Spiritual Husband or Spiritual Wife

Spiritual Husband or Spiritual Wife

tutafikatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2011
Posts
3,431
Reaction score
4,783
Naomba kushare kama nilivyoipata
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Wake au Waume wa kiroho ni pepo wanaotumika na shetani kuvunja na kuvuruga uwapo wa familia za kimungu au kutoruhusu kuwapo kwa ndoa.


Tabia za Mke/Mume wa kiroho
1. Kumfanya mwathirika aote njozi akifanya mapenzi kila siku
2. Kuleta msumbufu katika mahusiano au ndoa
3. Kutoleta furaha, amani, n.k.
4. Kumnyang?anya mwathirika haki zake na hivyo kutoweza kutimiza wajibu wake katika familia, labda kupika, kufanya kazi fulani ambazo katika jamii husika ni wajibu wa mwathirika kutekeleza. Mfano mwanamke atamwachia mume kupika chakula au kuosha vyombo, au mwanamke kutoweza kutoa uchafu wa kitu alichotumia, akimwachia majukumu mwanaume.
5. Kumfanya mwathirika kutokuwa na heshima kwa watu wazima, au viongozi wenye mamlaka
6. Kumfanya mwathirika kuwa na matendo ya ajabu, labda kuumiza wapenzi wake kila wakati na kubadirisha wapenzi mara kwa mara bila kujali matokeo yake
7. Husababisha kukosa amani, na kuleta magonjwa yasiyoeleweka kwa waathirika, kama mtu kuumwa sana kichwa bila sababu maalumu
8. Kushawishi kwa zawadi za kimwili.
9. Kukosa huruma
10. Kuja kwa sura zilizozoeleka mara zote, kwamba ni kwenye ndoto au kimwili
11. Kuleta tamaa nyingi za mwili, na vitu vya kimwili kama vito vya thamani, n.k
12. Wana wivu sana
13. wanaweza sababisha majanga siku ya harusi
14. Wanafunga wanaume na wanawake kwenye vifungo vya kiroho vya ndoa ambavyo huketa shida ya mwili kwa waathirika
15. Wanabadirisha nyumba zenye furaha kuwa uwanja wa vita

Njia watumiazo kukuingia
1. Kurithishwa
2. Dhambi yoyotr
3. Kuangalia picha za ngono
4. Kupitia ngono au kubakwa au kujiridhisha kimapenzi
5. Kushiriki katika mambo ya kishirikina kama kuchanjwa chale, kwenda kwa waganga wa kienyeji n.k.
6. Kupitia kujichora mwili na kuchanja chale


Dalili za uwepo wao kwako
1. Kuchelewesha kupata mwenzi wa ndoa au kutofunga ndoa kabisa
2. Kufanya utamaniwe sana kimapenzi na watu kama ofisini pasipo kuwa na sababu kubwa ya maana, ya kukufanya uwe hivyo.
3. Kukosa amani katika maisha yako, kwa kuishi ukilalamika kwa kila kitu
4. Kuwa na hasira, maamuzi ya ajabu, na kujiamini kupita kiasi
5. Kuwa na magonjwa ya ajabu ambayo yaweza hata kukushawishi kujiua kama kuumwa sana kichwa pasipo sababu maalumu
6. Kutumiwa tu na wapenzi wako wa nyuma kama kuzalishwa na kisha kuachwa bila ndoa
7. Kukataliwa na opposite sex.
8. Kufanya ngono kwenye ndoto mara kwa mara
9. Kutokuwa tayari kufanya majukumu yako yakupasayo, kama kupika, kufua, n.k. Huku muda mwingi ukigawa majukumu yako kwa watu wengine na wewe ukishinda kufanya vitu vyenye uharibifu, kama kushinda kwenye internet muda wote
10. Mimba kutoka baada ya kuota ndoto ukifanya mapenzi kwenye ndoto.
11. Kushindwa kufanya mapenzi na sexual partner wako hasa katika ndoa.
12. Maumivu makali kabla ya kufanya mapenzi au kupata hisia fulani inayotoa ghafla hamu ya tendo la ndoa
13. Kuamua kuishi pasipo ndoa (stay single).
14. Kumaliza siku zako katika umri mdogo (menopause).
15. Kukosa siku zako katika ndoto.
16. Kupoteza kazi au vitu vya thamani baada ya harusi
17. Pale mpenzi wako haswaa, ambaye mmekuwa pamoja wakati wa shida na raha anapokuwa adui wako wa ghafla.
18. Unapokuwa mjamzito katika ndoto
19. Pale unapoweza kumkimbia mtu anayekupenda, kukujali, kukuheshimu kwa dhati na kutojali hatua atakaxochukua
20. Unapoota unanyonyesha, na hata usipokuwa ndotoni matiti kutoa maziwa.
21. Kushindwa kubeba mimba.
22. Kufanya Harusi ndotoni.
23. Kulea watoto ndotoni.
24. Kutoweza kuishi maisha masafi.
25. Ndoto za mara kwa mara za kuwa ?wet?.
26. Kumkimbia mwandani aliye serious kukuoa
27. Kukimbiwa na mpenzi aliyekuwa tayari kufunga ndoa nawe.
28. Kuingilia ndoa za wenzako zilizo simama
29. Kutaka uonekane umefunika pale ulipo, macho yote yawe kwako
30. Kujisikia umechoka kila siku asubuhi.
 
Ninaweka Damu Ya Yesu Ktk Mada hii, ili kila atakaesoma roho ya wokovu na kumtumikia mungu imwingie kwa jina la Yesu Kristo. Natangaza Ile Roho ya hofu ya Mungu Isimame Na C hofu ya shetani. kwa jina la Yesu Kristo,nimeomba.Amen
 
Ninaweka Damu Ya Yesu Ktk Mada hii, ili kila atakaesoma roho ya wokovu na kumtumikia mungu imwingie kwa jina la Yesu Kristo. Natangaza Ile Roho ya hofu ya Mungu Isimame Na C hofu ya shetani. kwa jina la Yesu Kristo,nimeomba.Amen

Na iwe hivyo
 
[h=2]Spiritual Husband or Spiritual Wife ndio kitu kinachoitwa jini mahaba!.[/h]P.
 
Imekuw ni shida kubwa miongoni mwa wengi na hii ni sababu ya kushiriki ngono kabla ya ndoa lakini pia kushiriki ngoni na wati tofauti tofauti ambao wamebeba hiyo roho ikumbukwe pia kuna direct cobnection katika ulimwengu wa roho wakatu wa kushiriki tendo hivyo kuambukizana mambo kama hayo ni rahisi sana Mungu atupe maarifa ya namna ya kuishi katika dunia hii iliyojaa uchafu na vurugu nyingi.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom