Mambo ya soko huria kaka kama huwezi kulipia hizo gharama si uache,msiwalaumu bure Star Times mbona Dstv wanabei za kufa mtu na hakuna anayewalaumu?kwanza StarTimes walitoa vipeperushi longtime kuwa kuanzia october 1 kutakuwa na kifurushi kingine kinachoitwa UHURU kitakuwa na channel zaidi ya 46 na kitalipiwa sh 18,000.pia mimi nawapongeza StarTimes wamewezesha wengi kuziona channels ambazo tulio mabonde kwinama tulikuwa hatuoni,sasa tunaona live bila chenga.Nimesoma malalamiko mengi kuwa ST king'amuzi chao hakionekani vizuri kwa mimi hilo nalipinga huenda watu wanakosei setting,inabidi uwe na antenna yenye booster na ambayo iko juu ya paa ikiwa juu kiasi,ukifanya hivyo utaona bila tatizo.kule kukwama kwama ni hali ya ambayo inatokea na inabidi ucheze na kurekebisha antenna,hata Dstv inakwama,penye ukweli tuseme ukweli ,wa TZ tunapenda sana kulalamika bila kufanya utafiti au kutafuta ufumbuzi