Star Bunge Kuonyesha Bunge Live?

Heart Wood.

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
972
1,150
Wadau,
Amani iwe kwenu, nimeona tangazo kupitia Television ya StarTv kuwa, kupitia king'amuzi cha Continental,Bunge litakuwa Live.Mwenye taarifa za uhakika na kuweza kuthibitisha jambo hili Tafadhali sana atujulishe.

Katika mambo yaliyowagusa na kusononesha mioyo ya watu katika kipindi hiki ni kukosekana kwa Bunge Live.Laiti kama viongozi wangelijua namna wananchi tulivyosononeshwa kwa kukosa Bunge live,hakika wangelirudisha matangazo haya muhimu kwetu mara moja ambayo ni haki yetu ya msingi kwa mujibu wa katiba, kufahamu nini wawakilishi wetu wanakifanya iwapo ni kile tulichowatuma kweli au wameenda tu kusinzia na kuvuta posho.

Tupo tayari kununua ving'amuzi vya continental kwa gharama yoyote iwapo itathibitika kuwa ni kweli.Eee Mungu fanikisha Bunge hili liwe Live kwa namna yoyote ile.AMINA.
 
Back
Top Bottom