Staa wa filamu na muigizaji A List Tyrese apagawa na Royal Tour, Bongo

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
356
Kupitia katika kurasa zake za mitandao ya kijamii wa nguli wa muziki RnB na mwigizaji wa Filamu nchini Marekani Tyrese Gibson ameonesha kupagawa na uzuri wa Zanzibar kuelezea kwa hisia jinsi ambavyo huwa hawaoneshwi uzuri wa Afrika kwenye TV zao Nchini Marekani.

Tyrese alipata video yenye kuonyesha uzuri wa fukwe mojawapo za Zanzibar kupitia ukarasa wa mwanadada Chelseanotchelss na kuiongeza maneno kuwa hii si Maldives hapa ni Heaven.

Tyrese ambaye ametokea kwenye movie nyingi zikiwemo Fast and Furious na Black and Blue ameandika hivi

“Tafuteni kwenye google, hii sehemu ya kustaajabisha inaitwa ZANZIBAR, inapatikana sehemu ya Africa iitwayo TANZANIA, walituweka sote gizani kwa makusudi.... sisi huku Marekani HUWAONA WANYAMA TU KWENYE TV ZETU, hawataki hata mmoja wetu ajue utajiri na uzuri wa kweli wa AFRIKA”

Kwa mwaka 2023 #Tyrese anakuwa Staa wa pili kupost kuhusu Tanzania ambapo wa kwanza ni Mwimbaji Camila Cabello ikiwa ni wiki chache tu toka Mwigizaji Gabrielle Union na Mumewe kuja Zanzibar kupost videos na picha wakifurahia mwishoni mwa mwaka jana.

Vision ya Dkt. Samia kuutangaza utalii imekuwa kazi rahisi zaidi kutokana na muitikio kutoka pande mbalimbali za Dunia.
 
Back
Top Bottom