Spika Ndugai amtaka Prof. Assad(CAG) kufika mbele ya kamati ya maadili vinginevyo atapelekwa kwa pingu

Na kwa kuongezea, ukisema bunge ni dhaifu maana yake serikali nzima ni dhaifu.

Kwa maana PM, AG, na cabinet nzima ipo bungeni, hii maana yake serikali nzima iko bungeni.


Sent using Jamii Forums mobile app
Alichokisema Assad ni kuwa Bunge limeonyesha udhaifu kwa kushindwa kusimamia matumizi na ubathilifu serikalini. Yeye anatoa report tu, wasimamizi ni Bunge. Vile vile, CAG kwa hakusema ni report za mwaka gani. Sasa Ndugai yeye anakuja kafura na kutetea Bunge hili ... wakati kuna report nyingi tu huko nyuma ambazo mpaka leo hatujasikia Bunge likihoji kama vile za Uuzaji wa Nyumba za serikali n.k.
 
kazi yake inamkataza kutoa maoni yake?wapo waliokiuka maadili ya kazi mpaka kuvamia vituo vya TV na bunduki walifanywa nini? maadili yanaonekana leo? wapo waliokiuka maadili ya kazi mpaka kutaka kupora passport za wageni walifanywa nni?
Walikuwa ktk kuwajibika na si kukiuka maadili....mawazo ya wengi ni kuwa ilikuwa uvamizi
 
Prof Mussa Assad kuna sehemu kakosea kwenye ile kauli, Prof anajua utaratibu wa bunge kuwa baada ripoti yake kuwasilishwa bungeni ilibidi ijadiliwe mwisho wa siku kamati husika ndipo alipoitwa Katibu mkuu wa hazina kipindi miezi 2 iliyopita hapa baadae kamati ikimaliza kazi yake itapeleka ripoti kwa CAG tena then CAG ataangalia then ataipa Bunge ripoti juu ya kile kilichowasilishwa na kamati husika katika sakata hilo.
we ulitaka asemaje babu
 
Ndugu Mussa Assad ni mfano muhimu wa kuigwa kwa Wahasibu wote Tanzania na kwingineko. Ukweli, Uadilifu ni chachu ya taaluma-Accountancy. Alichosema Mussa si kigeni wala si dharau. Hajafichua yaliyomo kwenye repoti. Hii niujumbe kwa viongozi, hasa wa biashara, ukidharau repoti yoyote ya Muhasibu ujue utaijutia, na usuilizi mali zimeenda wapi?. Ikiwa huielewi repoti, mwambie alieinukuu au Mwenye ueleo akufafanulie. Lengo ni kuitumia repoti kufanya uamuzi wa busara na kuchukua hatua kuondoa uozo. Tabia ya kufubaza Wahasibu inasababisha UFISADI, matokeo yake vijana wanakua wezi wa hovyo kabisa.
 
Mawaziri ni wanasiasa. Wengi wao hawajui chochote. Technical person unayetakiwa kumwamini ni CAG na wahasibu wakuuu wa wizara. Lakini shida ya wahasibu wa Wizara hawaruhusiwi kusema chochote kwa sababu siyo wasemaji wa Wizara.

Maelezo ya Polepole na Waziri ni ya kupuuza. Taarifa ya CAG huwa na vielelezo. Maelezo ya akina Pllepole huwa ni special kwaajilo ya wajinga
Wewe na Waziri nani mwenye data za kazi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndiyo ipo Sinema inachezwa hapo wameanzia kwa Spika lakini fainali ni mtukufu kutaka kumng’oa CAG ili aweke msukuma ndugu yake Daud Arbaty Bashite awe analinda ufisadi wake
Hapo sasa naanza kuliona hilo game. Ila awamu hii ni hatari kuliko ebola. Nakumbuka kuna madudu yalitakiwa kufanyika basi mchezo walioucheza nilicheka sana. Feleshi akiwa DPP alimuandama mtu mahakamani hadi ilitisha aisee. Lakini yule mtu akambwaga vibaya sana kwenye kesi ile na Feleshi akaamua kukata rufaa ingawa muda ulishapita ila alifoji barua kwa niaba ya serikali. Rufaa ikakubalika na kesi ikapelekwa mahakama kuu. Wakati huohuo Feleshi akapandishwa cheo na kuwa jaji wa mahakama kuu na ile kesi aliyoitolea amri ikakatiwe rufaa akakutana nayo yeye kama jaji sasa. Mambo yalitisha aisee. Alipokuwa DPP alichukua mpunga kutoka kwa mlalamikaji na akashindwa kesi na akakata rufaa na sasa akawa jaji kuhukumu kesi ile ile. Watu weweeee. Niendelee nisiendelee
 
Yule ni muislam safi akiwapa nondo sijui watajifichia wapi mfn matumizi ya kodi zetu kujenga chatu airport yaliidhinishwa kilingeni?,vipi wana kilinge wengine wanahudumiwa na wengine wamechinjiliwa mbali huduma mfno lissu anaweza jibu hoja hio?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kuwa jambo hili limevuta hisia za watu wengi, ingependeza kwa ungeitishwa mdahalo wa wawili hao wahojiane hadhani kuhusu majukumu ya ofisi zao na namna wanavyotimiza wajibu zao zilizoainishwa kweneye katiba
 
Back
Top Bottom