Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,892
Anaandika #Bollen_Ngeti
SPIKA NDUGAI ANATAKA LISSU AFE??
KITENDO cha Bunge la Ndugai kumfutia mshahara na posho zingine za kibunge Tundu Lissu ni unyama na ushahidi wa dhahiri kuwa Spika Job Ndugai akibanwa anaweza walau kusaidia kujua waliopanga kumuua kwa mabunduki Lissu September 7, 2017.
Mwanzoni nilijua ni kauli tu za kisiasa lakini kwa Ndugai kuamua kweli kumfutia mshahara Lissu ni jaribio jingine la kutaka kumuua Lissu na safari hii naona wanataka afe kwa njaa na familia yake.
Risasi 16 zilishindikana kumuua Lissu baada ya Mungu kusimamia "show". Jaribio la pili lilikuwa ni kumfutia dhamana ili akamatwe na Interpol aswekwe ndani na magongo yake na majeraha. Hakika angekufa kwa mateso na uchungu. Hili nalo Mungu akaepusha. Mahakama ikakataa. Safari hii naona njia sahihi iliyochaguliwa ni kumfutia mshahara Lissu ili afe kwa njaa, watoto wasiende shule, ndugu tegemezi waathirike. Huku ni kumuua Lissu na ni uthibitisho kuwa nguvu ya kummaliza Lissu ni kubwa mno kiasi kwamba bila Mungu Lissu si kitu!
Ndugai anadai hajui aliko Lissu na anafanya nini huko asikojua. Ndugai akumbushwe tu kwamba Lissu yuko hospitali huko Ubelgiji akipatiwa matibabu baada ya kupigwa risaso 38 na 16 kumuingia mwilini na hivi karibuni amemaliza kufanyiwa upasuaji wa 23. Anasubiri uamuzi wa madaktari kumruhusu kutoka au la!
Lissu ni Mtanzania kama wewe na mimi. Ana ndugu, jamaa na marafiki hata ndani ya Mafikizolo, Chadema, Inzile, Gweregwere, CUF, jeshini, TISS, vyuoni, Magogoni nakadhalika! Tumuombee apone ili awatumikie wananchi wake. Tofauti zetu kisiasa zisitutofautishe hadi kufikia kuuana kwa njaa. Wabunge wote unganeni kumpinga Ndugai, pigeni kelele hadi nchi za mbali kupinga uamuzi huu wa Ndugai. Kumbukeni wakimmaliza Lissu watakugeukieni na ninyi. Hakuna aliye salama kwa sasa!
#AchaWoga2020