara nyingi huchukua hatua baada ya kupokea malalamiko.
Ninachoona hapo ni kwamba UKAWA wamekaa kimya ili waje wfungue kesi baadae ua wameona halina madhara kwao.
Binafsi naona tangazo lina madhara zaidi kwa CCM kuliko kwa UKAWA. KUNA WANANCHI HAWAJUI KAMA LOWASA AMEHAMA CCM NA HIVYO KWA KUWA WANAKIPENDA CCM NA HAWAMJUI MGOMBEA MAGUFULI, WATAMPA KURA EL.
HILI TANGAZO NAONA LIMEBUNIWA NA TEAM LOWASA WALIOPO NDANI YA CCM!
 
Tangazo hilo halifai...ukada uwekwe pembeni.

Dialo hilo tangazo linambeba Lowassa.
 
Umeshawahi kumhoji Mbowe hayo maswali, maana Katibu Mkuu ni mwajiriwa tu?
 
Tanzania vyombo vyetu vya habari(Radio,TV,Magazeti) vinaendeshwa kwa ushabiki wa kisiasa
 
Kituo hiki cha luninga cha Star TV kimejianika kama sehemu ya kampeni na propaganda za chama kimoja ambacho ni CCM. Habari zake,mijadala yake,matangazo yake na hata watangazaji wake wote wapo kiCCM.

Kimsingi,hilo si jambo jema kwa kipindi kama hiki cha uchaguzi. Wananchi tuna haki ya kujua mambo ya vyama tofauti ili tuamue. Kuzungumzia na kupigia debe chama kimoja si sawa.

Binafsi,nimeamua kutotazama tena Star TV na kuwaachia wafuasi wa CCM. Star TV waendelee na kampeni na propaganda zao kadiri watakavyo. Kwaheri Star TV,kwaheri TV ya CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…