Spika Sitta ngoma nzito, atoboa siri ya ujasiri wake

Critics, crtitics! ......mkubali msikubali mzee Sitta mchago wake mkubwa sana...kafanya bunge japo liwe na meno.....mmessahau wakati wa Msekwa? utafikiri wabunge wote walikuwa na degedege. Watu msio na shukrani nakuambieni, ingekuwa enzi za Msekwa, Richmond isingeleta dhoruba yeyote kwa serikali.Period! Mpeni mtu haki yake, Sitta ni kiongozi shupavu.
 
  • AUMIZA VICHWA KAMATI YA MZEE MWINYI
Geofrey Nyang'oro na Ramadhan Semtawa

SPIKA wa Bunge Samuel Sitta ametoboa siri ya ujasiri wake akisema inatokana na nguvu za Mungu, ambazo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika, bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.

ni vizuri kumtegemea mungu...inakupa matumaini ya namna fulani...na ni vizuri kuishi kwa matumaini kwani unaongeza muda wako wa kuishi.....

my take on this:
siku zake kama spika zinahesabika na bahati mbaya kwake naye anafahamu hilo...kitu ambacho ni interesting katika hili sakata ni kuwa the real power behind the show....EL...mwanaume wa shoka as per bi SS...yuko kimya akiendelea kuchanga karata zake...au pengine tuseme akinoa jambia la kuwafyeka wabaya wake...

mi nadhani mzee 6 ajiandae kuishi maisha ya kustaafu...kama ana washauri basi ni vema wakamweleza ukweli...he is finished na namna richmond ilivyokwisha baada ya lele zote walizopiga yeye na wale ambao Bi SS alidai njaa inawasumbua inatosha kuwa ni dalili ya hiki nnachokidai...

wamevuna walichopanda....mwenye macho haambiwi tazama...
 
SPIKA wa Bunge, Samwel Sitta amewataka viongozi nchini kusikiliza maoni ya viongozi wa dini na kwamba wanasiasa wanapaswa kuwa wasafi.

Spika Sitta aliyasema hayo jana wakati akichangisha harambee ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya kisasa inayotarajiwa kujengwa Kitunda jijini Dar es salaam na masista wa shirika la wabenekitini la mtakatifu Agnes lililopo Chipole mkoani Ruvuma.

Alisema viongozi wa dini wamekuwa wakitoa mchango mkubwa katika ujenzi wa shule, zahanati, hospitali, kutunza yatima na kufanya shughuli mbali mbali katika jamii na kwamba mchango huo, unafurahiwa na viongozi wa siasa.

Alisema kanisa katoliki nchini limefanya mambo mengi mazuri na watu wengi wamepata elimu kupitia shule za kanisa hilo, pia baadhi ya shule bora hapa nchini zimekwa zikimilikiwa na kanisa hilo.

Alisema pia zahanati na hospitali nyingi nchini ni ubia kati ya serikali na kanisa katoliki na kwamba kupitia vituo hivyo, wananchi wamekuwa wakipata matibabu ya uhakika.

"Sisi viongozi tuwe na moyo wa kuwasikiliza viongozi wa dini tupokee maoni kutoka kwa watu mbalimbali, mengine yanaweza kuwa ya mekosewa kwa sababu sitegemei askofu anaelewa utendaji kazi katika ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali, lakini anapotoa maoni ya kujenga ni lazima tuyafuate,"alisema Sitta.

Aliwataka viongozi wa madhehebu yote ya dini wasisite kukosoa viongozi wa siasa kwani ni haki yao na kuwashauri viongozi hao kujenga tabia ya kuwasikiliza viongozi wa dini wanapozungumzia maadili ya dini.

Awali Askofu Mkuu wa Jimbo la Songea Norbert Mtega alisema wameamua kujenga kanisa hilo, Dar es salaam badala ya Songea kwa kuwa kanisa katoliki lipo kwa ajili ya Taifa zima na litaendelea kutoa huduma sehemu yoyote duniani hivyo ni wajibu kusaidia jamii na kuwataka watu wote wenye uwezo wa kuchangia wasaidie kutoa michango ili wafanikishe ujenzi wa hospitali hiyo.

Aliwataka masista hao, kuwaombea daima wahisani wao ambao wamewasaidia kuchangia ujenzi huo ili waweze kufika mbinguni pia amewataka waendelee kutoa huduma bora kwa jamii, ikiwemo elimu, afya pamoja na kutunza yatima na maskini kwani wao ni wamisionari na kazi yao ni kutoa huduma na kuombea watu.

CHANZO MWANANCHI
 
  • AUMIZA VICHWA KAMATI YA MZEE MWINYI
Geofrey Nyang'oro na Ramadhan Semtawa

SPIKA wa Bunge Samuel Sitta ametoboa siri ya ujasiri wake akisema inatokana na nguvu za Mungu, ambazo zimekuwa zikimwezesha kutekeleza wajibu wake kwa uhakika, bila kuyumbishwa wala kuogopa kitu chochote.

Katika kujenga kizazi kipya cha viongozi bora wa taifa hili, Spika Sitta alisema vijana wajengewe maadili mema ili kuwaepusha na ufisadi.

Kauli hiyo ya Sitta imetolewa kipindi ambacho baadhi ya watu wamekuwa wakilishambulia Bunge kwamba limewasaliti Watanzania, kutokana na uamuzi wa Spika huyo kufunga mjadala wa kashfa ya Richmond Development (LLC) hivi karibuni.

Wakati makombora hayo yakielekezwa kwenye Bunge analoongoza, jana Spika Sitta alizidi kuonyesha kuwa bado yuko ngangari na kisha kutoboa siri ya ujasiri wake ambayo aliapa kuiendeleza.

Spika Sitta alisema: "Siri ya ujasiri nilionao katika uongozi inatokana nami kuwa karibu na Mungu. Hali hiyo ndiyo inayoniwezesha kutekeleza wajibu wangu kwa uhakika bila kuogopa kitu chochote wala kuyumbishwa".

Spika alisema hayo wakati wa hafla ya uzinduzi wa albam ya kwaya ya Kanisa Katoliki Mtakatifu ya Michael, Parokia ya Mtakatifu Xavery Chang'ombe Jimbo Kuu la Dar es Salaam jana.

Pamoja na kusema hilo, vyanzo huru vya habari vilivyo karibu naye vimedokeza kwamba, Spika amesema yeye siye anayepaswa kumuomba radhi Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kuhusu kashfa ya Richmond(LLC), badala yake mbunge huyo ndiyo aombe radhi Watanzania.

Akifafanua siri ya nguvu zake hizo katika hafla hiyo, Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo Mashariki (CCM), alisema mtu akiwa karibu ya Mungu neno la Mungu humsaidia kuwa mnyenyekevu mbele ya watu anaowaongoza.

"Inashangaza kuona kuna baadhi yetu husema eti nina shughuli nyingi na kuacha nyumba za ibada. Mungu ametuumba wote tukiwa sawa. Neno la Mungu humfanya mtu kuwa kiongozi bora na pia hupunguza kiburi cha kiongozi huyo mbele ya anaowaongoza," aliweka bayana Spika Sitta.

Spika Sitta ambaye tayari ametangaza rasmi azma yake ya kutetea kiti hicho baada ya uchaguzi wa Oktoba, aliwataka viongozi na watu wote kuwa karibu na nyumba za ibada ili waweze kujengewa uwezo na unyenyekevu mbele za watu wanaowaongoza ili wawe viongozi bora kama viongozi wa dini walivyo.

Katika kuonyesha msisitizo, Spika Sitta aliwapigia debe viongozi wa siasa na sekta nyingine akitaka viongozi wa dini wawaalike katika shughuli kama hiyo kwa vile maeneo kama hayo yatawaweka karibu na Mungu.

Akizungumzia nafasi ya vijana katika uongozi wa nchi, Spika Sitta aliwataka kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kutumia muda wao na nguvu zao kwa maslahi ya taifa.

Spika ambaye anaongoza Bunge kwa kauli mbiu ya Kasi na Viwango, alisema yeye anawapenda vijana kwani kwa mara ya kwanza yeye aliingia bungeni akiwa kijana mwenye umri wa miaka 32 na alipofikisha miaka 34 aliteuliwa kuwa naibu waziri.

Alisisitiza ni lazima vijana warithishwe maadili ili kuweza kulijenga taifa likiwa na amani na utulivu huku akisema, husikia mambo ya ovyo yanayofanywa na baadhi ya vijana aliyoyataja kuwa ni wizi, rushwa na yanayofanana na hayo.

Vyanzo vyetu vilivyo karibu na Spika Sitta vimeeleza kwamba, mkuu huyo wa mhimili huo wa kutunga sheria amekuwa akipasua vichwa vya wajumbe wa Kamati ya Mzee Mwinyi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Spika amekuwa na msimamo tangu kwenye mkutano wa Halmshauri kuu (Nec) ya CCM ambao ulimlazimu Rais Jakaya Kikwete kusema kwamba, Spika na Lowassa wote ni marafiki zake hivyo lazima wasuluhishwe.

"Ndani ya NEC ilibidi mwenyekiti wa CCM (Rais Kikwete) aweke bayana kwamba, Spika Sitta na Lowassa ni marafiki zake na tatizo kubwa ni Richmond hivyo lazima lipatiwe ufumbuzi ndiyo maana kamati ya mzee Mwinyi iliongezewa muda".

Lakini, licha ya kamati hiyo kupewa muda wa kutafuta suluhu, Spika amekuwa na msimamo thabiti huku akielezwa kugoma kumwomba radhi Lowassa badala yake kutaka Mbunge huyo wa Monduli ndiyo aombe radhi Watanzania.

"Alichosema Spika ni kwamba, hata kama kutakuwa na shinikizo haitakuwa rahisi kwake kumuomba radhi Lowassa badala yake yeye (Lowassa) ndiyo awaombe radhi Watanzania kwanza," kilidokeza chanzo hicho.

Kwa mujibu wa chanzo hicho, mzee Mwinyi na kamati yake wamekuwa katika wakati mgumu na huenda wakarejesha ripoti katika muda uliopangwa bila kupata suluhu kati ya watu hao.

"Spika Sitta hawezi kuomba radhi na Lowassa pia inaweza kuwa hivyo hivyo, sasa unategemea kuna suluhu hapo? Spika amekwisha sema hana ugomvi na Lowassa bali anasimamia maadili, sasa aombe radhi ya nini?" kilihoji chanzo hicho.

Tangu kuibuka kwa sakata la mkataba wa kifisadi kati ya kampuni ya Richmond na Tanesco, uliosainiwa Juni 23, 2006, kisha kusababisha Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu na Rais Kikwete kuvunja baraza la mawaziri, CCM na Bunge hata serikali vimejikuta vikiingia katika mgawanyiko mkubwa.

Kundi la Lowassa ambalo linaundwa na watu wenye nguvu ya fedha wamekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya CCM na hata bungeni, lakini Spika Sitta akiwa na kundi dogo la watu majasiri wanaojiita wapiganaji kumesababisha msuguano ndani ya CCM na bunge ambalo asilimia kubwa ya wabunge ni wa chama hicho.

Mgawanyiko huo ndiyo uliyoifanya NEC kuunda kamati ya mzee Mwinyi ikiwa na wajumbe watatu ambao ni Abdulrahman Kinana na Katibu Pius Msekwa, kutafuta suluhu hiyo.

Hata hivyo, kamati hiyo iliyoanza kazi Agosti mwaka jana ilishindwa kumaliza tatizo hilo baada ya Spika kukataa suluhu na Lowassa.

Licha ya Spika kukubali kuizika hoja ya Richmond bungeni bado msuguano uliendelea ndani ya chama na hivyo mkutano wa NEC uliofanyika hivi karibuni uliamua kuongezea muda kamati ya mzee Mwinyi kwa kuitaka ichunguze kiini cha tatizo.

wanafamilia wa jamii forum kuna mtu anahotuba ya kikwete alihutubia watanzania kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa kiongozi wa nchi kupitia bunge la jamhuri ya muungano hotuba ya tarehe 31.decemba 2005 naomba mutuletee tuisome upya tafadhali.
 
Mmh jaman Sitta nae ni binadam kama sis na anamapungufu yake lakini kajitaidi
 
Back
Top Bottom