Spong Cake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spong Cake

Discussion in 'JF Chef' started by Kwaito, Dec 14, 2011.

 1. K

  Kwaito Senior Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Msaada please namna ya kupika cake!!
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Keki zipo za aina nyingi, next time fafanua aina ya keki unayotaka tafadhali.

  Keki iliyo rahisi ni hii Spong Cake

  Maitaji/Vifaa


  EGGS .............................. 5
  SUGAR ............................ 1 kikombe cha robo lita
  Siagi................................¼ Kg
  Vanilla................................ Vijiko 2 vya chai
  Unga wa Ngano.................. vijiko vya chakula10
  Barking Powder................... vijiko vya chai 2
  Zabibu kavu......................... ½ kikombe cha robo lita (si lazima)

  Jinsi ya kutayarisha:
  Tia mayai na sukari kwenye blender saga mpaka iwe nyeupe (laini) kisha tia siagi (i.e Tan Bond or Blue Band) endelea kusaga mpaka iwe laini kabisa tia zabibu ¼ cup, baking powder, vanilla,and cocoa (Ukipenda) endelea kusaga halafu mwisho utatia unga vijiko 5 utamalizia kuchanganya kwenye bakuli sababu blender halitosaga kisha tia kwenye trea ya kuokea na juu utatia zabibu Kisha utaoka.

  Jinsi ya kujuwa kama keki ipo tayari ni kuingiza kijiti kwenye keki na kikitoka na mchanganyiko unao nata ujuwe bado, ila kikitoka kikavu basi keki yako ipo tayari, pia hata rangi ya nje utaiona imebadirika.

  Enjoy.
   
 3. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 1,026
  Likes Received: 172
  Trophy Points: 160
  thanx a lot mkuu for this useful thread,am gonna use this together with my lovely wife and we'll come with feedback. by the way you deserve a like.
   
 4. m

  mama dunia JF-Expert Member

  #4
  Oct 12, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye vijiko, mbona umeweka vi5 badala ya kumi tena? au unaweka nusu yake ,pls nieleweshe my dia, maana ndo najiandaa nikabake hahahah
   
 5. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  X-PASTER hapo kwenye siagi sidhani kama ni sahihi sponge cake au fatless cake kwa jina lingine huwa haitaji fat na vipimo vyake vinakuwa katika proportion sawa kwa kuongezea unga unatakiwa uwe soft kwa kuwa hakuna raising agent inayotumika na muda wa kubake huwa dk nane hadi 15 ni hayo machache ya kuongezea na kama utaamua kuweka cocoa weka kiasi saw na unga
   
Loading...