Stand ya Bus mkoa wa Mara-Bweri inatia Aibu

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
44cf1bfbdb47b49ffbd10953790ac50a.jpg
9504d1f0a82e9c1bd4dc350bc1b496cd.jpg
3abeff3abab3826be118bafeac10ef7a.jpg

Hizi ni baadhi ya picha nilizopiga mida hii hapa stand ya mabus ya mkoa wa Mara maarufu kama Bweri
Hivi mbona mkoa huu na wilaya hii ya Musoma ambako ni nyumbani Kwa Baba wa Taifa kumesahaulika kiasi hiki!??
Barabara nyingi za Musoma mjini ni vumbi tupu,uwanja wa ndege vumbi tupu,stand ya mabus nayo madimbwi kibao kama muonavyo pichani
Manispaa ya Musoma naona wameisahu hii stand yani ni aibu tupu
 
Kusema kweli Tanzania ni Darasalamaa tuu huko kwingine ukienda nikama umehama Nchi vile
Hata ustaarabu wa watu wa mikoani huwa siuwezi hasa huko Kanda ya ziwa yani wapo hovyo hovyo tu...mtu kukurushia ngumi au kukutukana ni jambo la kawaida sana.
 
Nilikuwa musoma mwaka 2010 iko hivyo ina maana hawajaiendeleza kweli??????!!!!!!!
 
Stand za kiwango ni ya Morogoro pale Msamvu,Ya Singida ile inayojengwa pale na Ya Moshi ambayo kwa sasa kuna haha ya kuihamisha kutokana na wingi as magari na kuonekana ni ndogo.
 
44cf1bfbdb47b49ffbd10953790ac50a.jpg
9504d1f0a82e9c1bd4dc350bc1b496cd.jpg
3abeff3abab3826be118bafeac10ef7a.jpg

Hizi ni baadhi ya picha nilizopiga mida hii hapa stand ya mabus ya mkoa wa Mara maarufu kama Bweri
Hivi mbona mkoa huu na wilaya hii ya Musoma ambako ni nyumbani Kwa Baba wa Taifa kumesahaulika kiasi hiki!??
Barabara nyingi za Musoma mjini ni vumbi tupu,uwanja wa ndege vumbi tupu,stand ya mabus nayo madimbwi kibao kama muonavyo pichani
Manispaa ya Musoma naona wameisahu hii stand yani ni aibu tupu
Kama mnataka hiyo stand ichangamke, waambie wawakilishi wenu (Wabunge na Madiwani) watoe ushauri ihamishiwe Makutano hapo Round about kulikuwa kuwa na kituo cha mafuta cha Zakaria. Vinginevyo, hiyo stand itaendelea kudumaa kutokana na Geographical location ya mji wa Musoma. Ukiangalia sana mabasi ya Mwanza - Tarime - Sirari hayaingii huko Bwire, yanashusha abiria hapo Makuatano, stand ya Bweri abiria wake ni wachache sana na wengi wao ni wenaoanzia maisha hapo. Ebu angalia hata katika picha yako magari makubwa kwa maana ya magari ya kwenda mikoa mikoa mingine ni mangapi !!! ni moja tu. Hebu nenda Sirari au Tarime uone magari makubwa yalivyo mengi. Toeni stend huko mafichoni ili iwe kiungo baina ya Mkoa wa Mara na Mikoa mingine.
 
Wenye Mkoa wetu huo wa Kutukuka tumeshaizoea hiyo hali Wewe Wakuja tu huko Mkoani Mara kinakuhusu nini?
 
Wabunge si wako hapo mjini???? Muwaambie wafanye hiyo kazi. Wanazidiwa na singida ambayo iko ya mwisho kutoka chini kiuchumi
 
Kama mnataka hiyo stand ichangamke, waambie wawakilishi wenu (Wabunge na Madiwani) watoe ushauri ihamishiwe Makutano hapo Round about kulikuwa kuwa na kituo cha mafuta cha Zakaria. Vinginevyo, hiyo stand itaendelea kudumaa kutokana na Geographical location ya mji wa Musoma. Ukiangalia sana mabasi ya Mwanza - Tarime - Sirari hayaingii huko Bwire, yanashusha abiria hapo Makuatano, stand ya Bweri abiria wake ni wachache sana na wengi wao ni wenaoanzia maisha hapo. Ebu angalia hata katika picha yako magari makubwa kwa maana ya magari ya kwenda mikoa mikoa mingine ni mangapi !!! ni moja tu. Hebu nenda Sirari au Tarime uone magari makubwa yalivyo mengi. Toeni stend huko mafichoni ili iwe kiungo baina ya Mkoa wa Mara na Mikoa mingine.
Hoja zako na mada haziendani.

Kwa hiyo watu wa Musoma mjini waifuate stendi ya mabasi kijijini cha Nyankanga(wilaya ya Butiama)?

Kinachotakiwa ni stendi hiyo kuboreshwa na ndio stendi kuu ya Mkoa wa Mara kwa maana makao makuu ya mkoa ni Musoma mjini.

Kuna uzembe unafanywa na halmashauri kurekebisha stendi hii, tozo zao wanakusanya lakini marekebisho hawafanyi na hili sio tatizo la stendi hii peke yake sehemu nyingi tu watu wanapiga hela na ukarabati hawataki kufanya.
 
Stand za kiwango ni ya Morogoro pale Msamvu,Ya Singida ile inayojengwa pale na Ya Moshi ambayo kwa sasa kuna haha ya kuihamisha kutokana na wingi as magari na kuonekana ni ndogo.
Bila kusahau stand ya Tanga.
 
Hoja zako na mada haziendani.

Kwa hiyo watu wa Musoma mjini waifuate stendi ya mabasi kijijini cha Nyankanga(wilaya ya Butiama)?

Kinachotakiwa ni stendi hiyo kuboreshwa na ndio stendi kuu ya Mkoa wa Mara kwa maana makao makuu ya mkoa ni Musoma mjini.

Kuna uzembe unafanywa na halmashauri kurekebisha stendi hii, tozo zao wanakusanya lakini marekebisho hawafanyi na hili sio tatizo la stendi hii peke yake sehemu nyingi tu watu wanapiga hela na ukarabati hawataki kufanya.
Ehee, nisamehe Mkuu, ingawa asili yangu ni Nyarusurya, lakini haya mambo ya kuwa nje muda mrefu !!! Nilikuwa sijafahamu kuwa kuwa Makutano ni Musoma Vijijini ambako Makao Makuu ni Butiama, lakini hata hivyo mbona hata sasa watu wa Musoma mjini wanaifuta stand kijiji cha Bweri tena nje ya mji.
 
Nyankanga sio Musoma vijijini, huko ni Butiama.
Bweri ndio mwisho wa Musoma mjini, kuanzia kijiji cha Nyabange ni Butiama kuelekea hadi Nyankanga mpaka Kiabakari mpaka huko Butiama.
Musoma vijijini ni sehemu za Majita huko kwa Muhongo.

Japo sipo huko kwa muda mrefu ila habari zote ninazo.
Musoma vijijini na Butiama kwa sasa ni vitu viwili tofauti, zote ni wilaya na pia majimbo ya uchaguzi.
 
Pia na Stendi Kuu ya BUNDA pale..tangu imeanzishwa mpk leo ipo vilevile aisee..poor distribution of resources and poor plans
 
Mkuu Hii Stend N Kubwa Sana Lakini Viongozi Wetu Hawajali Kabisa, Ikitengenezwa Naamin Itakuwa Ya Kitaifa.
Wape Hi Sana Hapo BND,
 
Kusema kweli Tanzania ni Darasalamaa tuu huko kwingine ukienda nikama umehama Nchi vile
Hata ustaarabu wa watu wa mikoani huwa siuwezi hasa huko Kanda ya ziwa yani wapo hovyo hovyo tu...mtu kukurushia ngumi au kukutukana ni jambo la kawaida sana.
Ehee, nisamehe Mkuu, ingawa asili yangu ni Nyarusurya, lakini haya mambo ya kuwa nje muda mrefu !!! Nilikuwa sijafahamu kuwa kuwa Makutano ni Musoma Vijijini ambako Makao Makuu ni Butiama, lakini hata hivyo mbona hata sasa watu wa Musoma mjini wanaifuta stand kijiji cha Bweri tena nje ya mji.

umenikumbusha nyarusurya, nilisoma Musoma sec
 
Back
Top Bottom