TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,562
Wakati wa kampeni zako za urais uliahidi kwamba serikali yako itawapigania wanyonge, kwamba utakula sahani moja na vigogo walizowea kuhujumu taifa na kuwanyanyasa wanyonge, kwamba serikali yako itawafanya wanyonge waishi kwa raha ndani ya nchi yao. Na hata wakati wa kutoa hotuba ya kufungua bunge ulisisitiza kuhusu hilo.
Cha kushangaza vigogo ulioapa kuwashughulikia ambao walimelifikisha taifa hapa lilipo kwa matendo yao ya ufisadi bado wanakula raha tu,wengine wamepewa hadi nyadhifa kubwa Kubwa ndani ya bunge letu tukufu.
Wanaoshughulikiwa ni wanyonge tu, wamevunjiwa nyumba zao kwa hoja kwamba wamejenga ktk maeneo hatarishi,wala utawala wako hukufikiria mara mbili wakati wa kuwashughulikia,wakati huo huo waliohujumu taifa kwa ufisadi na hata kulisababishia taifa hasara ya kudaiwa deni la zaidi ya trilioni 30 wala hawaguswi.
Kuna hawa ambao kwa makusudi walikwepa kulipa kodi,wamechunguzwa na wamekutwa na kosa la kutolipa kodi,cha kushangaza eti serikali yako inawabembeleza kulipa kodi,mmewapa miezi 3 ya kulipa kodi,mbona wale wenzangu na mimi hawakubembelezwa hivyo kwa kuongezewa muda wa kujiandaa kuvunja nyumba zao? Walishughulikiwa haraka.
Sasa kuna hili la kuzuwia TBC kurusha kipindi cha bunge live wakati wote,hii si sawa na huwatendei haki wanyonge ulioapa kuwapigania. Wakati mnapitisha uamuzi huu, ni Azam TV na Continental pekee ndio wanaorusha live bunge, kuweza kuangalia bunge kupitia Azam inabidi ulipie king'amuzi 12,000 kila mwezi,sisi maskini hatuwezi kumudu hizo gharama, tulikuwa tukitegemea ving'amuzi vya IPP Media ambapo TBC ilikuwa ikipatikana huko,tena ni bure, tulikuwa hatulipii kwa mwezi.
Sisi wanyonge tulipenda sana kufuatilia mijadala ya bunge ili kuona ikiwa wabunge wetu tuliowachagua majimboni kwetu wanazungumza yale tuliyowaagiza, sasa mnatunyima hii haki ya kupata taarifa kwaajili ya maslahi ya nani?
Mnatunyima haki yetu ya kupata taarifa ili iweje? Mheshimiwa usipokuwa makini swala dogo kama hili litaharibu mema yote uliyoanza kuyafanya mpaka sasa,unawajua Watz walivyo wasahaulifu, na unajua kwamba una maadui wengi wa kisiasa si ndiyo? Wanaweza kulitumia hili swala dhidi yako and to be honest, this is very sensitive issue, you have to handle it very carefully or else will lead to your political downfall faster than you could imagine.
Yangu ni hayo kwa leo.