Stanslaus Nyongo Ataka Majadiliano ya Tija Dira 2050

Stanslaus Nyongo Ataka Majadiliano ya Tija Dira 2050

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
3,119
Reaction score
1,430

STANSLAUS NYONGO ATAKA MAJADILIANO YA TIJA DIRA 2050​

NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Haroon Nyongo amekumbusha umuhimu wa majadiliano ya pamoja badala ya ukosoaji ili kujenga uelewa wa pamoja utakaofanikisha upatikanaji wa Dira 2050 itakayotokana na maoni ya wananchi na wadau.

Nyonogo amesema hayo katika Mkutano wa Asasi za Kiraia uliojadili mapitio ya Rasimu ya Kwanza ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 uliofanyika Dar es Salaam.

Amesema wakati akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za maendeleo ya Jamii alikutana mara kwa mara na asasi hizo za kiraia, akisema usipoelewa dhamira yao ya kukumbusha baadhi ya mambo, huenda ukafikiri kuwa wanaikosoa serikali kila wakati jambo ambalo sio la kweli.

Ameeleza kuwa kama Serikali wamejiandaa vya kutosha kusikiliza kila maoni ya Wadau na Wananchi, akisema jambo hilo ni muhimu zaidi ili kuhakikisha kuwa Dira 2050 inakuwa halisi na inayotokana na maoni ya wananchi.
 

Attachments

  • Screenshot 2025-01-11 at 17-50-42 Instagram.png
    Screenshot 2025-01-11 at 17-50-42 Instagram.png
    714.4 KB · Views: 23
Back
Top Bottom