Spika Ndugai awaonya wabunge kuanzia kikao kijacho

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Jan 3, 2012
4,582
2,783
DIDyOEBXYAAdS9u.jpg

Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wabunge watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu bungeni hawatavumiliwa na huenda adhabu ikaongezeka maradufu kwa wasiozingatia kanuni.

Ndugai aliyekuwa nje ya nchi kwa mwezi mmoja akitembelea Nigeria, Dubai na Iran alisema hayo jana alipojibu swali la mwandishi wa habari.

Spika Ndugai alisema vikao vya mkutano ujao wa Bunge vitaanza Septemba 5. “Tumekuwa tukiwatoa nje mara kadhaa lakini imefika mahali tumewafungia wengine mwaka mzima, ila sasa tumechoka wakirudi na wakaendelea na jeuri yao msishangae adhabu zikapanda na kuwa kubwa zaidi, kwa sababu tumechoka,” alisema.

Wabunge Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini), wote Chadema, walisimamishwa katika mkutano uliopita wa Bunge kuhudhuria vikao vya mkutano wa saba, nane na wa tisa hadi mwakani, ambapo watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi 10 kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya chombo hicho cha kutunga sheria.

Ndugai awaonya wabunge kuanzia kikao kijacho
 
Mbona Bunge la wananchi lilishakwisha enzi za JKN sasa hivi haya Mabunge yanayolipwa kwa fedha za walipa kodi ni Mabunge ya watawala.Wakishatoka watakuja kusimulia namna walivyokuwa wakikiuka kutenda haki
 
Nigeria, Dubai na Iran ndiko alikokwenda kujifunza namna ya kuendesha mabunge ya vyama vingi?
 
Huu jamaa anakamia sana mechi kama ile timu iliyobadilisha jezi! Haiwezekani mtu useme ukibalehe (bunge likianza) utagonga sana mademu!
 
Huyu mchapabakora anafuata maagizo kutoka juu hajui kuwa yeye pia ni kiongozi wa mhimili unaojitegemea
Mara nyingi watawala au mwenye cheo hujisahau hafikirii kesho yeye huona hapa tu. Akumbuki kuwa kuna kesho kutwa au kuna siku atatoka kwenye wadhifa huo. Hakika nawaambia watakaopata shida ktka uzee wao kama mungu atawaweka hai ni pamoja na Ndugai na Magufuli Kinga ya kutoshtakiwa rais ipo siku itatolewa tu. Na wakati huo ndio wanaelekea ktk umri ule wa akina Kingunge. Wasijisahau watoto wetu wajukuu wetu wanakuja kwa hari na technolijia ya kisasa hizi maonezi au siasa za kuoneana yataisha na itakuwa ni DEMOKRASIA. Ndio hapo sheria itakapofuata mkondo wake hata wakiwa na miaka 100.
 
Spika Ndugai alisema vikao vya mkutano ujao wa Bunge vitaanza Septemba 5. “Tumekuwa tukiwatoa nje mara kadhaa lakini imefika mahali tumewafungia wengine mwaka mzima, ila sasa tumechoka wakirudi na wakaendelea na jeuri yao msishangae adhabu zikapanda na kuwa kubwa zaidi, kwa sababu tumechoka,” alisema.

Wakibaki wenyewe wa Mcc patakuwa uwanja mzuri wa kupitisha mambo kuulaini! Asipate shida sana!
 
..yeye anafikiria kuwafanyia wenzake ubaya mda wote...nani amemhakikishia kuwa yeye atafika kikao kijacho cha bunge?...au anasahau kuwa yote upangwa na Muumba!..ulevi wa madaraka mbaya mno mno.....
 
Hata akifanyaje speaker ajaye sio yeye!! Atakuwa speaker wa kwanza mstaafu ndani ya Bunge maana njaa bado anayooo!!!!! Tena sanaa
 
Hizo akanuni wanazozitumia kuadhibu wabunge wa upande mmoja wakumbuke kuwa ipo siku nawao wataondoka madarakani,wenzao watakapokuja kuwageuzia kibao kwa kuanza kuzitumia dhidi yao wasije wakalalamika.
 
inasikitisha kuona spika wa bunge akili yake kuwaza namna gani ya kuwakomoa wabunge wa upinzani... badala ya kuja na mawazo mapya na yamaendeleo aliyojifunza uko ughaibuni......
 
Back
Top Bottom