Heshima yenu wakuu. Kwa wiki sasa sipati matangazo ya tv baada ya dishi langu kupoteza chaneli. Sasa nina mpango wa kununua king'amuzi, lakini kabla ya kuingia huko naombeni ushauri kwa mnaotumia ving'amuzi. Kipi ni bora kati ya star times na hawa jamaa wa zuku?
Currently I am using Star times i have not face any problem with them so far! but i prefer Zuku over Star time henceforth take Zuku ndugu! cause quality of picture ktk Zuku zina overide Star times. plus more local channel and international channel ktk Zuku!
Zuku nao wana matatizo kuna wakala wao kampumi tanzu ya Bw Mufuruki ukipiga simu zao walizoweka kwenye mtandao moja inaenda kwa mdada ,huyo mdada anasema imekuwa kero kwake kwani anapigiwa simu mara kwa mara na wateja kwenye namba ambayo hyo wakala kaiweka kwenye mtandao,na namba ingine ukipiga haipokelewi bali unasikia nyimbo tu,kuna kingine kinakera kuhusu hao mafundi wao ,panapo majaliwa nitaweka jamvini tabia za baadhi ya mafundi wao.kwa channel na muonekano Zuku wapo mbele sana ,Startimes wameachwa mbali sana kwa kila kitu.Kifupi ST ni cha mtoto kwa ZUKU
Swali lamsingi nikwamba local chanel zipi zinapatikana Zuku na Zipi St?
local channels zote zinapatikana kwenye zuku.
So far ni TBC1. ITV bado wanatia ngumu. lakini I hope soon cut-off date ya Digital Migration itawalazimisha.
Tafuta Mesh Dish la Free to Air utapata Channels zote Local. Ukipata Technician mzuri anaweza akakuwekea BUC tatu na ukapata channels nyingi sana Local na za nje.
Kwa hiyo ZUKU ni bora kuliko Star Times??Zuku nao wana matatizo kuna wakala wao kampumi tanzu ya Bw Mufuruki ukipiga simu zao walizoweka kwenye mtandao moja inaenda kwa mdada ,huyo mdada anasema imekuwa kero kwake kwani anapigiwa simu mara kwa mara na wateja kwenye namba ambayo hyo wakala kaiweka kwenye mtandao,na namba ingine ukipiga haipokelewi bali unasikia nyimbo tu,kuna kingine kinakera kuhusu hao mafundi wao ,panapo majaliwa nitaweka jamvini tabia za baadhi ya mafundi wao.kwa channel na muonekano Zuku wapo mbele sana ,Startimes wameachwa mbali sana kwa kila kitu.Kifupi ST ni cha mtoto kwa ZUKU
Hiyo ni kweli tutakuwa na ving'amuzi kibao lakini havina local channels.tcra inabid waje na ideas mpya, kwa sasa watumiaji wa hivi ving‘amuz tunapata shida sana. wangekuja na kanuni inayowalazimisha warushe local channels zote, kwa channels za nje ndo wawe na ushindani, vinginevyo watu tutakua na vingamuzi vyote ili tu kupata chanels nyingi za hapa kwetu
Lengo ni kuwa watu waachane na hayo madish, ishu ni kuwa hivi ving'amuzi vipatikane hadi huko vijijini. Suala la muhimu ni kuwa chanels zote za ndani zionekane.Habari za leo.
Mimi nawashangaa naona kama serikali inafanya biashara kupitia ving'amuzi, sasa mtu uwe na startime, Ting, zuku Dstv itawezekanaje?? 1.nadhani wangeamua kuchagua kampuni moja ambayo itaweza kurusha channels zote kwenye king'amuzi ....alafu ishushe sana kodi maana sina uhakika kama kila mtanzania ataweza kununua ving'amuzi.
2.Itakuwaje kwa watanzania na wengineo ambao walikuwa wanategemea masafa kwa njia ya satellite dish??me nadhani channels zote ambazo zinawekwa kwenye vingamuzi ziwekwe pia kwenye dish kwa wale wanaotumia dish huko maporini.
Habari za leo.
Mimi nawashangaa naona kama serikali inafanya biashara kupitia ving'amuzi, sasa mtu uwe na startime, Ting, zuku Dstv itawezekanaje?? 1.nadhani wangeamua kuchagua kampuni moja ambayo itaweza kurusha channels zote kwenye king'amuzi ....alafu ishushe sana kodi maana sina uhakika kama kila mtanzania ataweza kununua ving'amuzi.
2.Itakuwaje kwa watanzania na wengineo ambao walikuwa wanategemea masafa kwa njia ya satellite dish??me nadhani channels zote ambazo zinawekwa kwenye vingamuzi ziwekwe pia kwenye dish kwa wale wanaotumia dish huko maporini.
Jamani mbona mimi niliweka zuku na nimeitoa?nimeona haina tija kwangu kulipa 40,000 kwa mwezi kuangalia news tuu hakuna mpira. Nimeamua kuweka easy tv, angalau ni cheap na unaona chanel za news na local kama star, itv,tbc, capital,eastv.