Spika ndugai alinena hiyo jana akiwa bungeni alitahadharisha sana kama taifa tuna hitaji ajira zinazo serikalini zizingatie uwiano ulio sawa yaani kimikoa, na hata Kidini.
Ametahadharisha endapo ajira zitaelemea kuajiri au hata kuteua watu wa aina mmoja kwa maana ya kimaeneo hata kiimani moja zaidi ni hatari sana kwa umoja na mshikamano wa taifa letu.
Nakubaliana nae asilimia 100 kuwa Taifa hili la Tanzania ni letu sote hivyo ni kweli na haipendezi na wala haifai, watu wa aina mmoja au kanda mmoja au hata wa aina mmoja ya imani ndio wawe wame hodhi nafasi zote za ajira au hata za kuteuliwa ktk nafasi za utumishi wa umma, jambo hilo lisipo angaliwa bila kuoneana aibu litaipasua Taifa letu siku za mbeleni, hivyo ni muhimu sana jambo hilo likazingatiwa ktk ajira na teuzi ili kuweka uwiano ulio sawa kwa mustakibali wa umoja wa taifa letu.
Ili kujenga na kuimarisha umoja na uzalendo ni muhimu ktk kuteua watumishi wa serikali uweke mseto wenye usawa mabao utawakilisha sura ya Taifa letu.
Kila mara kumekuwapo na manung'uniko ya watu wa Imani moja kuona wao wameminywa ktk nafasi za seriikalini na wengine wapo wengi zaidi kuliko wao, jambo hili sio zuri lazima litazamwe kwa nia njema, na jambo hili pia linahitaji utafiti.
Napendekeza kabla ya kutekeleza kila idara ya serikali yenyewe ifanye utafiti kwa watumishi wake wote ilio nao je?
Inazingatia Jografia ya nchi yetu? Je, kuna uwiano wa kiimani ktk nafasi mbalimbali?
Madhara ya kujaza kundi au aina ya watu fulani ktk utumishi wa umma ni hatari sana kwa umoja na uzalendo wa nchi yetu.
Asante Mhe. Spika kwa kutoa angalizo hilo la msingi na lenye nia njema ya kujenga ummoja wa nchi yetu. Ni matumaini yetu mamlaka za uteuzi na ajira zitalizingatia hilo.
UMOJA NI NGUVU, NCHI ITA JENGWA KWA UMOJA WETU NA SIO BAADHI YA WATU.
USHIRIKIANO WA WATU WOTE KTK KULIJENGA TAIFA LAO NI JAMBO MUHIMU SANA KWA UMOJA NA UIMARA WA NCHI, TUSIONEANE AIBU TUAMBIZANE UKWELI KWA MASILAHI YA TAIFA LETU.
Mungu ibariki Tanzania.