St. Peters Oysterbay Liangalieni hili

St. Peters Oysterbay Liangalieni hili

Umeogopa nini kufika ofisini na kuwaambia haya!!!
Kama muumini na mchelewaji jitolee tu kuwa unakusanya viti vyote mwishoni na wanaopanga hao fikiria watakuwa wa kulipwa au kujitolea ili wachelewaji mfike mkae tu..

Just a common sense......hapa najiuliza kwa sauti.....au kuna masharti?
 
Hata tukiwahi wote haimaanishi kuwa tutaenea ndani kanisa ni dogo waumini wameongezeka. Ni wajibu wa uongozi wa kanisa kufikiria jinsi ya kuaccomodate wateja wao
Hilo wazo ni la kupeleka Kwa wahusika tena katoriki mna utaratibu mzuri unaweza kulisemea hata kwenye jumuiya yenu likafanyiwa kazi kwa haraka zaidi kuliko huku
 
Hiyo kero ipo ndani ya uwezo wako amka saa11,kawahi kupanga viti,ukiafanya mara mbili tu,utaungwa mkono na wengi
Kila mtu akileta kero ya kanisani kwake hapa sijui kama patatosha, hahahaha nawaza tu
 
Mimi kama muumini wa kanisa katoliki ningependa kutoa maoni yafuatayo kuhusu kanisa la St. Peters Oysterbay ukilinganisha na lile la Katoliki Mwananyamala (haya ndiyo ninauzoefu nayo)katika kurahisisha huduma kwa waumini.Kuna mambo mawili ambayo huwa yananikera na ambayo najua yapo ndani ya uwezo wa wahusika;
1. Upatikanaji wa viti pale nje ya kanisa kwa wale wanaochelewa , ...utaratibu wa Mwananyamala ni mzuri sana ..yaani unakuta viti vingi vimeshapangwa nje kuzunguka kanisa...hata ukichelewa kiasi gani, utakuta kuna viti vimepangwa.Hii ni tofauti na St Peters, viti huwa vipo vimerundikwa makundi makundi,mtu akichelewa inabidi awasumbue wengine ili akachukue kiti kimoja tu....Huwa najiuliza,sasa inamaana wahusika hawalioni hili ? kwa nini wasipange viti viingi pale nje waumini waje kukaa tu???tena wakati mwingine hata hivyo vilivyorundikwa unaweza usivikute mpaka uende kule Rugambwa Hall madarasani
2.Upatikanaji wa Maji ya baraka- utaratibu wa Mwananyamala ni kwamba kuna sehemu mbalimbali kule nje ambapo haya maji yamewekwa hivyo siyo lazima uingie ndani hivyo kama ulikuwa nje basi unamaliza mambo yako nje na kuondoka.......sasa pale St Peters , maji ya baraka yapo sehemu zilezile ambako miaka iliyopita ilikuwa ni sawa sababu labda waumini walikuwa wachache ...yamewekwa ndani ya kanisa tu...sasa Misa ikiisha ni vurugu kati ya waliomaliza Misa wanahitaji kutoka na wanaoingia Misa inayofuata au walikuwa wanasalia nje nao wanahitaji kuchovya maji ili waondoke...wanakutana na wale waliokuwa ndani nao wanatoka nje....ni chaos, chaos isiyo na sababu kwa kweli.........
Tunaomba wahusika walifanyie kazi suala hili ambalo halihitaji gharama kubwa katika kulitekeleza
Tatizo la waumini wa kufika kanisani siku ya jumapili tuu na kukuta kila kitu kimeandaliwa unasali unalala mbele

1.Kumbuka hakuna mtu anayemiliki kanisa ni mali ya waamini wote , hata wewe ulitakiwa uwe umewahi na kuvipanga viti hivyo

2. Kama ulikuwa na hoja ya msingi, kuna mabaraza ya walei jiunge huko na toa maoni ya kuboresha

3.Siku nyingine na anza sasa kwenda kufanya usafi kanisani , kupanga viti kwani hakuna mtu aliyeajiriwa kwa hilo na wengine waje wasali kama wageni rasmi tuu
 
Si uwaambie kwenye Jumuiya yenu ili viongozi wakienda kwenye kikao cha viongozi wa baraza la walei watoe hoja yako (japo haina mashiko)
 
Oysterbay VS Mwananyamala.Ingawa kanisa linatakiwa kuwa na viwango sawa lakini akili,mawaz,mtizamo,utendaji na ufanyaji maamuzi wa watu unaathiriwa sana na maeneo walioko!Ni dhahiri akili za kiostabei zingependa hata mabenchi yao yawe ya sofa,zingependa misa iwe ya watu wachache(na pengine wenye hadhi) hivyo basi akili hizo haziwezi kuvutika na overflow na kushughulika na overflow,wakati huku kwetu Mwananyamala Overflow ndio maisha yetu hivyo lazima tuwe juu kushughulika na mambo ya overflow!!
 
Tafuta muda ukiwa free pita pale kanisani onana na wahusika ofisini wape maoni yako watayafanyia kazi. Lile ni jengo tu kanisa ni wewe mkuu.
 
Hiyo kero ipo ndani ya uwezo wako amka saa11,kawahi kupanga viti,ukiafanya mara mbili tu,utaungwa mkono na wengi
Hawa ndio wale waumini wakienda kanisani wajshatoa Sadaka wanahisi wamelipia huduma zote, hata kwaya ikiimba haitikii utadhani ameikodi kwaya imuimbie, sala hashiriki, hata mda wa kupiga makofi hapigi,

Kama ni kijana wahamasishe viwawa wenzio muwe mnapeana zamu ya kupanga viti, kama mbaba wahamasishe uwaka, kama mmama hamasisha wawata wenzio, kama mzee kusanya rejio maria wenzio, kama karismatiki au utoto mtakatifu Fanya vivo hivo, kanisa litasonga mbele, kinyume cha hapo hutufai
 
SIkilizeni..kwa kawaid akila wiki kunakuwa na jumuiya inayoratibu na kusimamia shughuli za kanisa ,ukiachia Walei ,Viwawa,Uwata nk....hawa wanatakiwa kufanya usafi wa kanisa na mipangilio mingine...sasa wanashindwa kupanga viti kweli?..Juzi jtano ya majivu ilikuwa hivyohivyo....mpangilio haueleweki...wengine wamekaa wengine wamesimama.....sehemu hiyo hiyo...na siyo kwamba hakuna viti bali hakuna mpagilio
 
Back
Top Bottom