Spika Sitta ngoma nzito, atoboa siri ya ujasiri wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Spika Sitta ngoma nzito, atoboa siri ya ujasiri wake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Feb 22, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Feb 22, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  • AUMIZA VICHWA KAMATI YA MZEE MWINYI

  Geofrey Nyang'oro na Ramadhan Semtawa

  SPIKA wa Bunge Samuel Sitta ametoboa siri ya ujasiri wake akisema inatokana na nguvu za Mungu, ambazo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika, bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.

  Katika kujenga kizazi kipya cha viongozi bora wa taifa hili, Spika Sitta alisema vijana wajengewe maadili mema ili kuwaepusha na ufisadi.

  Kauli hiyo ya Sitta imetolewa kipindi ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakilishambulia Bunge kwamba limewasaliti Watanzania, kutokana na uamuzi wa Spika huyo kufunga mjadala wa kashfa ya Richmond Development (LLC) hivi karibuni.

  Wakati makombora hayo yakielekezwa kwenye Bunge analoongoza, jana Spika Sitta alizidi kuonyesha kuwa bado yuko ngangari na kisha kutoboa siri ya ujasiri wake ambayo aliapa kuiendeleza.

  Spika Sitta alisema: "Siri ya ujasiri nilionao katika uongozi inatokana nami kuwa karibu na Mungu. Hali hiyo ndiyo inayoniwezesha kutekeleza wajibu wangu kwa uhakika bila kuogopa kitu chochote wala kuyumbishwa".

  Spika alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa albam ya kwaya ya Kanisa Katoliki Mtakatifu ya Michael, Parokia ya Mtakatifu Xavery Chang'ombe Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana.

  Pamoja na kusema hilo, vyanzo huru vya habari vilivyo karibu naye vimedokeza kwamba, Spika amesema yeye siye anayepaswa kumuomba radhi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuhusu kashfa ya Richmond(LLC), badala yake mbunge huyo ndiyo aombe radhi Watanzania.

  Akifafanua siri ya nguvu zake hizo katika hafla hiyo, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema mtu akiwa karibu ya Mungu neno la Mungu humsaidia kuwa mnyenyekevu mbele ya watu anaowaongoza.

  "Inashangaza kuona kuna baadhi yetu husema eti nina shughuli nyingi na kuacha nyumba za ibada. Mungu ametuumba wote tukiwa sawa. Neno la Mungu humfanya mtu kuwa kiongozi bora na pia hupunguza kiburi cha kiongozi huyo mbele ya anaowaongoza," aliweka bayana Spika Sitta.

  Spika Sitta ambaye tayari ametangaza rasmi azma yake ya kutetea kiti hicho baada ya uchaguzi wa Oktoba, aliwataka viongozi na watu wote kuwa karibu na nyumba za ibada ili waweze kujengewa uwezo na unyenyekevu mbele za watu wanaowaongoza ili wawe viongozi bora kama viongozi wa dini walivyo.

  Katika kuonyesha msisitizo, Spika Sitta aliwapigia debe viongozi wa siasa na sekta nyingine akitaka viongozi wa dini wawaalike katika shughuli kama hiyo kwa vile maeneo kama hayo yatawaweka karibu na Mungu.

  Akizungumzia nafasi ya vijana katika uongozi wa nchi, Spika Sitta aliwataka kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kutumia muda wao na nguvu zao kwa maslahi ya taifa.

  Spika ambaye anaongoza Bunge kwa kauli mbiu ya Kasi na Viwango, alisema yeye anawapenda vijana kwani kwa mara ya kwanza yeye aliingia bungeni akiwa kijana mwenye umri wa miaka 32 na alipofikisha miaka 34 aliteuliwa kuwa naibu waziri.

  Alisisitiza ni lazima vijana warithishwe maadili ili kuweza kulijenga taifa likiwa na amani na utulivu huku akisema, husikia mambo ya ovyo yanayofanywa na baadhi ya vijana aliyoyataja kuwa ni wizi, rushwa na yanayofanana na hayo.

  Vyanzo vyetu vilivyo karibu na Spika Sitta vimeeleza kwamba, mkuu huyo wa mhimili huo wa kutunga sheria amekuwa akipasua vichwa vya wajumbe wa Kamati ya Mzee Mwinyi.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, Spika amekuwa na msimamo tangu kwenye mkutano wa Halmshauri kuu (Nec) ya CCM ambao ulimlazimu Rais Jakaya Kikwete kusema kwamba, Spika na Lowassa wote ni marafiki zake hivyo lazima wasuluhishwe.

  "Ndani ya NEC ilibidi mwenyekiti wa CCM (Rais Kikwete) aweke bayana kwamba, Spika Sitta na Lowassa ni marafiki zake na tatizo kubwa ni Richmond hivyo lazima lipatiwe ufumbuzi ndiyo maana kamati ya mzee Mwinyi iliongezewa muda".

  Lakini, licha ya kamati hiyo kupewa muda wa kutafuta suluhu, Spika amekuwa na msimamo thabiti huku akielezwa kugoma kumwomba radhi Lowassa badala yake kutaka Mbunge huyo wa Monduli ndiyo aombe radhi Watanzania.

  "Alichosema Spika ni kwamba, hata kama kutakuwa na shinikizo haitakuwa rahisi kwake kumuomba radhi Lowassa badala yake yeye (Lowassa) ndiyo awaombe radhi Watanzania kwanza," kilidokeza chanzo hicho.

  Kwa mujibu wa chanzo hicho, mzee Mwinyi na kamati yake wamekuwa katika wakati mgumu na huenda wakarejesha ripoti katika muda uliopangwa bila kupata suluhu kati ya watu hao.

  "Spika Sitta hawezi kuomba radhi na Lowassa pia inaweza kuwa hivyo hivyo, sasa unategemea kuna suluhu hapo? Spika amekwisha sema hana ugomvi na Lowassa bali anasimamia maadili, sasa aombe radhi ya nini?" kilihoji chanzo hicho.

  Tangu kuibuka kwa sakata la mkataba wa kifisadi kati ya kampuni ya Richmond na Tanesco, uliosainiwa Juni 23, 2006, kisha kusababisha Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu na Rais Kikwete kuvunja baraza la mawaziri, CCM na Bunge hata serikali vimejikuta vikiingia katika mgawanyiko mkubwa.

  Kundi la Lowassa ambalo linaundwa na watu wenye nguvu ya fedha wamekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya CCM na hata bungeni, lakini Spika Sitta akiwa na kundi dogo la watu majasiri wanaojiita wapiganaji kumesababisha msuguano ndani ya CCM na bunge ambalo asilimia kubwa ya wabunge ni wa chama hicho.

  Mgawanyiko huo ndiyo uliyoifanya NEC kuunda kamati ya mzee Mwinyi ikiwa na wajumbe watatu ambao ni Abdulrahman Kinana na Katibu Pius Msekwa, kutafuta suluhu hiyo.

  Hata hivyo, kamati hiyo iliyoanza kazi Agosti mwaka jana ilishindwa kumaliza tatizo hilo baada ya Spika kukataa suluhu na Lowassa.

  Licha ya Spika kukubali kuizika hoja ya Richmond bungeni bado msuguano uliendelea ndani ya chama na hivyo mkutano wa NEC uliofanyika hivi karibuni uliamua kuongezea muda kamati ya mzee Mwinyi kwa kuitaka ichunguze kiini cha tatizo.
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,323
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tusubiri hatma yake hivi karibuni tu.
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Amtumainiye Mungu ni kama mlima wa Sayuni. Wala hautikisiki, milele na milele!
   
 4. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #4
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  huyo ni muongo......... anatafuta huruma ya wanachi baada ya kuboronga!!.......tena anajua fika kuwa uspika tena kwa tiketi ya ccm, ni miujiza tu inaweza kumpa.................
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  Feb 22, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kama kweli anamtegemea Mungu...angerudisha hizo million 46 atakazopata mwisho wa bunge. Tena yeye anapata million 92...maana ni baba na mama wako bungeni! Kudadadeki! Tunadanganyana humu!!
   
 6. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #6
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,187
  Likes Received: 2,715
  Trophy Points: 280
  Kaka fafanua muongo kivipi?
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  kila mtu anasili za ujasili wake.........mfano lowasa na rostamu siri ya ujasili wao ni jeuli ya FEDHA......................
   
 8. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,036
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  utoto huuuuuuu.......................basi kagombee na wewe.....miwivu tu
   
 9. Elisante Yona

  Elisante Yona Senior Member

  #9
  Feb 22, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 130
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mimi ninasema ni wakati wa Mungu kujidhihirisha hapa tanzania.na kweli kama mtu Mungu yuko upande wake haya yote ambayo yamefichwa gizani yatafunguliwa maana watanzania haya yote tunayaweka mikononi mwa Mungu aliye hai,hawa wote ni kuwapiga chini uchuguzi wa mwaka huu,watanzania tuanze safu mpya ya viongozi wenye hofu ya Mungu na sio maneno maneno.

  Elisante Yona
   
 10. T

  TumainiEl JF-Expert Member

  #10
  Feb 22, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 3,064
  Likes Received: 1,974
  Trophy Points: 280
  Sita Anastaili pongez zakimataifa. Huyu naiman atakuja kuwa rais wetu na hakika taifa hili litakuwa Paradiso ndogo. Mungu ibariki Tz na Mungu mbarik spika Sita. Amen
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Hawa nao tumewachoka sasa.
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ha! ndio maana wanapigana vikumbo kumbe 2015 target aisee jamaa wanaakili ya kula nchi?
   
 13. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Sijui ni ujasiri upi alioufanya na umesaidia vipi katika kutetea maslahi ya nchi. Richmond imezimwa, Sakata la Vitambulisho vya taifa limezimwa, EPA wahusika wote bado wanapeta, wachukuaji bado wanachukua rasilimali zetu na kutuachia 3% tu! Kiwira imezimwa, sasa sielewi ni ujasiri upi anaouzungumzia labda aseme usanii tu.
   
 14. Mlenge

  Mlenge Verified User

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: Oct 31, 2006
  Messages: 462
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Spika, pamoja na Bunge, ni taasisi zilizofeli kulinda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa vile zimeridhia mikataba ya Afrika Mashariki, ambayo, pamoja na mambo mengine, inalipunguzia mamlaka na madaraka bunge hilo. Even from 'selfish-point of view', wangeukataa mkataba wa EAC, (ulikataliwa wakati wa Msekwa), hata kama hawaipendi nchi hii.

  Wakiwa marais watatawala nini? Mamlaka yote yamepelekwa EAC.

  Au shida ni kwamba wawe watawala tu, wenye misafara na kuitwa waheshimia, as an end in itself?

  Halafu sisi wananchi ndio tunajiletea wenyewe matatizo. Hizo milioni 46 kiinua mgongo ni dola ngapi? 30,000 or so. Hata mshahara wa wiki moja wa mchezaji wa wastani uingereza ni mkubwa kuliko huo. Matokeo ya kuwalipa Wabunge hela 'njiwa' compared to wenzao wa nji jirani, au wale wa bunge la EAC, huwafanya Wabunge waone kitu kama Bunge la EAC kama mlango mwingine wa kuweza kujipatia 'ulaji', wakiishi kwa matumaini kwamba siku moja zamu inaweza kuwa yao kwenda 'kwenye ulaji' au wakienda wengine wanawapunguzia wao ushindani wa ulaji 'mdogo' wa Bunge letu.

  So anyone with dreams of being President of Tanzania, while not fighting to preserve the union and consitution of Tanzania which membership to EAC duly violates, how should we call them?
   
 15. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,534
  Likes Received: 1,542
  Trophy Points: 280
  afafanue nini vitu viko wazi..na huyu mzee kazidi anatumia majukwaa ya kuzindua albamu za disco la yesu kuongelea siasa...too low for him...hivi akikjaa kimya domo linamuwasha..?
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Kila la heli Mhe Sitta, kila lenye wema hupingwa na wengi, wakati wa BWANA YESU kuuleta ukweli duniani aliungwa mkono na wachache kuliko waliompinga, hata dunia ya sasa ina watu wengi wanaokufuru kuliko wanao sifu uwezo wa MUNGU, songa mbele bila kujari nani atasema nini au nani atafanya nini, Ni heri kufa mtu ukipigania KWELI ya MUNGU kuliko kuishi ukiwa fisadi na adui wa MUNGU kwani lipi lililo jepesi mtu kuwa adui wa wanadamu kwa kusema ukweli, ama adui wa MUNGU kwa kuukumbatia uovu?
  Imeandikwa, hakuna atayekuwa rafiki wa wanadamu akiibeba kweli maana, hiyo kweli ni mkuki kwa waovu,
   
 17. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #17
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  hatuwezi kuuliza utimamu wa akili yako, twayaona maneno yako, yanadhihirisha udhaifu na ufinyu wa mawazo yako na kuonesha
  usivyokuwa na chembe hata kidogo ya upembuzi
   
 18. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #18
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  amefanya nini jamani?
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  huwa watu wanawasingizia watu wa vijijini kuwa hawajaamka, angalia humu wanaomsupport Sitta na uwaulize kafanya nini!

  Sitta ni CCM, kamati ya mwinyi ni CCM, haitakiwi uwe na chetu cha darasa la saba kujua mchezo unaochezwa hapa

  mwaka wa uchaguzi huu!
   
 20. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #20
  Feb 23, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  shida wewe hata hujui kuwa ni pesa yako ndo wanaenda kula!! Kwenda shule muhimu sana!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...