Bishop Hiluka
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 7,147
- 14,699
Michuano ijayo ya Kombe la Sport Pesa Super Cup, mwaka 2018, inatarajiwa kufanyika Kenya ikishirikisha timu nane za Kenya na Tanzania.
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji wa Sport Pesa inayodhamini michuano hiyo, Abbas Tarimba alisema jana wamefurahishwa na ushindani ulioonyeshwa na timu katika michuano ya mwaka huu iliyomalizika juzi kwa Gor Mahia ya Kenya kutwaa ubingwa huo.
Alisema pamoja na changamoto zilizojitokeza kwenye michuano hiyo, lengo lao la kuzinoa klabu kujiimarisha na ligi zao limefanikiwa na wanafurahi kuona hakuna malalamiko ya timu.
Hongera sana Gor Mahia, hongera Zedekiah Otieno (the team coach), hongera Kenya… muiwakilishe vema East africa on the coming match (July 13, 2017) against Everton…