Nawashukuru Star Times kwa kujibu hoja yangu kuhusu ufanisi wa kisimbuzi chao ya tarehe 21 Februari 2014. Hii ni ishara ya uwajibikaji kwa umma. Kwa maelezo yao, channels za bure hazionekani vizuri kutokana na kukosa ushirikiano toka kwa wenye stesheni za TV husika yaani ITV, EATV, TBC, Star Tv na Channel Ten. Nawashauri Star Times wawasiliane na TCRA ili wawalazimishe wahusika kutoa ushirikiano kwani suala la kuonyesha stesheni za bure ni la KISHERIA na siyo HIARI. Sheria na Kanuni za mawasiliano ya Kielektroniki ziko wazi juu ya suala hili. Wasiingize maslahi binafsi katika suala hili ili kulazimisha watu kununua visimbuzi vyao. TCRA waingilie kati kwani ndio wasimamizi wakuu wa suala hili.