Spika Ndugai tunaomba pia mchanganuo wa Uchangiaji Bungeni licha ya Mahudhurio

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,523
4,991
Tumesikia Spika akitoa mchanganuo wa mahudhurio bungeni. Kilichonistua kidogo ni kwamba wale wabunge wote waliotajwa kuwa na mahudhurio mazuri Bungeni, ni majina ambayo siyafahamu kabisa, yaani siyo wabunge ambao ni maarufu kwa michango yenye kufikirisha na yenye mchango mkubwa kwa taifa. Hilo likanifanya nianze kufikiria zaidi.

Mfano Lema anaongoza kwa kuwa na mahudhurio hafifu. Lakini hata ukiangalia tu clip zinazopenya kutoka bungeni kuja mitandaoni, anaonesha kwamba ule muda mchache anaopata kuingia Bungeni, anautumia kikamilifu katika KUIHENYESHA SERIKALI, akitekeleza wajibu wake wa kikatiba kwamba UPINZANI KAZI YAKE NI KUIKOSOA NA KUISIMAMIA SERIKALI. Mbunge anaweza kufika siku moja tu bungeni na akatoa mchango mkubwa ambao unalifaa taifa, kuliko mbunge ambaye hakosi hata siku moja, lakini hatoi mchango wowote: Hasomi miswada, hafanyi utafiti, hatoi mchango wowote unaowezesha miswada kuboreshwa. Huyu anatia hasara kubwa afadhali hata huyo mbunge ambaye anatumia muda mwingi mahakamani kupambana na dola ambalo lina sheria kandamizi.

Ukimwangalia Lema, anatoa mchango mkubwa sana kwa taifa, siyo kizazi hiki tu, bali hata vizazi vijavyo. Maandishi yake, mazungumzo yake, clip zake, zitaendelea kuwepo, na ni somo zuri kwa watanzania. Lema yuko very active ndani na nje ya Bunge, na ni mbunge mahiri kwa vigezo vyovyote.
Lakini pia ujasiri wake ni somo tosha kwa vijana kwamba kama ni mpambanaji basi upambane kwelikweli. na hii yote inaonekana licha ya jitihada za serikali ya JPM kuzima bunge live, kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, na kubana uhuru na demokrasia kwa kila hali.
kwa hiyo hiyo rula ya kutumia utoro bungeni haitoshi kutupa taarifa kuhusu utendaji. Na pia sishangai kumsikia Ndugai akitoa Takwimu za "mahudhurio" pekee, kwa sababu zitawainua kidogo vilaza wa CCM. Tunahitaji sasa mchanganuo mwingine kutoka kwa Spika wetu, ambao utazingatia idadi ya hoja anazotoa,
 
Kiranja Rungu hawezi kusema hata walioyasema kwa kuwa Chumba Cha Mauaji hakuna msemaji zaidi ya Muuaji Mkuu.
 
Hao CCM wanahudhuria ili kujikusanyia 'sitting allowance' tu, na si kingine. Mahudhurio yao hayana faida yoyote. Huyo Lema wanayesema ana mahudhurio hafifu ndio namuona ana mchango kubwa wenye tija awapo bungeni kwa hizo siku chache kuliko hao wanaohudhuria vikao vyote.
 
Back
Top Bottom