chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,383
- 24,939
Habari wakuu,
Ni majuzi tu hapa mkuu wa Mkoa Bw. Makonda alitukana bunge zima la JMT akiwemo Spika Ndugai na wabunge wa vyama vyote lakini spika akapata kigugumizi kumuita kwenye tume ya haki na maadili ya bunge mpaka wabunge walivyoshinikiza ndipo spika akasikia kwa shingo upande.
Haikuishia hapo bado spika hakutoa masaa 24 kwa makonda kwamba asiporipoti ndani ya muda huo akamatwe na polisi na kufikishwa mbele ya tume.
Leo hii Mh Mdee na M/kiti wa KUB Mh Mbowe wametamka maneno ya kawaida kabisa Mh Spika kakomaa, bado hakuishia hapo ametoa saa 24 waweze kuripoti.
Jamani jamani Spika acha ubaguzi, hii nchi ni yetu sote.
Unaposimamia haki fanya hivyo kwa usawa kwa pande zote.
Nawatakia sikukuu njema ya Karume day.