Spika Ndugai: PhD zina manufaa kwenye kufundisha na kutafiti lakini siyo bungeni, Dkt. Ndugulile aliwahi kumuita Waziri Profesa Ziro

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,012
142,044
Akimpongeza mbunge wa Mtera mh Lusinde kwa uchambuzi mzuri wa hotuba ya Waziri Mkuu uliotumia dakika 15 Spika Ndugai amesema Kibajaj anawazidi wasomi wengi mle bungeni.

Spika amesema bungeni yanahitajika maarifa huo uprofesa ni kwa ajili ya kufundisha na kufanya tafiti hivyo katika siasa uprofesa hauna maana yoyote.

Ndio maana wabunge watatu wamewaponda maprofesa tukianza na Kishimba, Kibajaji na kuna wakati Dr Ndugulile aliwahi kumuita waziri fulani Profesa Ziro nikamtoa nje haa haaa amecheka Ndugai.

Ndugai amewataka maprofesa kuwa makini wanapohutubia bungeni kwani darasa la 7 akina Kibajaji, Msukuma Tabasamu, Jah people, Kiinanasi, Babu Tale nk nk wako makini kweli.

Chanzo: TBC

My take; Mbona wabunge wa darasa la 7 ni wanaume watupu!
 
Pumbavu, mawazo ya darasa la saba! Kwanza ukiwafuatilia ni tabia za kujipendekeza, pili kwa kuwa muda wote utetea mihimili lazima wapongezwe, ila bila kujali matakwa ya baadhi ya waliodhulumika leo kumsema jiwe kwa matendo yake maovu haitajiki elimu yeyote.

Mtu ametenda mabaya asemwe faida wengine wasirudie maovu, wawekezaji wamekimbia, biashara zimeuwawa, uchaguzi umearibiwa, watu waliishi kwa hofu, uhuru finyu, ndio tupongeze? Watapongeza hao hao kina kibajaji!
 
Halafu eti ndio bunge hilo tunategemea liishauri serikali ili tupate maendeleo!

by the way Ndu guy anasikitisha sana, hao la 7B wanaongea pumba tu hakuna substance yoyote ile...ni mafundi wa kuongea kwa kutiririka tu kama pipa lililoachiwa juu ya kilima na kukosa uelekeo!
 
Tatizo hicho kinundu kichwani
 
Shida ya mjinga zinaanzia hapo; anadumu akijiamisha kujua, na kumbe anaendelea kutojua kwamba hajui.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…