Spika Ndugai ashangaa Kubenea kukamatwa na Polisi akiwa mgonjwa

Kisa idadi ya risasi ilipishana na ya Mzee wa Bakora.Hivyi Hitler anaweza akazaliwa tena akawa na ngozi nyeusi?
 
Spika Ndugai amefunguka hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio na kusema kwamba Kubenea alikuwa ameitwa na Kamati ya Maadili lakini yeye akawa ametoroka kurudi Dar es Salaam jambo ambalo lililazimu akamatwe na baada ya kufikishwa kwenye kamati akawa ameshindwa kuhojiwa kutokana na kuonekana kuwa hayuko sawa kiafya.

Spika Ndugai amesema Kamati kuendelea kukaa ofisini kwa muda mrefu ni gharama sana ndiyo maana polisi walitumika kumkamata na siyo walifanya kumkamata kwa sababu walikuwa wanajua kuwa ni mgonjwa.

"Hakukamatwa kwa sababu ni mgonjwa, Kubenea alitakiwa aonane na Kamati ya Maadili, yeye akatoroka kwenda Dar es salaam. Kamati kukaa hapa ndani ya wiki moja ni mishahara ya kutosha ndiyo maana polisi wakaenda kumkamata, Kama alikamatwa akiwa mgonjwa ni bahati mbaya. "Hakukamatwa kwa sababu ni mgonjwa. Lakini kama ukiitwa kwenye mamlaka ya kimahakama lazima utoe ushirikiano kama unaumwa unasema tu na cheti cha daktari unaonyesha . Kama huumwi utakamatwa tu" amesema

Ameongeza kwamba "Kuwa mbunge hakukufanyi kuwa mtu mwenye mapembe. Lazima ufate sheria na taratibu zinavyotaka kwani mbunge ni sawa na mwananchi mwingine yeyote"

Katika hatua nyingine Spika Ndugai amefunguka na kusema Mbunge anakuwa na kinga kidogo pale anapokuwa kwenye ukumbi wa bunge na akitoka nje anakuwa kama mwananchi wa kawaida na hata kinga yake inakuwa imepotea.

Ameongeza pia yeye kuagiza Wabunge kukamatwa wanaofanya vitu vya kutengenezea bunge picha mbaya ni kazi yake kwa sababu kiongozi huyo tayari amelihusisha bunge hivyo kuagizwa watu wanaotoa maoni yao mitandaoni wahojiwe ni sahihi.

"Mbunge anayeropokea popote mimi nitamshughulikia tu, kwani ni kudhalilisha bunge letu. Haijalishi kwamba umezungumzia ukiwa nchi gani au mtandaoni sisi lazima tukuhoji na wewe utakuwa umepata fursa nzuri ya kujieleza kuhusu nini ulikuwa unamaanisha" ameongeza.

Chanzo: EATV

Albadir imeashàjibu tutashuhudia kauli za kujikanyaga sana.
 
Jamaa muongo sana tunavinajisi vitabu tukufu wanavyoapia kipindi wakiapishwa wanavyovishika.
 
Kongwa ni moja ya wilaya masikini sana,mwaka wa juzi,watu walipata njaa mpaka wakawa wanakula viwavi jeshi!!Kuna umasikini uliotopea!!

Hali hii ya umasikini wa wananchi,wakati mwingine huwa ina akisi aina ya viongozi wanaowachagua!Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya njaa,umasikini na umbumbumbu...Asiyeshiba,huwa hafikiri sawasawa
Viwavi was in Chamwino kwa Kibajaj ingawa Congwa ni njaa pia na huduma mbovu
 
Ndugai ni Spika wa hovyo haijawahi kutokea
Ni kweli! Adam Sapi Mkwawa, Pius Msekwa, Samwel Sita na Anna Makinda, jamaa hafiki hata 10% ya uwezo wa hawa wazee ingawa baadhi yao waliongoza bunge la chama kimoja! Huyu Ndugai ameachwa mbali hata na Zungu wa Ilala! Ni spika wa ajabu katika nchi zote za jumuiya ya madola!
 
Sawa tu mzee wangu, Ila kumbuka utakuja kustaafu tu siasa. Hakuna rangi utakayokuja iona kwa Sheria hizihizi uzitumiazo
 
Chakula kikuu cha Wagogo wa Kongwa wakati wa njaa huwa ni Viwavi jeshi,, huyu naye kuna uwezekano mkubwa alivibugia sana alipokuwa mtoto!!
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kwanza wajifunze kuandaa hotuba, haiwezekani mtu mmoja akaongea na katikati ya maongezi yake akajipinga bila ya kujua.
Kama kweli mbunge akiwa nje ya bunge hana kinga anakuwa raia wa kawaida! Ili uweze kumkamata kwa kutumia polisi. Kwa kifupi unataka kutuambia kuwa mbunge anakuwa mbunge akiwa bungeni tu, ila nje ya bunge ni raia wa kawaida.
Sasa kwanin akotoa maoni yake nje ya bunge unaenda kumhoji vip wakati alikuwa raia?
Unapojaribu kuongea Ba WaTz jua hauongei na mazuzu! Wapo watu wenye akili timamu na uelewa wa kutosha.
Iko wazi kuwa kuna taratibu unakiuka ndio maana naneno yako yana kinzana.
Ukiona sheria zinakinzana basi ama sheria au mtafrisi wa sheria amekosea! Kwa vile hizi sheria zilitumika tangu bunge hili la Tz lizaliwe basi Tatizo sio sheria bali ni wewe
 
Tatizo ni ukanjanja wa wanahabari, walishindwaje kumuuliza kwa nn yule DC na RC wa dar walivyoitwa wakaenda kwa muda wao, kwa nn hakuàgiza polisi wakawakamate?. Mahojiano ya Sikh hizi ni ya kujaza tu pages, bila kujali kama wameuliza kiufanisi na kupata majibu kwa niaba ya wananchi/ walaji!
 
Kongwa ni moja ya wilaya masikini sana,mwaka wa juzi,watu walipata njaa mpaka wakawa wanakula viwavi jeshi!!Kuna umasikini uliotopea!!

Hali hii ya umasikini wa wananchi,wakati mwingine huwa ina akisi aina ya viongozi wanaowachagua!Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya njaa,umasikini na umbumbumbu...Asiyeshiba,huwa hafikiri sawasawa
Aiseee.
 
Spika Ndugai amefunguka hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na kipindi cha East Africa Breakfast cha East Africa Radio na kusema kwamba Kubenea alikuwa ameitwa na Kamati ya Maadili lakini yeye akawa ametoroka kurudi Dar es Salaam jambo ambalo lililazimu akamatwe na baada ya kufikishwa kwenye kamati akawa ameshindwa kuhojiwa kutokana na kuonekana kuwa hayuko sawa kiafya.

Spika Ndugai amesema Kamati kuendelea kukaa ofisini kwa muda mrefu ni gharama sana ndiyo maana polisi walitumika kumkamata na siyo walifanya kumkamata kwa sababu walikuwa wanajua kuwa ni mgonjwa.

"Hakukamatwa kwa sababu ni mgonjwa, Kubenea alitakiwa aonane na Kamati ya Maadili, yeye akatoroka kwenda Dar es salaam. Kamati kukaa hapa ndani ya wiki moja ni mishahara ya kutosha ndiyo maana polisi wakaenda kumkamata, Kama alikamatwa akiwa mgonjwa ni bahati mbaya. "Hakukamatwa kwa sababu ni mgonjwa. Lakini kama ukiitwa kwenye mamlaka ya kimahakama lazima utoe ushirikiano kama unaumwa unasema tu na cheti cha daktari unaonyesha . Kama huumwi utakamatwa tu" amesema

Ameongeza kwamba "Kuwa mbunge hakukufanyi kuwa mtu mwenye mapembe. Lazima ufate sheria na taratibu zinavyotaka kwani mbunge ni sawa na mwananchi mwingine yeyote"

Katika hatua nyingine Spika Ndugai amefunguka na kusema Mbunge anakuwa na kinga kidogo pale anapokuwa kwenye ukumbi wa bunge na akitoka nje anakuwa kama mwananchi wa kawaida na hata kinga yake inakuwa imepotea.

Ameongeza pia yeye kuagiza Wabunge kukamatwa wanaofanya vitu vya kutengenezea bunge picha mbaya ni kazi yake kwa sababu kiongozi huyo tayari amelihusisha bunge hivyo kuagizwa watu wanaotoa maoni yao mitandaoni wahojiwe ni sahihi.

"Mbunge anayeropokea popote mimi nitamshughulikia tu, kwani ni kudhalilisha bunge letu. Haijalishi kwamba umezungumzia ukiwa nchi gani au mtandaoni sisi lazima tukuhoji na wewe utakuwa umepata fursa nzuri ya kujieleza kuhusu nini ulikuwa unamaanisha" ameongeza.

Chanzo: EATV

Ndungai hebu nikumbushe ile kauli yako ya kuagiza Mdee kukamatwa na kuletwa bungeni
 
Back
Top Bottom