Star TV mbona hamumwaliki Kingunge?

Star TV mbona hamumwaliki Kingunge?

Kila mmoja anakumbuka kuwa Dr.Slaa na wengine waliohama CHADEMA mlikuwa mnawaalika kwenye vipindi vyenu kila wiki wakieleza kile kilichosababisha wao kuhama au kuacha siasa.Mbona mzee Kingunge haiwi kama wengine ukizingatia huyu mzee ni nguli ktk siasa na chama chake mwenye kadi namba 8?
kwanini polepole haalikwi itv
 
Ataalikwa kwenye tv ya Rainfred......inatosha.
 
Nani amwalike mganga wa kienyeji kwenye tv yake.hata ingekuwa mimi sikubali
 
Kama wasaidizi wenyewe walikuwa akina kingunge si ajabu nyerere utawala wake ulipata kashikashi kama zile.

Kuna mtu na akili zake sawasawa anaweza kuamini kuwa huyu kingunge ndio alikuwa mmoja wa wasaidizi wa karibu kabisa wa nyerere?

Huyu mzee alikuwa anamfanyia usanii tu nyerere. Hakupikwa akapikika. Si ajabu siku zote alikuwa hana hata ujasiri wa kukemea madudu yaliyo kuwa yanafanyika miaka na miaka kwenye chama chake.

Eti leo ndo ameyaona na ndio anatoka!

Mbona mengine mengi alikuwa anayachekea chekea tu?

Hili limefanyika kwa manufaa ya nchi ndio anajifanya kususa.

umejuaje km alishawahi kuwaonya na kuwaambia lakini wakawa hawasikii? tusimuhukumu mzee wa watu kisa tu kachoka na mambo ya CCM.
 
siasa za ubaguzi na matumizi mabaya ya vyombo vya habari likitokea la kutokea isiwe tabu na wamiliki pia waende kula Hague.
kina chonitisha ni siasa za ukanda zimeamza mapema, sasa tena siyo ccm au cuf au chadema, bali kaskazini, butiku, warioba, mongela, kusaga,ruge, startv na diallo, shigongo, mama mongela , wasira. hii itatumaliza kabisa
 
Kila mmoja anakumbuka kuwa Dr.Slaa na wengine waliohama CHADEMA mlikuwa mnawaalika kwenye vipindi vyenu kila wiki wakieleza kile kilichosababisha wao kuhama au kuacha siasa.

Mbona mzee Kingunge haiwi kama wengine ukizingatia huyu mzee ni nguli ktk siasa na chama chake mwenye kadi namba 8?

Hata itv hawawaaliki akina polepole sijui kwa nini yaani!
 
Du mna myoyo kweli bado mnaangaliaga star tv.
 
Star tv haina tena mvuto ..ndio maana ina station na vipindi visivyoeleweka
 
Toka atoke yule mzee wa anga za Kimataifa siwafatilii tena..maana ni vipindi vya ngonjela tuu sasa.
 
Mbona ITV hawamwaliki Polepole?

ITV ni UKAWA

STAR TV ni CCM
 
Mkuu ukweli no kwamba hawawezi kumwalika, mmiliki wa TV anamuunga mkono magufuri ndio maana wanajaribu kutumia fursa yoyote inayojaribu kuonesha udhaifu wa mgombea wa UKAWA. Tanzania ni nchi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki ambayo licha ya kufahamu ukweli Kuwa vyama vya upinzani bado vichanga nguvu nyingi imekuwa ikitumika kuvikandamiza kwa kupotosha mantiki ya uwepo wake. Mi nashangaa kivipi hivi vyama vinakuwa tishio kwa chama kilichopo madarakani miaka zaidi ya 50 mpaka baadhi ya watu kufikia kuandaa mipango ya hila dhidi yao, je wanaoandaa mipango hiyo hawatambui mchango wa vyama vya upinzani duniani kote? Na kulikuwa na haja gani ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi kama tulikuwa bado hajutaelewa maana halisi ya msingi wake. Inashangaza kuona baadhi ya viongozi wa dini wanahusisha vyama vya upinzani na vurugu na hii inaonesha kwa nchi kama Tanzania dhana ya upinzani kueleweka bado tunasafari ndefu maana kuna watu kutokana na maslahi binafsi wanaviona ni kikwazo kwa maendeleo yao na wanatumia huu mtizamo hasi kuwa aminisha na wengine.

Mkuu hasante sana kwa comment nzuri. (natumia simu)
 
Nimeacha muda mrefu kuangalia hiyo kitu,hata ving'anuzi vyao sio vya kununua!
 
Back
Top Bottom