Star tv - dangerous love (movie)

Technician

JF-Expert Member
Mar 30, 2010
841
222
.........UPDATES..........
Hatimaye Rado anauwawa na Prosephina,Aireen nae anatupwa toka juu ya
gorofa na kufariki,anabaki Hommer na Prosephina.
Prosephina anafanikiwa kumpata mama yake mzazi.maisha yanaendelea.

............................THE END..............................
STAR TV

DANGEROUS LOVE-MOVIE

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa movie kali inayokwenda kwa jina

la "DANGEROUS LOVE",Ama kweli kuna picha ambazo unaweza kuziona

ukadhani hazikutungwa hapa duniani na binadamu wenzetu,ukweli

ni picha ambayo imenifanya kuwahi nyumbani ili tu nipate muda

mzuri wa ku-watch mpaka nione mwisho wake.

Kuna mastaa kama watatu lakini kiongozi wao anaonekana zaidi

ni Mr Hommer,kijana mtanashati,mwenye mapenzi ya kweli kwa

Prosephina mwanamke ambaye alikuwa chaguo la Mr Rado kijana

tajiri aliyetokea kumpenda sana Prosephina kiasi cha kutumia muda

wake mwingi sana kumlinda asitoroke kwenye nyumba alimohifadhiwa.

Lakini hata hivyo anamwajiri mtu aliyejifanya mfanyabiashara kwake kazi

ya kumlinda Prosephina kutahamaki kaajiri mpenzi wake na mpango unasukwa wa

kutoroka makazi yao na hatimaye wanakuwa wote mipango ya kufunga harusi inafanyika

lakini harusi yenyewe inaingia utata baada ya msichana aliyekuwa kipenzi cha Mr Hommer

aitwaye Aireen akituma majambazi kuteka gari la bibi harusi na kumshikilia ndani ya jengo

lisilojulikana na hatimaye harusi kuvunjika.

Leo ni wmendelezo wa picha yenyewe ukitaka usikose kuangalia STAR TV jioni saa 3.00 usiku

baada tuu ya vichekesho vya uwanjani.

Nawashukuru STAR TV kwa kurusha Movie kali hewani ambayo imenifanya niwahi kurudi

nyumbani na kukuta watoto wakinisubiri kuangalia picha.
 
Hizo nizo kazi za vichwa. Ila mie nawapa salute mtunzi na waongozaji wa La Revancha ( The Revange). All most all characters are serious concerned with the title. Nice choice of characters, they worked hardly. Nice location. You don't have to be busy with main characters only, other charaters have their stories too. Many life diversity have been explained here, love, fight, family, friendship, betrayal, loyalt, discrepancy, secrets, richness and poverty. Their explanation are in many ways and unique. As a work of art, it is real incredible to have so many different stories and relate them to one story of revange. I love it.
 
STAR TV

DANGEROUS LOVE-MOVIE

Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa movie kali inayokwenda kwa jina

la "DANGEROUS LOVE",Ama kweli kuna picha ambazo unaweza kuziona

ukadhani hazikutungwa hapa duniani na binadamu wenzetu,ukweli

ni picha ambayo imenifanya kuwahi nyumbani ili tu nipate muda

mzuri wa ku-watch mpaka nione mwisho wake.

Nawashukuru STAR TV kwa kurusha Movie kali hewani ambayo imenifanya niwahi kurudi

nyumbani na kukuta watoto wakinisubiri kuangalia picha
.


Asante kwa kutujuza habari za uwepo wa movie nzuri, ila nakupa ushauri wa bure, hapo kwenye red si vzr kuangalia movie za mapenzi na watoto, mnawakomaza mapema, halafu kesho keshokutwa mnarudi kuomba ushauri watoto wenu sijui wamefanya vituko gani na watoto wa jirani!

Otherwise, thank you for briefing us.

HP
 
Me napenda sana hii tamthilia hasahasa madam madel cjuw,maid wa prosfna,..na kamdomo ka mama homer,teh teh
pia napenda UNTAMED BEAUTIES ya chanel ten,cjuw berenice atakufaje na roho yake!lol
WOMAN OF STEEL,ya itv,imeniuma valentina alivoachwa kwenye mataa,cku ya ndoa,.bt nlifurah pia wicked cousn wa Valentina alivoumbuka airport,hahah
CURSE BY THE SEA ya Capital tv,..Mario Cimaro(Victor Manuel)he is my fav! Tamthilia ni maigizo yanayoonesha uhalisia wa maisha!
 
Asante kwa kutujuza habari za uwepo wa movie nzuri, ila nakupa ushauri wa bure, hapo kwenye red si vzr kuangalia movie za mapenzi na watoto, mnawakomaza mapema, halafu kesho keshokutwa mnarudi kuomba ushauri watoto wenu sijui wamefanya vituko gani na watoto wa jirani!

Otherwise, thank you for briefing us.

HP

Hii movie inafundisha mambo mengi sana
na sio mapenzi kwa mvulana na msichana tuu
bali pia kwa mzazi,unamuona mama Hommer jinsi
anavyowajali watoto wake?
Pia inafundisha kutokataa tamaa,unamuona Hommer
pamoja na mateso yote hakumuacha mpenzi wake
Prosephina.Hata hivyo unamuona Hommer jinsi anavyowapenda
wadogo zake?na kuwapa matumaini na ujasiri wa kutokata tamaa
nataka na watoto wangu wawe kama Hommer,na mama yao awe
kama mama yake Hommer.Watajifunza mazuri na si umalaya usio
na mbele wala nyuma.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom