Stahili za mtumishi anayejiendeleza kielimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Stahili za mtumishi anayejiendeleza kielimu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Adm, Feb 17, 2012.

 1. A

  Adm Senior Member

  #1
  Feb 17, 2012
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wasalaam wanasheria wa jf,naomba msaada wa kisheria kuhusu stahili zangu ambazo natakiwa nizidai kwa mwajiri wangu. Mi ni mwalim ambaye kwa sasa nipo chuo kikuu nikisoma shahada ya kwanza. Barua ya ruhusa kutoka kwa mwajiri kwenda kusoma inaeleza kwamba nijigharimie. Swali langu ni kwamba kwa barua hiyo sina tena haki ya kumwomba mwajiri anilipie chochote katika masomo yangu?
   
 2. k

  kijumo Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari ndugu yangu.
  hongera pia kwa kujiunga na mafunzo ya chuo kikuu. Napenda kukufahamisha kuwa kama wewe ni mtumishi wa serikali kuna ruhusa za aina mbili za masomo kwa mfanya kazi.kwanza ni ruhusa ya kusoma bila malipo na pili ni ruhusa ya kusoma kwa malipo. Mara zote mfanyakazi anapoenda kusoma barua yake ya ruhusa itaeleza moja wapo ya mambo hayo mawili. Kama umepewa ruhusa ya masomo kwa malipo utakuwa na haki zote za kupewa malipo hayo kwani huo ni mkataba ambao mwajiri amejibana (bind). Unachotakiwa kufanya wewe kama mfanyakazi ni kutovunja masharti ya mkataba wako mfano kurudi kazini wakati wa likizo na kuleta matokeo yako ya mihula. ukivunja masharti ya mkataba wako mwajiri anaweza kutumia kama kinga ya kutokulipa madai yako. Ikitokea mwajiri amekaidi kutekeleza ahadi zake una haki ya kupeleka madai yako CWT katika tawi lako.hapo ikishindikana una haki ya kwenda katika tume ya usuruhishi (comission for mediation and arbitration) na hatimaye mahakama kuu kitengo cha kazi. Sidhani kama kuna mwajiri mwenye shingo ngumu kiasi cha kukubali mfike hatua ya juu.
   
Loading...