Spika wa kwanza mwanamke wa bunge la DRC

Spika wa kwanza mwanamke wa bunge la DRC

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,190
Reaction score
24,620
Spika wa kwanza mwanamke kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Apr 25, 2019 13:51 UTC
Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamemchagua Bi Jeanine Mabunda kuwa Spika mpya wa Bunge la nchi hiyo na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo nchini humo.
Jeanine Mabunda anatoka katika muungano wa Common Forum for Congo (FCC) unaoongozwa na Joseph Kabila ambapo aliungwa mkono pia na muungano wa Rais Felix Tshisekedi.
Bi Jeanine Mabunda alikuwa mgombea pekee baada ya mpinzani wake Henri Thomas Lokondo, kuondolewa, na zoezi hilo kususiwa na wabunge wa upinzani wakisema mchakato wa kumchagua Spika mpya wa Bunge la nchi hiyo haukuwa huru na wa haki.
Spika mpya wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anayechukua mikoba ya Aubin Minaku aliyekuwa Spika kuanzia 2012 hadi 2019 amewahi kuhudumu nafasi ya Waziri wa Viwanda na mshauri wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Joseph Kabila katika masuala ya kupambana na vitendo vya ubakaji na kuwatumia watoto kama askari vitani.
Aidha amewahi kuwa pia kiongozi wa wanawake katika chama cha Joseph Kabila cha PPRD. Wakati huo huo, wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaendelea kusubiri kwa hamu na shauku kubwa uteuzi wa Waziri Mkuu mpya, miezi kadhaa baada ya Felix Tshisekedi kuchukua mikoba ya Joseph Kabila kwenye uongozi wa nchi.
Hivi karibuni, Rais Felix Tshisekedi alikutana na Joseph Kabila na kujadiliana kuhusiana na uteuzi wa mtu anayepaswa kuchukua nafasi ya Waziri Mkuu ambayo imesalia wazi, miezi minne baada ya uchaguzi wa urais uliompa ushindi Felix Tshisekedi na kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
4bsgf4758f52611epht_800C450.jpg
 
Back
Top Bottom